Kama tetesi hizi ni kweli viongozi Simba mtaharibu!

Kama tetesi hizi ni kweli viongozi Simba mtaharibu!

Viongozi wangu wa Simba waache ujinga ,wakubal wanatuchezea kwenye usajir ,huwez mbebesha lawama kocha kwa michezaji garasa Kama Ile .

Itafika muda hata sisi mashabiki tutawapa michezo kadhaa nyie viongozi mkishindwa Hilo mtaondoka hata kwa maandamano hapo clubuni..
Na kinachofuata saiz hakuna kuja uwanjan Hadi muache kusajili wachezaji wa mafungu.
Ni heri muwe mnasajil wachezaj hata watatu tu Ila wa maana kuliko huo ugoro wenu.
Mkimtimua kocha tambueni hamtakua mtatua tatizo ,tatizo ni kusajil na sio njaa njaa.

Nilianza kuwadharau viongozi wa Simba baada ya kushindwa kumnasa manzok kw amilion 400 ajab et Simba ni timu kubwa ,pumbavu zenu.
Endeleen kujaza takataka za million 50,60,70 alafu et tuna malengo ya nusu fainal .
Nawambia viongozi wote wa Simba soon mraanza kuchezea mayai viza popote mkipita
 
SImba hawana kikosi cha kupambana na timu kubwa kimataifa saivi. Hilo lipo wazi kabisa
Kuna kazi kubwa pale kiungo na pia tunahitaji kuwa shape upya Kapombe na Tshabalala wawe bora kwenye ukabaji then kushambulia iwe ni kitu cha pili lakini ulinzi kwanza.

Angalia Nabi alichofanya juzi ambacho kwasisi mashabiki wa Simba tungeua kocha. Umuweke nje Aziz K na sureboy aanze Mudadhiri? Alafu baadae umtoe Bangala aingie Gift?

Sisi Simba tunaharibu wachezaji sana sana, hata Chama kuna muda anacheza ki father na Sakho pia. Tunafanya makocha wawe waoga kwa hawa wachezaji!

Simba wote hadi mashabiki tunapaswa kubadilika, baada ya game ya Raja mashabiki wanataka timu apewe Mgunda! Hivi tuna funza vichwani sisi?

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Wakuu,

Matokeo ya weekend yametuvuruga Simba kuanzia mashabiki, wachezaji, makocha hadi viongozi! Ni kama hakuna anayejua tumekosea wapi.

Kuna tetesi mitandaoni kuwa kocha Robertinho amepewa game tatu kuamua hatma yake, Azam, Vipers in and out. Huu ni uganga wa kienyeji sio hesabu za mpira.

Unapompa kocha mechi tatu, wachezaji wana sehemu gani? Kama kwa unprofessional reasons wachezaji wakiamua kumhujumu kocha? Kwa kipimo kipi kuona huyu kocha mpya ni kocha wa ovyo?

Tunategemea management mlifanya tathimini ya kutosha na kuona huyu atafaa kutengeneza Simba itayotisha misimu kadhaa, Sasa imani yenu imefia wapi ghafla?

Simba main victims wa matokeo mabaya daima ni kocha na hii imejikita hadi kwa mashabiki! Tumeishia kuwa na lundo la makocha hadi aibu! Mnafikiri tatizo ni hao makocha au kichaka cha kuficha udhaifu wa viongozi?

Tusisahau hawa viongozi wamevurunda usajili bora hata Singida Big stars! Wachezaji wote waliosajiliwa wamevurunda! narudia wote kasoro Phiri! Ntibatokiza na Baleke ni dirisha dogo na hapo huyo Baleke hata Mazembe hawamtaki wanamtoa kwa Mkopo tu! Wamemleta Sewadogo hajacheza msimu mzima!

Huyu kocha akirudi leo Vipers alafu tukutane nae Feb 25 hatumuwezi ndio mjue hawa makocha wanaonewa tu. Hata hii Yanga iliyoimarika ni kumvumilia Nabi! Mashabiki wa Yanga walishaona Nabi hawezi hizi game lakini ilikuwa mihemko tu!

Viongozi njooni na mkakati mpya wa scouting ambao tutanunua wachezaji wa maana, lakini pia ili kuepusha hujuma badala ya kumpa kocha mkuu mechi 3 toeni game tatu kwa benchi lote la ufundi na pia wachezaji wakatwe maslahi yao tukitolewa ili uwajibikaji uwe timu nzima sio kuonea kocha mkuu tu.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Kocha anahusikaje sasa hapo. Kwanza kaletwa katikati ya msimu na hajui hata timu imeingiaje makundi.
Pili kwa aina ya wachezaji kama Kibu, Kapama, kanoute, Mkude Simba, Kyombo, babu Onyango, Bocco, sawadogo, Sakho na Inonga Simba haitoboi popote hata mfanyeje kuwa na hawa watu kwenye kikosi. Mtaendelea kuhudhuria kwenye mashindano mbalimbali badala ya kushindana. Tatu huko Dubai mlienda kufanya nini mechi 2 za kimataifa hamna hata goli moja la kufunga? Nne Bil. 20 ziko wapi?????
 
Hawa viongozi wa simba hawana akili timamu yani wanatusajilia akina sawadogo halafu wanamlaumu kocha?
Kuweni wavumilivu na ninyi khaaa! Mlitegemea muifunge Raja? Mbona Mancity, Madrid, Manu, Barca na Liverpool wanafungwa na mashabiki hawaji na kelele za kipumbavu kama hizi? Yaani kwa kiwango cha Raja unashangaa simba kufungwa? Mmeshasahau mafanikio ya kuwezeshwa kuingia makundi mara nne mfululizo. Kama mnafikiri kazi ni rahisi hivyo toeni pesa zenu msajili wachezaji mnaowataka. Kelele zote kwa ajili ya mifuko ya wenzenu, oneni aibu.
 
Wanamlaumu vipi kocha kwa team kama raja Casablanca ile team sio size yetu kabisa watoe uwendawazimu wao..

Badala ya kusajili vitu vya maana wao wanawaza ten percent na udananda kwenye usajili ndio matokeo yake haya kudhalilika utadhani tumejisaidia hadharani..
Afadhali wewe umeliona hilo. Kwakweli nawashangaa mashabiki wa Simba wanaoona ajabu kufungwa na timu yenye kiwango bora kama kile.
 
Unapompa kocha mechi tatu, wachezaji wana sehemu gani? Kama kwa unprofessional reasons wachezaji wakiamua kumhujumu kocha? Kwa kipimo kipi kuona huyu kocha mpya ni kocha wa ovyo?
Hivi unajua Kazi kubwa ya Kocha kwa hawa proffessionals wanaojua tactics na Technics inside out ni man management more than anything ?

Sasa kama wachezaji wake wakiamua kumuhujumu huoni kwamba atakuwa ameshapoteza 90% ya uwezo wake ambao ni Managing ?
 
Hatoi pesa na hili ni tatizo. Tumemkosa Manzoki kwa ubahili tuka risk aje dirisha dogo ili tukwepe kutoa mzigo. Adebayo tukashindwa kufika bei! Aziz K alikuwa kwenye rada ubahili wetu Yanga wakaingilia deal tukasusa kwa kujiona wakubwa!

Nani alimleta Mzungu? Okwa na Akpan hata Ihefu hawapangwi? Unaleta mtu ambaye kama Okwa ambaye hamfikii hata robo kijana wetu Ndemla si kichaa hiki!

Hawa friends of Simba kama wameshindwa kumfanya huyo tajiri atoe fungu la usajili nao waiache timu irudi kwa wanachama tujipange upya.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Who is Manzoki? Angefanya nini cha ajabu? Kama unamuhitaji sana siungeingia mfukoni na kutoa kiasi kilichowashinda Simba? Manzoki, Manzoki, Manzoki wakati hujawahi hata kumuona akicheza popote.
 
Wakuu,

Matokeo ya weekend yametuvuruga Simba kuanzia mashabiki, wachezaji, makocha hadi viongozi! Ni kama hakuna anayejua tumekosea wapi.

Kuna tetesi mitandaoni kuwa kocha Robertinho amepewa game tatu kuamua hatma yake, Azam, Vipers in and out. Huu ni uganga wa kienyeji sio hesabu za mpira.

Unapompa kocha mechi tatu, wachezaji wana sehemu gani? Kama kwa unprofessional reasons wachezaji wakiamua kumhujumu kocha? Kwa kipimo kipi kuona huyu kocha mpya ni kocha wa ovyo?

Tunategemea management mlifanya tathimini ya kutosha na kuona huyu atafaa kutengeneza Simba itayotisha misimu kadhaa, Sasa imani yenu imefia wapi ghafla?

Simba main victims wa matokeo mabaya daima ni kocha na hii imejikita hadi kwa mashabiki! Tumeishia kuwa na lundo la makocha hadi aibu! Mnafikiri tatizo ni hao makocha au kichaka cha kuficha udhaifu wa viongozi?

Tusisahau hawa viongozi wamevurunda usajili bora hata Singida Big stars! Wachezaji wote waliosajiliwa wamevurunda! narudia wote kasoro Phiri! Ntibatokiza na Baleke ni dirisha dogo na hapo huyo Baleke hata Mazembe hawamtaki wanamtoa kwa Mkopo tu! Wamemleta Sewadogo hajacheza msimu mzima!

Huyu kocha akirudi leo Vipers alafu tukutane nae Feb 25 hatumuwezi ndio mjue hawa makocha wanaonewa tu. Hata hii Yanga iliyoimarika ni kumvumilia Nabi! Mashabiki wa Yanga walishaona Nabi hawezi hizi game lakini ilikuwa mihemko tu!

Viongozi njooni na mkakati mpya wa scouting ambao tutanunua wachezaji wa maana, lakini pia ili kuepusha hujuma badala ya kumpa kocha mkuu mechi 3 toeni game tatu kwa benchi lote la ufundi na pia wachezaji wakatwe maslahi yao tukitolewa ili uwajibikaji uwe timu nzima sio kuonea kocha mkuu tu.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Tatizo mnapanda njugu mnataka kuvuna soya
 
Back
Top Bottom