Kama tetesi hizi ni kweli viongozi Simba mtaharibu!

Viongozi wangu wa Simba waache ujinga ,wakubal wanatuchezea kwenye usajir ,huwez mbebesha lawama kocha kwa michezaji garasa Kama Ile .

Itafika muda hata sisi mashabiki tutawapa michezo kadhaa nyie viongozi mkishindwa Hilo mtaondoka hata kwa maandamano hapo clubuni..
Na kinachofuata saiz hakuna kuja uwanjan Hadi muache kusajili wachezaji wa mafungu.
Ni heri muwe mnasajil wachezaj hata watatu tu Ila wa maana kuliko huo ugoro wenu.
Mkimtimua kocha tambueni hamtakua mtatua tatizo ,tatizo ni kusajil na sio njaa njaa.

Nilianza kuwadharau viongozi wa Simba baada ya kushindwa kumnasa manzok kw amilion 400 ajab et Simba ni timu kubwa ,pumbavu zenu.
Endeleen kujaza takataka za million 50,60,70 alafu et tuna malengo ya nusu fainal .
Nawambia viongozi wote wa Simba soon mraanza kuchezea mayai viza popote mkipita
 
SImba hawana kikosi cha kupambana na timu kubwa kimataifa saivi. Hilo lipo wazi kabisa
Kuna kazi kubwa pale kiungo na pia tunahitaji kuwa shape upya Kapombe na Tshabalala wawe bora kwenye ukabaji then kushambulia iwe ni kitu cha pili lakini ulinzi kwanza.

Angalia Nabi alichofanya juzi ambacho kwasisi mashabiki wa Simba tungeua kocha. Umuweke nje Aziz K na sureboy aanze Mudadhiri? Alafu baadae umtoe Bangala aingie Gift?

Sisi Simba tunaharibu wachezaji sana sana, hata Chama kuna muda anacheza ki father na Sakho pia. Tunafanya makocha wawe waoga kwa hawa wachezaji!

Simba wote hadi mashabiki tunapaswa kubadilika, baada ya game ya Raja mashabiki wanataka timu apewe Mgunda! Hivi tuna funza vichwani sisi?

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Kocha anahusikaje sasa hapo. Kwanza kaletwa katikati ya msimu na hajui hata timu imeingiaje makundi.
Pili kwa aina ya wachezaji kama Kibu, Kapama, kanoute, Mkude Simba, Kyombo, babu Onyango, Bocco, sawadogo, Sakho na Inonga Simba haitoboi popote hata mfanyeje kuwa na hawa watu kwenye kikosi. Mtaendelea kuhudhuria kwenye mashindano mbalimbali badala ya kushindana. Tatu huko Dubai mlienda kufanya nini mechi 2 za kimataifa hamna hata goli moja la kufunga? Nne Bil. 20 ziko wapi?????
 
Hawa viongozi wa simba hawana akili timamu yani wanatusajilia akina sawadogo halafu wanamlaumu kocha?
Kuweni wavumilivu na ninyi khaaa! Mlitegemea muifunge Raja? Mbona Mancity, Madrid, Manu, Barca na Liverpool wanafungwa na mashabiki hawaji na kelele za kipumbavu kama hizi? Yaani kwa kiwango cha Raja unashangaa simba kufungwa? Mmeshasahau mafanikio ya kuwezeshwa kuingia makundi mara nne mfululizo. Kama mnafikiri kazi ni rahisi hivyo toeni pesa zenu msajili wachezaji mnaowataka. Kelele zote kwa ajili ya mifuko ya wenzenu, oneni aibu.
 
Afadhali wewe umeliona hilo. Kwakweli nawashangaa mashabiki wa Simba wanaoona ajabu kufungwa na timu yenye kiwango bora kama kile.
 
Unapompa kocha mechi tatu, wachezaji wana sehemu gani? Kama kwa unprofessional reasons wachezaji wakiamua kumhujumu kocha? Kwa kipimo kipi kuona huyu kocha mpya ni kocha wa ovyo?
Hivi unajua Kazi kubwa ya Kocha kwa hawa proffessionals wanaojua tactics na Technics inside out ni man management more than anything ?

Sasa kama wachezaji wake wakiamua kumuhujumu huoni kwamba atakuwa ameshapoteza 90% ya uwezo wake ambao ni Managing ?
 
Who is Manzoki? Angefanya nini cha ajabu? Kama unamuhitaji sana siungeingia mfukoni na kutoa kiasi kilichowashinda Simba? Manzoki, Manzoki, Manzoki wakati hujawahi hata kumuona akicheza popote.
 
Tatizo mnapanda njugu mnataka kuvuna soya
 
Imeingia makundi mara nne mfululizo, wewe ndiye umeifikisha hapo? Kuweni mashabiki wastaarabu bhana khaa!
Ni mara tano mfululizo pamoja na Ile walipotolewa NUSU FAINALI na UD Songo kwa "Mkwapa"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…