OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Just for your information
Afrika ina maelfu ya timu zenye viwango tofauti tofauti. Kuna zenye viwango duni, viwango vya kati na vigogo. Nikikazia neno Vigogo namaanisha timu mfano wa Simba Sc kutoka Tanzania, East Afrika.
Kuna vigogo kadhaa tuseme 10 mpaka 15. CAF wamekaa wakaumiza vichwa majuma kadhaa wakitafuta vigogo 8 tu ili kushiriki Super League.
Baada ya vikao vya kitaalamu na uchambuzi hatimaye yakapatikana mavigogo zaidi 8. Yaani vigogo ambao hata ukiamshwa saa 8 usiku ukiambiwa taja vigogo 8 unavitaja chap unarudi kulala.
Kwa hiyo nakuambia kama timu yako ipo miongoni kwa vigogo wa ngazi za juu basi asikkubabaishe mtu. Atakubabaisha kwa lipi sasa. Mimi timu yangu ipo. Sio kosa langu timu yako kutokuwa kigogo.