Uchaguzi 2020 Kama TPSF ni wakweli, then, JPM, CCM itashinda ushindi wa kishindo cha ajabu! But for National Unity, TL ateuliwe Ubunge kuwafariji his sympathizers?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali, ikitokea Tundu Lissu ameshindwa uchaguzi huu kihalali katika Uchaguzi Mkuu huru na wa haki, jee tumchagize JPM, for the the sake of national unity, and to heal the nation, amteue Tundu Lissu kuwa Mbunge wa kuteuliwa katika zile nafasi zake kumi za uteuzi as a consolation prize na kuwapooza sympathisers wake watakao mpigia Tundu Lissu, compassionate and sympathetic votes?.

Hoja hii imeanzaje?
Saa hizi ni usiku wa manane, usingizi umekata ghafla nikaanza kuwaza uchaguzi na haswa kitu cha ajabu sana nilichokisikia leo kwenye mkutano wa Taasisi ya Sekta Binafsi, TPSF, pale katika ukumbi Kimataifa wa mikutano, JNICC, hivyo nikaamua kuendelea kuandika zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa".

Declaration of Interest
Naomba kuanza na declaration of Interest
Mimi Pascal Mayalla, japo ni kada wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, mimi sio kada fagilia, kada shangilia au kada piga makofi, mimi ni kada Mzalendo ambaye ninatanguliza mbele maslahi ya taifa. Hivyo ukiamua usinisome au usizingatie hoja zangu kwa vile sasa na mimi ni kada wa CCM, rukhsa kuishia hapa, nisije kukukerehesha nikakuharibia bure siku yako ya leo, na kwavile leo ni Jumatatu, ukiianza vibaya, utakuwa umeharibu wiki yako yote.

Kwa vile mimi ni muumini wa ukweli, na uwazi na ninaamini ukweli na uwazi ndio utaliponya taifa, sitaacha kuusema ukweli bayana ili kulisaidia kuliponya taifa langu, Pasco Mayalla licha ya sasa kuwa ni kada wa CCM, lakini Pasco bado ni yule yule juzi jana na leo, na hoja zake ni zile zile za kwa Maslahi mapana ya taifa.

Mkutano wa TPSF
Jana nimehudhuria mkutano wa Taasisi ya Sekta Binafsi, TPSF ambayo ni Taasisi Apex, yaani Taasisi Mwamvuli, an Umbrella Organisation, chini ya mwamvuli huo wa TPSF, kuna taasisi nyingine nyingi zinazo deal na sekta binafsi. Taasisi nyingine zote zilizo chini yake, jana zimemshukuru rais Magufuli kwa mambo makubwa, mazuri na ya kuonekanika aliyo yapanga, akayasema na kuyatenda kwa kuyafanya na kuyatekeleza, hivyo, wakuu wa taasisi zilizo chini ya mwamvuli wa TPSF, mmoja baada ya mwingine, jana walipanda jukaani na kunadi mazuri ya Magufuli kwenye tasisi zao, na kuahidi kuwa wametumwa na wanachama wao, kumpigia kura zote rais Magufuli wamemuhakikishia kura zote wanachama wote walio chini ya mwamvuli wa TPSF zitakwenda kwa JPM na wagombea wa CCM pekee, kwasababu aliahidi kwa kusema na sasa ametenda.

Hivyo kama ni kweli, hao wanachama wa Taasisi zote zilizo chini ya TPSF wameamua unanimously kumpigia kura JPM na CCM, then, kiukweli kabisa, rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, JPM, katika uchaguzi huu, yeye na CCM Itashinda kwa ushindi wa kishindo kikubwa cha ajabu kabisa kuwahi kutokea Tanzania, tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa ile 1992!.

Kwasababu nimeshuhudia chaguzi zote 5 za vyama vingi toka ule wa 1995, 2000, 2005, 2010, 2015 na sasa uchaguzi huu wa 2020 ni wa 6!, huko nyuma haijapata kutokea, hii ndio kwa mara ya kwanza, sekta binafsi nayo inatoa msimamo wa kisiasa, na kuzungumza kwa kauli moja unanimously kuunga mkono mgombea mmoja wa chama kimoja tuu cha siasa!.
Kwasababu hizo taasisi, sio taasisi za kisiasa na zinategemewa wanachama wake wako huru kujiunga na vyama vyovyote vya siasa na wako huru kuchagua viongozi wao wowote wanaowapenda kutoka vyama vyovyote, hivyo kama this time wameamua kwa kauli moja kutangaza hadharani kumchagua mgombea mmoja, JPM na kuichagua CCM tuu, huu sasa ni uamuzi wa kisiasa, then there is no way Tundu Lissu anaweza kupata kura zozote za maana!.

Hii ya TPSF, ni ukiondoa watumishi wa serikali ambao sote tunajua watamchagua nani, then TPSF encompasse

Hapo ni ukijumlisha Wafanyabiashara ndogondogo wote, wasiosajiliwa, wamachinga, mama lishe, wenye bodaboda wote, madereva, makundi ya wanawake, vijana na wenye ulemavu wote ambao kwenye list ya TPSF hawamo, ila jana pale ukumbini walikuwepo na wameahidi kura zote kwa JPM na CCM, hivyo kama hii ni kweli, then its as if rais Magufuli na CCM anakwenda kukomba kura zote za Watanzania wote toka makundi yote ya jamii, swali la kujiuliza ni kama ndio hivyo, nani atachagua upinzani?.

Kwa vile kabla sijajiunga siasa, nilistaafu kwanza uandishi wa habari, hivyo sikuweza kufuatilia ni lini hizi taasisi zote chini ya TPSF zilifanya AGM zake na kupitisha hizo resolutions kumsupport JPM na CCM, na kwa vile AGM zote ni open conferences zinatakiwa kutangazwa, kama kuna yoyote aliyesikia matangazo ya AGM, za taasisi hizo zikiitishwa, atujuze, unless AGM ziliitishwa na media zilialikwa ila kutokana na media kuwa too busy na politics, resolutions za AGM hizi hazikutangazwa hivyo hizo resolutions zote ni halali na ziko valid ila mimi ndio nikazisikia hiyo jana, lakini ikitokea, hakuna vikao vyovyote rasmi vilivyoitishwa na taasisi hizo, kupitisha hizo political resolutions kwenye taasisi zao, na badala yake ni vingozi tuu wa Taasisi hizo, wamefikia maamuzi ya kuwaamulia wanachama wao wamchague nani na chama gani na kuyatangaza maamuzi hayo hadharani kuwa wote wameamua kwa kauli moja, bila AGM, bila, bila kushirikishwa, then this leaves much to be desired!, na kwavile kura ni siri, then lets wait for JPM na CCM landslide victory, or surprises iwapo hawakushirikishwa!.

Sasa kwa vile kura zote zimeahidiwa kwa JPM na CCM only, lakini kwenye mikutano ya Tundu Lissu pia inajaza watu wenye too great expectations kuwa Tundu Lissu atashinda, bila kuonyesha atashinda kwa sera zipi, hoja zipi na kura zipi toka makundi gani ya kijamii, lakini kwavile na kiukweli kabisa kwa kilichomtokea Tundu Lissu kushambuliwa na risasi 16 za moto na akapona na sasa ni mgombea, huu ni muujiza mkubwa wa Mwenyezi Mungu na usikute ule umati wa watu katika mikutano ya Tundu Lissu ni umati wa kushuhudia tuu muujiza wa kupona kwa Tundu Lissu na sio umati wa wapiga kura, na akitokea kupata kura, then Tundu Lissu atapata kura chache za sympathetic na compassionate votes kwa maswahibu yaliyomfika.

Hivyo nashauri for the sake of national unity, kwasababu rais Magufuli anakwenda kukomba kura zote za Watanzania wote, haku kuna watu wana too great expectations na Tundu Lissu, mimi kama Mtanzania Mzalendo, katika wiki hii ya mwisho ya kampeni za uchaguzi, namuomba mgombea wetu na Mwenyekiti wa chama changu CCM, JPM, atangaze na ku ahidi wafuasi wa Tundu Lissu kuwa baada ya uchaguzi, atamteua Tundu Lissu kuwa Mbunge wa Bunge la JMT katika zile nafasi zake kumi ya uteuzi, ili Tundu Lissu angalau aweze kurejea Bungeni kuendelea kulichangamsha Bunge letu lijalo and at the same time, kuwafariji wale minority wote waliopanga kumpigia kura za sympathetic votes na compassionate votes, na hivyo to heal wafuasi na washabiki wake?.

Jee wenzangu mnalionaje hili?. si ni jambo jema?. Tena kama hoja za TPSF ni kweli, hii maana yake, Bunge lijalo litakuwa ni Bunge la CCM dominated house, hivyo sio tuu namuombea uteuzi Tundu Lissu pekee, bali namuomba JPM pia amteue, hata Zitto Kabwe, na Freeman Mbowe kuwa wabunge, amteue Benard Membe kuwa balozi, Maalim Seif yeye hana wasiwasi ni atakuwa Makamo kule Zanzibar hivyo wafuasi wake watatulia!.

Upendo, Amani, Utulivu na National Unity ni components muhimu sana kumsaidia Magufuli kwenye mitano tena yake.

Nawatakia Jumatatu njema.

Paskali
 
Pamoja na kutambua ushindi wa JPM upo wazi kabisa kutokana na ugeugeu na unafikir wa upinzani Ila bandiko lako limeegemea ktk kujipa promo na kujipendekeza zaidi.

Paskal tambua JPM anasifika kwa makubwa alofanya ndan ya muda mgupi lakini asifiwi kwa masifa ya mapambio ili mpate vyeo wengine.

Hebu safisha kalamu yako, kuna mengi JPM kafanya unaweza kuyachambua kwa uweledi na kulinganisha awamu zilopita,Mnashindwa na Masanja mkandamizaji anayeonesha kinaga ubaga nchi ilivyojengwa!

Nataka=njaa isikuharibu kabisa akili, JPM haitaji sifa za kujipendekeza kwa maslahi ya mtu, yule ni mzalendo na muumini wa uzalendo asili kabisaaa,na Sisi huku mtaani tunamkubali kinomaaaaa
 
Lisu ni mpango wa Mungu, hao wote wanamhadaa ili asiendelee na kampeni, wanamdanganya kuwa ameshashinda, Safi Sana, lazima neno la mwalimu Nyerere litimie, kwamba, wakuiondoa ccm ni ccm wenyewe, kwasasa vituko vyote vinavyoonekana ni Mpango wa Mungu kuweka bayana chanzo Cha ccm kuangushwa kwa fedheha 28 October,
Kama dola ya RUMI ilianguka, ccm haitoshindikana pia
 
Japo mada zako nyingi unaandika kama fumbo fumbo but kwa uelewa wangu bado umempgia kampeni Mgombea wa Chama chako kuna mistari umeonyesha wazi wazi. Jua kuwa siasa ni Sera na Sera huvuta watu..naongelea watu wenye akili Timamu. Ukifuatilia kampeni za Lissu wafuasi wengi ni vijana na vijana wengi ni wenye ufahamu. Vijana wengi ndy wahanga wa mfumo CCM.

Sera za Chama hiki kwenye maslahi ya msingi wa maisha ya vijana hazjajibu matatizo ya maisha yao. Nikuulize swali Paskali "wewe unamtoto kijana niambie ni Sera zipi za chama chako znamfavour mwanao zit aje hapa?

Kuhusu Hao.wenyewe hawawez kuwaongelea wananchi wenye kutaabika kwa mda mrefu. Vip kweny vikao vyao miili yao ilionyesha dhaifu hali kama vile mama zetu wanaosaka maji km kibao vjjn kule? Yaani Paskali majitu yalioshiba vitambi yaje yawasemee wananchi wenye taabu kwa miaka 45 nawe ukaamini?

Hao uliowataja hapa unajuaje kama wamefuatwa na kitengo cha propaganda ili ya mpigie Promo mtu fulani?

Miaka hii amukeni mjue wananchi wameamka kujua mbichi na mbovu. Tundu Lissu amenadi Sera kwa umakini wa hali ya juu sana. Ushindi wake unaweza kuwa wa wazi kabsa kabsaaa. Wewe Paskali unajua hili na wananchi wengi wanajua hili.

Wazo la Tundu Lissu eti kuteuliwa litoke wapi wakati ni mshindi wa waziwazi na watu wenye akili wanajua? Yaani wewe unataka kusema Wale waliomfanyia fitina zote na kumvua ubunge leo wajifanye wanapenda wampe ubunge waliomvua Bila sababu?? Hili likitokea mimi ntaamini amewashinda ila wanaamua kumtuliza ".

Wenye maamuzi kweny uchaguz ni wananchi si kikundi cha watu.

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
" kwa sababu rais Magufuli anakwenda kukomba kura zote za watanzania wote".

Haya maneno hayana ukweli, mimi ni Mtanzania ila kura yangu alishaikosa.

Kaka paschal TPSF ulitaka wasiunge mkono juhudi, lile swali lako la ikulu mpaka leo limekugharimu.

Wewe umewaombea kina Lissu, Zitto na Mbowe.
Rais awateue baada uchaguzi mkuu, mimi nakuombea kwa Mungu mwenye kiti cha enzi, Mr never told akishinda uchaguzi huu, akuteue.

Katika vitu vigumu hapa duniani, kimoja wapo ni kuutetea uongo. Si amefanya mambo mazuri atulie, Watanzania wana jambo lao Oktoba 28.
 
Kwanza nilishaamua kakudharau siku nyingi kwasababu ya Mambo matatu.

1. Kusema Lissu alijipiga risasi mwenyewe.

2. Kumsnichi kabendera mpaka akapatwa na yaliyompata.

3. Kuwa muongo wa makusudi kabisa hasa kwenye siasa za Tanzania.

Pengine ndio maana waliokujua walikupa kura moja tu na hiyo ndio sample ya kweli yoyote anayejiambatanisha na magu anavuna mabua wewe ni mfano dhahiri.

Swali langu:
Kama wewe ulipata one vote je magu si ni replica na reflection ya kura zako/yako? Hiyo CCM yako itashindia wapi? Hakuna mtu timamu kwasasa anataka kusikia habari za Magufuli labda mtumie dola ila kihalali hamshindi na mtashindwa kwa Kishindo.

Mnachokifanya Sasa ni last kiks of a dying horse mnatapatapa na hao mnaowaita tpsf kwanza wanawanafikia tu mioyo Yao Wala haiko nanyi.

Mitano tuliyowapa mmelitesa na kulinyanyasa taifa Nani awape Tena kura nendeni zenu huko wauwaji wakubwa nyie.
 
Uzuri hiki ni kizazi kingine kabisa, hakitawaliwi na propaganda wala vitisho vya kidictator. Hiyo mind games kuwa Magufuli atashinda sana ni ili watu wakate tamaa wasipige kura.

Ni hivi kura tutapiga vibaya sana, na tunataka mshindi halali atangazwe. Hatuna tatizo la kushindwa, ila tunataka mshindi halali atangazwe. Isitoshe Tundu Lisu hahitaji vyeo vya dezo. Tunasubiri uchaguzi utakaojaa dhuluma na hadaa ya wazi ili CCM watangazwe washindi.
 
Na kujikomba kote kwa magu wanaccm wenzie walimpa kura moja tu hilo pekee ni jibu tosha kwamba amechagua fungu bovu.
 
Kwani imekuwa block vote? Kura ni ya kila mtu mmoja mmoja na kila mtu anajua kura yake ampe nani, hizo taasisi zinaweza kuwashawishi watu kumpigia kura mtu fulani, lakini bado uamuzi wa kumchagua kiongozi unabaki kwa mpiga kura mwenyewe, na wapiga kura wengi nadhani ni watu wasiyo na ajira rasmi.

Na kuna wale ambao jamaa zao wameathiriwa na "vyeti feki, tumbua tumbua" wasiyo ongezwa mishahara wala kupandishwa madaraja. Hivyo kura ni siri ya mtu tusubiri siku ya kupiga kura, kujumlishwa na kutangazwa matokeo ya uchaguzi, what is needed is free, fair and peaceful election.
 
Kwa sasa tumalize uchaguzi, leo Lissu yupo wapi?
 
Mayalla huwa nakuita mjinga tena sana. Post Kama hii ni upuuzi mtupu kwa mtu wa umri wako. Magufuli hajafanya chochote zaidi ya miradi ya ujanja ujanja yenye kila harufu ya wizi. Uonevu na visasi. Kifupi hafai. Lissu hana doa hana kashfa hata ya mahusiano kama Magufuli na kina sundi etc mv Bagamoyo, nyumba za serikali hivyo vyote ni uchafu.

Sasa tunajua ataiba kura na kujitangaza ila nakuapia atakimbilia Burundi ndani ya awamu ijayo mark my words. We are pressed to the wall.

Hata sisi ndani ya CCM tunataka ashindwe ili tumtoe uenyekiti sababu amekipasua Chama kabisa. Huo ndio ukweli wee Mayalla mjinga.
 
Lissu angetaka dezo angeshavipataka, huyu mchumia tumbo mganga njaa asitutoe kwenye reli.
 
Tunaishi kinafiki, TPSF ni sector ilioumizwa sana na awamu hii hatujasahau kodi kufukua makaburi ya zamani, fungia viwanda,fine za ajabu, kutaifisha mifugo, machinga wapo mbele ya maduka ya watu, kudharauliwa, lugha tata "nakamua mafisadi na majizi, wataishi kama mashetani.."

Kilichofanyika na TPSF ni sawa na ufanyalo P "funika kombe mwanaharamu apite" "Jifanye mjinga siku ipite" ... waswahili walisema.
 
Ndugupaskali

Lissu ana kura zote za haya makundi

1. Watumishi wote wa umma ikiwemo TISS na polisi
2. Wakulima
3. Machinga
4. Mama Ntilie
5. Vijana wasio na ajira maalumu
6. Wanafunzi wa elimu ya juu
7. Vijana waliokosa ajira kabisa
8. CCM wote wasiofadika na mfumo
9. Chadema wote
10. Viongozi wa dini zote
.
.
.
20. Waislam
 
Mkuu
Mkuu sijui nikuamkie shkamoo au nikuombee baraka!

Unajua jamaa anapata majibu humuhumu hii ndio sample ya matokea tunaanza na uzi wake mwenyewe kumhakikishia kwamba anaongea uongo kubwa j huyu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…