Kama tu Injinia Hersi wa GSM na Yanga SC yake anaonyesha 'Udhaifu' huu kwanini Yanga SC isiwe na Matokeo mabaya na ya hovyo hovyo?


Tatizo watu wameanza kupenda timu badala ya mpira…. Na watu wanapenda kusikia propaganda badala ya uwalisia pia wanapenda story za vijiweni ulikuwa progress ya timu… GSM wamefanya makubwa sana kuliko hata kuchukua ubingwa… Yanga ina Kambi ya Kisasa kuliko hata Simba niwaambie
 
Tatizo mashabiki wa Mpira wanapenda kusikia maneno ya kuropoka kama ya manara au Masau bwire lakini wakisikia maneno ya mipango kutoka kwa Eng Hersi Said, Popat wanaona kama wanapiga kelele… lakini kiukweli mpira wetu unaitaji sana watu wana namna hii ili kuufanya mpira wetu uwe wa kisasa zaidi… Welldone Eng Hersi Said
 
Hakuna watu wana mipango mikubwa pale Yanga kama GSM wamefanya makubwa sana…
 
Hakuna watu wana mipango mikubwa pale Yanga kama GSM wamefanya makubwa sana…
Nakubaliana nawe kabisa kuwa GSM wamefanya makubwa sana Yanga SC ikiwemo Kuwadanganya wana Yanga SC kuwa wameuza Jezi 80,000 kwa Kipindi chote badala ya 250,000 za ukweli ( idadi kamili )

Ni kweli kabisa Mkuu GSM wamefanya makubwa Yanga SC kwa Wao kuuza zaidi ' Merchandisers ' nyingi zenye Logo ndogo ya Yanga SC na Logo kubwa ya GSM huku Klabu ikiwa haijapata mapato yoyote yale katika Akaunti yake.

Ni kweli kabisa Mkuu GSM wamefanya makubwa Yanga SC kwa Wao kutumia Mgongo wa Jina la Yanga SC ' Kujipromoti ' zaidi katika Media na Mitandao mbalimbali hadi kupata ' Mileage ' kubwa kuliko ambayo Yanga kama Klabu ingetakiwa kuipata.

Ni kweli kabisa Mkuu GSM imefanya makubwa Yanga SC kwa Kuwakalisha katka Hoteli Kubwa Mbili za Regency Mikocheni na huko waliko sasa Avic Town ambako kote huko GSM na Injinia Hersi Said wana ' Ubia ' napo ( nao ) Kibiashara hivyo Yanga SC kama Klabu wakitakiwa Kulipa kumbe hawajui tu kuwa ' indirectly ' wanawalipa na Kuwatajirisha zaidi GSM na Hersi huku Yanga SC ya Mwenyekiti Dkt. Mshindo Msolla kila Siku ikilia Njaa ( Ukata ) tu na Wachezaji kucheleweshewa Mishahara na Madeni yao mbalimbali.

Unataka niendelee Mkuu / niishie hapa?
 

Kwa hiyo unataka kusema GSM anaibia Yanga sio? Kwa hiyo GSM haina covarage kubwa bongo mpk wapokuja kuidhamini Yanga sio? Sasa kama GSM wanaibia Yanga ebu sema Yanga imeingiza kiasi gani yenyewe kama yenyewe kama hata tunaweza kumlipa Kabwili salary? Watz tusiwe wajinga sisi wenyewe tunashindwa kufanya mabadiliko ya haraka ya uwendeshaji ili hawa matajiri wakija tuwabane….
 
Usinipotezee muda hauna unachokijua.
 
Tatizo amezidi ' Kudanga ' na Waarabu.
[emoji134][emoji134][emoji134][emoji119][emoji119][emoji119]
Hata kama angekua afanyi hizo mambo ila huyo mdada hana analojia katika michezo, yaani ni tupu labda apewe vipindi vya taarabu ndo anaweza....
 
Usinipotezee muda hauna unachokijua.

Kwa hiyo wewe na story za kijiwe cha kahawa mnazo danganyana kila siku…. Yaaani watu hawajui hata kila net profit ya jezi moja lakini anashupalia…. Kila story za vijiwe vya kahawa
 
Ninachokumbuka pia alijibu kuwa Yanga imetinga nusu fainali kombe la Azam Federation Cup na akaahidi kuwa Yanga ndio itakuwa Bingwa.

Pia akajisifu kwa Yanga kutwaa kombe la Mapinduzi.

Kuhusu hilo swali la Tunu ni kweli alikwepa kulijibu makusudi ili asiingie kwenye mtego wa kuisifia Simba.
 
Wewe hersi anakuhusu nini?kama ni dhaufu tuachie sisi yanga kinakuwasha mku ndu nini
 
Ndugu yangu Genta umeongea point safi kabisa, waandishi na watangazaji wengi wa habari za michezo hawana weledi ktk kuhoji na kuuliza maswali ya msingi kwa wahojiwa,,, wanapuyanga tu

Ila binafsi ktk sekta hii bado naendelea kumpa kongole sana mwanadada SALAMA JABIR

Anajua kuhoji maswali ya msingi, anajua namna ya kumfanya mhojiwa arudi ktk main point/swali aliloulizwa, ana maarifa mapana ya mambo mbalimbali (current issues) ndio maana anahoji kuanzia wanamuziki, wanasiasa, wanamichezo mpaka waigizaji etc

SALMA JABIR popote ulipo nakupa KONGOLE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…