Kama tumemuacha huru aliyesababisha vifo pale Moshi huyu 'Mfalme' wa Mwanza tunamtesa kwa lipi?.

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,311
Reaction score
9,027
Mimi ni miongoni mwa wapingaji wakubwa wa hizi shughuli za kiroho zinazofanywa na Wajanja wachache na kunufaika kwa migongo ya Wengine...na nilitamani sana kuona lile lililotokea pale Moshi wakati ule likifikia kutoa haki kwa wale Wahanga.

Hivi karibuni kumetokea tukio pale Mwanza na sasa Muhusika Mkuu anashikiliwa na Vyombo vya dola.

Siungi mkono vitendo vyovyote vya uvunjaji wa sheria lakini natamani kujua ni sababu zipi haswa zimetumika kuachana na tukio lilosababishia vifo na sasa tunatumia nguvu kupambana na huyu aliyefungia Watu ndani kwake.

Kama yule hakukosea vipi huyu kakosea?, ni lipi kubwa kati ya kusababisha kifo na kufungia Watu?.

Niombe tu kwa Mamlaka zetu ifike mahali kuwe na utaratibu wa kufuatilia hizi shughuli zote zinazofanyika kwa mgongo wa imani, ni muhimu kujua ni nini kinaendelea nyuma ya pazia badala ya kusubiri kundi kubwa la Watu wakishadhulumiwa ndio tunashtuka muda ukiwa umeshapita.

Mamlaka zifanye kazi kuzuia matatizo na mafundisho potofu badala ya kukaa pembeni kwa kutishiwa na kauli ya "Imani za Watu".
 
Ni kweli, ila ngoja waje wafuasi wake wa mkanyaga mafuta utajua hujui.

Tumekuja tayari! Nani analeta usumbufu hapa tumshughulikie mara moja? Yale mafuta yana upako wa kweli!

Mimi mwenyewe nilipo yakanyaga tu hayo mafuta siku ile, nikajikuta kwenye akaunti yangu ya benki zimeingia milioni 20! Na mpaka leo hata sijui zilitoka wapi!
 
Sio kazi ya serikali kuzuia mafundisho potofu ya kiimani yasiyovunja sheria za nchi, huko ni kuingilia haki za raia.
 
Sababu ni mwanamke kujiita mfalme na nchi ina Rais wa kike daah maisha haya
Nilishangaa wananchi wanasema mbona hatumii biblia au Quran, nikajiuliza kwani Wahindu, Mabudha mbona hawatumii hivyo vitabu na hamhoji.
Zumaridi yeye kaanzisha dhehebu lake, lingekuwa limeanzishwa na wahindi au wazungu ingeonekana poa tu.
 
Sio kazi ya serikali kuzuia mafundisho potofu ya kiimani yasiyovunja sheria za nchi, huko ni kuingilia haki za raia.
Sidhani kama ni sawa kukaa pembeni na kuacha Raia kuambiwa watapata maisha bora bila kufanya Kazi.

Kwamba watapata mahitaji yao kwa miujiza na Mamlaka ibaki inaangalia tu?.

Au ajitokeze anayewaaminisha Wafuasi wake kuwa wote wasiomuamini yeye ni Maadui tupambane nao na Mamlaka ibaki inaangalia tu?.
 
Kwani inashindikana kupata maisha bora bila kufanya kazi?
Wengi tu duniani wana maisha bora bila kufanya kazi.
 
Kuna watu Corona ilipoingia waliwaambia raia wafunge na kusali siku tatu ili janga liondoke, mbona hilo hushangai?!
Sidhani kama ni sawa kukaa pembeni na kuacha Raia kuambiwa watapata maisha bora bila kufanya Kazi.

Kwamba watapata mahitaji yao kwa miujiza na Mamlaka ibaki inaangalia tu?.

Au ajitokeze anayewaaminisha Wafuasi wake kuwa wote wasiomuamini yeye ni Maadui tupambane nao na Mamlaka ibaki inaangalia tu?.
 
Yule ana bifu na police mahakama itamuachia Hakuna kesi pale hazina ushahidi. Police walienda kumvamia nyumbani kwake na kutaka kumkamata bila utaratibu akawagomea so wanamkomoa
 
Mimi ni miongoni mwa wapingaji wakubwa wa hizi shughuli za kiroho zinazofanywa na Wajanja wachache na kunufaika kwa migongo ya Wengine...na nilitamani sana kuona lilotokea pale Moshi wakati ule likifikia kutoa haki kwa wale Wahanga.

Hivi karibuni kumetokea tukio pale Mwanza na sasa Muhusika Mkuu anashikiliwa na Vyombo vya dola.

Siungi mkono vitendo vyovyote vya uvunjaji wa sheria lakini natamani kujua ni sababu zipi haswa zimetumika kuachana na tukio lilosababishia vifo na sasa tunatumia nguvu kupambana na huyu aliyefungia Watu ndani kwake.

Kama yule hakukosea vipi huyu kakosea?, ni lipi kubwa kati ya kusababisha kifo na kufungia Watu?.

Niombe tu kwa Mamlaka zetu ifike mahali kuwe na utaratibu wa kufuatilia hizi shughuli zote zinazofanyika kwa mgongo wa imani, ni muhimu kujua ni nini kinaendelea nyuma ya pazi badala ya kusubiri kundi kubwa la Watu wakishadhulumiwa ndio tunashtuka muda ukiwa umeshapita.

Mamlaka zifanye kazi kuzuia matatizo na mafundisho potofu badala ya kukaa pembeni kwa kutishiwa na kauli ya "Imani za Watu".

Hakuna kipimo au mfumo wa kuthibitisha yapi ni mafundisho sahihi yapi si sahihi.
Na sahihi kwa nani.
 
Nilishangaa wananchi wanasema mbona hatumii biblia au Quran, nikajiuliza kwani Wahindu, Mabudha mbona hawatumii hivyo vitabu na hamhoji.
Zumaridi yeye kaanzisha dhehebu lake, lingekuwa limeanzishwa na wahindi au wazungu ingeonekana poa tu.
Hawezi tumia biblia au quran sababu si Mkristo wala si Muislamu.
 
Kuna watu Corona ilipoingia waliwaambia raia wafunge na kusali siku tatu ili janga liondoke, mbona hilo hushangai?!
Corona imetoka kuzimu na sasa haipo ilikuja kwa watu maalumu Ili kujaza pengo la kuzimu baada ya kuzimu kupoteza watu wengi sana ilipopigwa kombora zito likauwa wengi kuzimu.
Shetani akaamua kuleta corona Ili kuvuna kwa mda mchache watu wengi.
Aliyeileta corona duniani ni daktari agent na ..... nchini China taifa linalomuabudu shetani,then ilipofumuka akarejea kuzimu. Kuzimu imejaa washaziba pengo corona haipo.
 
Kama wewe unaamini hivyo hata Zumaridi, Gwajima na Mwamposya wana haki ya kuamini hivyo wanavyoamini.

Back
Top Bottom