May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Mimi ni miongoni mwa wapingaji wakubwa wa hizi shughuli za kiroho zinazofanywa na Wajanja wachache na kunufaika kwa migongo ya Wengine...na nilitamani sana kuona lile lililotokea pale Moshi wakati ule likifikia kutoa haki kwa wale Wahanga.
Hivi karibuni kumetokea tukio pale Mwanza na sasa Muhusika Mkuu anashikiliwa na Vyombo vya dola.
Siungi mkono vitendo vyovyote vya uvunjaji wa sheria lakini natamani kujua ni sababu zipi haswa zimetumika kuachana na tukio lilosababishia vifo na sasa tunatumia nguvu kupambana na huyu aliyefungia Watu ndani kwake.
Kama yule hakukosea vipi huyu kakosea?, ni lipi kubwa kati ya kusababisha kifo na kufungia Watu?.
Niombe tu kwa Mamlaka zetu ifike mahali kuwe na utaratibu wa kufuatilia hizi shughuli zote zinazofanyika kwa mgongo wa imani, ni muhimu kujua ni nini kinaendelea nyuma ya pazia badala ya kusubiri kundi kubwa la Watu wakishadhulumiwa ndio tunashtuka muda ukiwa umeshapita.
Mamlaka zifanye kazi kuzuia matatizo na mafundisho potofu badala ya kukaa pembeni kwa kutishiwa na kauli ya "Imani za Watu".