Kama tumeshindwa kuiondoa CCM kwa kura sasa tufanyeje?

Kama tumeshindwa kuiondoa CCM kwa kura sasa tufanyeje?

Baada ya kuishinda CCM katika kura na matokeo kuwa mazuri kwa upinzani na yaliyojaa ushindi,bado CCM wametumia uchaguzi huo huo kujitangaza washindi ?
Je kuna ushauri wowote ,maana uchaguzi wapinzani waliudhibiti kisawasawa na ushindi ukawepo mezani imebaki kutangazwa tu ,Lakini bado CCM akatumia mwanya wa utangazaji kutangazwa mshindi .
Tukachwa na kauli CCM sio mshindi halali wa uchaguzi kauli hadi leo imo vinywani kwa wapinzani.
Je kifanywe nini ili hata hili pengo laUtangazaji nalo lizibwe ?
Ni ngumu sana kuiondoa ccm madarakani kama maaskari (wanajeshi) na wananchi watakuwa hawajaamua kufanya hivyo!
Kumbuka kwamba ccm Wana vyombo vya dola hasa polisi na TISS. Na wanatumia ugumu wa ajira kuwahonga ajira vijana waliokwama kimaisha ili tu wakati wakiwataka waweze kuwatumia wapendavyo!
 
Acha uongo na ujinga
Sibishani na vijana waliojifunza siasa kupitia propaganda za mitandaoni.. Ukijua kutafsiri picha na muonekano wake utaelewa vizuri nilichokuandikia. Hii ndio CCM usioijua kijana!

images (20).jpeg


2878995_images_9.jpeg


images (23).jpeg
 
Njia iliyobaki ni wananchi kuacha kufanya manunuzi ya bidhaa kwa fujo... Kama ulikuwa unatumia bando elfu tano kwa siku Anza kutumia buku.. bia kumi kunywa tatu.. watoto badala ya soda watengenezee juice.. Gari ulikuwa unapiga misele mingi unapunguza nk... Serikali itakosa Kodi watapiga magoti wenyewe .. Kuna nchi ilifanya hivi viongozi waliufyata.. Ila sisi wanafiki hatuwezi...
 
Back
Top Bottom