Kiimani na hata mahala pengi tu utawasikia Watu wakisema kwamba Mwenyezi Mungu hakosei, hajakosea na kwamba huwa hakosei na wengi wetu ama Kiuwoga au ' Kimbumbumbu ' tu au kwa kuwa wa ' hovyo hovyo ' katika Kufikiri tayari tumeshaaminishwa hivyo.
Sawa kama kweli Mungu hakosei sasa inakuwaje kila mara huwa tunaisikia hii Kauli ambayo nainukuu hapa " Hakuna Binadamu aliyekamilika chini ya Jua, Mwezi au Dunia hii ". Je hapa tushike lipi au tuelewe lipi?
Na kama Wote tunakiri kwamba Mwenyezi Mungu hakosei katika ' Uumbaji ' wake na Sisi Wanadamu ni mfano wake tosha iweje tena leo tunasema hadi kwa msisitizo kabisa kwamba Binadamu wote hatujakamilika?
Tujadili na Karibuni katika huu ' mjadala ' ambao nawahitaji tu wale ambao wamebarikiwa Critical Thinkig na Logical Reasing ya kutosha wachangie na nimetahadharisha mapema tu katika ' Headline ' kama unajijua au kujihisi huna huo uwezo tafadhali tusichoshane na pita zako tu mia.
Nawasilisha.