Kama tunaaminishwa kuwa Mungu hakosei inakuwaje hakuna kiumbe mkamilifu chini ya jua?

Kama tunaaminishwa kuwa Mungu hakosei inakuwaje hakuna kiumbe mkamilifu chini ya jua?

Trust me, I'm not an atheist!

Ninaamini uwepo wa Mungu kama nguvu kubwa iliyo umba ulimwengu na vilivyomo.

Tatizo ni pale ninapofungua vitabu vitakatifu vinavyosemekana kua neno la Mungu then nakutana na vitu vyenye kuleta mkanganyiko kuliko suluhu!

Mkuu, naamini Mungu ana mfumo wake (DINI) ambao anaendesha mambo yake kwa taratibu zake, na ni muhimu binadamu kufuata mfumo huo. Kama vile software kwenye kifaa cha kielektroniki.

Sasa sijaelewa unaponiambia nisiwe religion centred mkuu!
Ungetoa mfano.Ni eneo gani katika biblia linakuchanganya?
 
mkuu nilikua sina uhakika kama nimeku-follow but today nimehakikisha nikakuta sijakufollow so soon utaona notification yangu....keep it up...you're a truly G.THINKER
Maandishi murua sana haya mkuu, muhimu niyatafakari kwa kina, Nakushukuru kwa kuniamini na kunifollow mkuu. I'll follow you back.

Umenikosha!
 
"Hakuna binadamu aliyekamilika" hii ni kauli ya binadamu pale tunapokuwa tumekosea hivyo tunataka huruma upande wa pili. Haina mahusiano ya Mungu kwenye kauli hiyo.
 
Kwa hiyo kwa ujumla msimamo wako ukoje mkuu juu ya Dini na Mungu?
Ninaamini uwepo wa Mungu na ukuu wake.

Napata ukakasi kuhusu dini tulizonazo na misingi yake. Pia vitabu tunavyoviita vitakatifu ambavyo vimeandikwa na wanadamu wenzetu ndivyo vinavyonipa wasi wasi zaidi.

Kwa kiasi fulani ninaamini hivi vitabu vimeandikwa na watu fulani kwa lengo maalum kutimiza matakwa yao. Na ndio maana vinakua na mapungufu yenye kuleta mkanganyiko.

Angeandika Mungu mwenyewe kusingekua na hoja zinazopingana.


Tu cut the long story short, I believe in God, but i think religion is a human project!

I rest my case!
 
Kiimani na hata mahala pengi tu utawasikia Watu wakisema kwamba Mwenyezi Mungu hakosei, hajakosea na kwamba huwa hakosei na wengi wetu ama Kiuwoga au ' Kimbumbumbu ' tu au kwa kuwa wa ' hovyo hovyo ' katika Kufikiri tayari tumeshaaminishwa hivyo.

Sawa kama kweli Mungu hakosei sasa inakuwaje kila mara huwa tunaisikia hii Kauli ambayo nainukuu hapa " Hakuna Binadamu aliyekamilika chini ya Jua, Mwezi au Dunia hii ". Je hapa tushike lipi au tuelewe lipi?

Na kama Wote tunakiri kwamba Mwenyezi Mungu hakosei katika ' Uumbaji ' wake na Sisi Wanadamu ni mfano wake tosha iweje tena leo tunasema hadi kwa msisitizo kabisa kwamba Binadamu wote hatujakamilika?

Tujadili na Karibuni katika huu ' mjadala ' ambao nawahitaji tu wale ambao wamebarikiwa Critical Thinkig na Logical Reasing ya kutosha wachangie na nimetahadharisha mapema tu katika ' Headline ' kama unajijua au kujihisi huna huo uwezo tafadhali tusichoshane na pita zako tu mia.

Nawasilisha.
Mkuu, ni kweli Mungu hakosei, alimuumba binadamu kwa mfano wake yaani mkamilifu, ukamilifu wa binadamu uliishia pale binadamu alipoanza kutenda dhambi, mtu asiye na dhambi ni mkamilifu mbele za mwenyezi Mungu ila mbele za binadamu mwenzie ndo utasikia kuwa hakuna binadamu aliye mkamilifu kwa maana binadamu tunatenda sana dhambi isipokuwa watoto wadogo tu wasiojua hili wala lile ndo wakamilifu Marko 10:14 Yesu anawaambia wale watu waliokuwa wanawazuia watoto kuingia kwenye mkutano "waacheni watoto wadogo waje kwangu msiwazuie, kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao" hapa anamaanisha kuwa watoto wadogo ni wakamilifu yaani Mungu kawaumba kwa ukamilifu na ndo maana ni rahisi kwao kuumiliki ufalme wa Mungu, lakini kwa mtu aliyefika umri wa kujitambua ndo ukamilifu humtoka maana huanza kutenda dhambi kwa namna yoyote ile
 
Kwenye bibilia, kuna sehemu nyingi tu ambapo Mungu kafanya matukio na kisha kusikitika, kuonyesha kuwa alikosea, mfano ni pale alipoleta gharika, alisikitika na kudai kuwa hatateketeza tena dunia kwa maji wala kwa moto...

Lakini ukiacha hilo, inaonekana Mungu kila anachofanya anakosea tu na alikosea from the very beginning, hakupanga kabisa kumuumba Eva(Hawa), ila alipomuumba Adam, akagundua kuwa amekosea kumuumba bila msaidizi, ikabidi Amubongonyoe mbavu ili kumuumba Eva, pia huyo Mungu hakupanga Adamu na hawa wazaliane, alitaka waishi tu humo kwenye bustani, shetani kamzidi ujanja, kaenda kutoa siri, ikabidi abadilishe mipango, akawafukuza kwenye bustani na kuwaambia watakula kwa jasho....

Usisahau pia kuwa shetani aliyetoa siri nae aliumbwa na Mungu, Mungu akiamini kuwa huyo shetani atakuwa malaika mtiifu kwake, lahaula!! sivyo hivyo, shetani kabadilika hadi wakashindwana, kaamua kumtupa duniani... Kuna visa vingi ambavyo vinaonyesha kuwa Mungu kila kitu anakosea, na mambo yalivyo, sivyo ambavyo alitaka yawe, ni kana kwamba mambo yalimshinda, akayaacha yaende alijojo.

Hii ya kusema kuwa Mungu hayupo kwenye logic wala reasoning, ni kauli tu ya kujaribu kupambaza watu, ili waache kufikiri, wakubaliane na vitu vya kutunga tu, ambavyo vinajicontradict vyenyewe.
Hakuna binadamu aliekamilika hiyo kauli ni sawa na hii ya "mgaa gaa na upwa hali wali mkavu" zote hizi ni kauli za wahenga tu.Hivyo zipuuze tu!

Mungu katuumba kwa ukamilifu mkubwa saana maana kama matako angeyaweka kifuani tungesema kakosea sababu hatuwezi kukaa comfortably but akayaweka pale nyuma yakiwa na nyama nyama mfano wa spongy sehemu sahihi kabisa ili tukae comfortably na tukiona anayo mbebe tunamsifu kwa kuyaita "Neema za Allah " tuyaite msambwanda kwa lugha za majanki.

God is the best designer ever.
 
"Hakuna binadamu aliyekamilika" hii ni kauli ya binadamu pale tunapokuwa tumekosea hivyo tunataka huruma upande wa pili. Haina mahusiano ya Mungu kwenye kauli hiyo.
Swadakta...
🙂🙂🙂
 
Ukiwaza sana kuhusu MUNGU mwisho wake utakufuru,

Kuna thread ilisha wahi tupiwa humu kwenye Jf, MUNGU si chochote na SHETAN si chochote.

Tunatumia kauli/Maneno haya
Binadamu haja kamilika ni pale tu kupunguza ukakasi katika familia/jamiii na n.k kwa mtu anaweza fanya kosa ili kupoza lazima kuna misamiati itumike katika jamii iliyozungukwa.

Ukija upande wa mtu/watu wakitokea wamekufa/fariki lazima tutumie maneno haya MUNGU HANA MAKOSA, TULIMPENFA LAKINI AMEPENDA ZAIDI YEYE MUUMBA, lakini ukirudi kutafakari kwa kina MUNGU hawezi akakuumba na ukazaliwa, na ndani ya mwaka mmoja au miaka miwili unakufa eti MUNGU kakupenda, MUNGU akubebe ukiwa na miaka miwili au mitatu ukienda mbinguni utafanya kazi gani, Kwa upande wangu mimi naamini MUNGU kazi yake ni KUUMBA na kukubariki uishi duniani kwa vipaji/maarifa na mengineyo anakupa, ila kazi ya kuua siyo yake bisaaaa,

Najua humu tupo dini tofauti lakini lakini kuna kapande kaliandikwa
"JILINDE NAMI NITAKULINDA"Hapa kila mtu huwa anatafsiri yake.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Hivi kwa nini aliamua tundu mbili za pua zetu zielekee chini wakati tumesimama huku akijua kabisa chini kuna vumbi na kwa 'bouyancy rule' hewa inayopanda inaweza kuingiza vumbi hilo kwenye pua? (Hapa si kosoi uumbaji hata kidogo, na mimi nakubaliana na Humble African kuwa Mungu ni fundi sanifu mzuri kuliko kila kitu kuwahi kuwepo). Hili ni swali la udadisi tu...! Hivyo intel walioitwa hapa nisadie nielewe hili katika 'engineering design perspective' ama namna nyingine inayofaa bila kuhoji Uwezo wa Mungu.
Mvua ikinyesha au ukioga huoni maji yatazama puani kama shimoni? [emoji23]
 
Mungu ni Mungu ,mapungufu tuliyonayo binadamu yanakamilisha ubidamu wetu, sisi ni mfano wa Mungu kwa tabia lakini si wakamilifu kama yeye.
 
Jizoeze kufanya tathmini ya kiwango cha imani yako kwanza kwa kuangalia kama kinatosheleza kutatua changamoto unazozipitia au la.. Angalia imani yako ipo wapi na kwa nani?. Ukigundua imepungua basi ongeza, kama ipo pahala pengine nje ya Mungu irejeshe kwake na si mwandamu au uwezo na nguvu zako. Maandiko yako wazi kabisa ,kwamba, sisi hatuwezi kufanya jambo lolote bila yeye..ukiwatazama wanadamu wanaenda mbali sana na pengine kutaka kukosoa uwezo wa Mungu na ndio maana wanakuja na logic ambazo kwa namna moja ama nyingine ni kupotosha kama si kuvuruga imani ya mtu fulani, ni kweli na ipo wazi kwamba Mungu hajawahi kukosea katika kila jambo alilolifanya chini ya jua hili..Mungu atabaki kuwa Mungu na wanadamu watabaki kuwa wanadamu siku zote..PERIOD
 
Every thing imperfect came after sin not before sin. You can only understand HIM through scriptures ONLY SCRIPTURES
 
Na unakubali Mungu katuumba kwa mfano wake? Mambo ya dini na imani ni wewe unavyoyatafsiri tu. Binadamu tunatofautiana na tuna hulka tofauti pia ijapo ktk mambo mengine unaweza ukaziona tofauti kidogo lakini walau vitu vingi vina tofauti na hii ni kuonesha pengine uhitaji ama uweza wa Muumba ..kwamba hakuna analoweza kupitaka na likashindikana, akitaka hata ambacho hakipo leo kwa sura/umbo kesho kinaweza kuwepo.

Kwahiyo tofauti alizoziumba labda ni kutaka kudhihirisha kwake yeye kuna kila kitu na anatoa kila kitu kwasababu ya kuwaonesha wanadamu uwezo wake ulio tele
 
Back
Top Bottom