Kwenye bibilia, kuna sehemu nyingi tu ambapo Mungu kafanya matukio na kisha kusikitika, kuonyesha kuwa alikosea, mfano ni pale alipoleta gharika, alisikitika na kudai kuwa hatateketeza tena dunia kwa maji wala kwa moto...
Lakini ukiacha hilo, inaonekana Mungu kila anachofanya anakosea tu na alikosea from the very beginning, hakupanga kabisa kumuumba Eva(Hawa), ila alipomuumba Adam, akagundua kuwa amekosea kumuumba bila msaidizi, ikabidi Amubongonyoe mbavu ili kumuumba Eva, pia huyo Mungu hakupanga Adamu na hawa wazaliane, alitaka waishi tu humo kwenye bustani, shetani kamzidi ujanja, kaenda kutoa siri, ikabidi abadilishe mipango, akawafukuza kwenye bustani na kuwaambia watakula kwa jasho....
Usisahau pia kuwa shetani aliyetoa siri nae aliumbwa na Mungu, Mungu akiamini kuwa huyo shetani atakuwa malaika mtiifu kwake, lahaula!! sivyo hivyo, shetani kabadilika hadi wakashindwana, kaamua kumtupa duniani... Kuna visa vingi ambavyo vinaonyesha kuwa Mungu kila kitu anakosea, na mambo yalivyo, sivyo ambavyo alitaka yawe, ni kana kwamba mambo yalimshinda, akayaacha yaende alijojo.
Hii ya kusema kuwa Mungu hayupo kwenye logic wala reasoning, ni kauli tu ya kujaribu kupambaza watu, ili waache kufikiri, wakubaliane na vitu vya kutunga tu, ambavyo vinajicontradict vyenyewe.
Hakuna binadamu aliekamilika hiyo kauli ni sawa na hii ya "mgaa gaa na upwa hali wali mkavu" zote hizi ni kauli za wahenga tu.Hivyo zipuuze tu!
Mungu katuumba kwa ukamilifu mkubwa saana maana kama matako angeyaweka kifuani tungesema kakosea sababu hatuwezi kukaa comfortably but akayaweka pale nyuma yakiwa na nyama nyama mfano wa spongy sehemu sahihi kabisa ili tukae comfortably na tukiona anayo mbebe tunamsifu kwa kuyaita "Neema za Allah " tuyaite msambwanda kwa lugha za majanki.
God is the best designer ever.