Nafaka
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 12,154
- 31,246
Dah hivi uko serious au unatania mkuu... Nchi ambayo mpaka sasa kuna watu wanatembea mamilioni ya KM kusaka maji? Nchi ambayo ina rasilimali za kutosha lakini bado GDP yake inazidiwa na ka nchi kama Kenya? GDP ya Kenya ni 92 bills dollars ya tz 66.Habari wana jukwaa.
Kama kungekuwa na mashindano ya kushindanisha marais na kutafuta rais wa dunia kama tunavyofanya kwenye vilabu vya mpira wa miguu basi Magufuli wa Tanzania angeshinda asubuhi na mapema na kutawazwa kuwa rais wa dunia.
Rais Magufuli tangu achaguliwe kuwa rais wa Tanzania mwaka 2015 amekuwa akiwaburuza mno marais wenzake kote duniani! Hali hii ilipelekea msomi nguli kutoka Kenya prof Lumumba abatize shughuli na harakati zote za maendeleo za wa Afrika kuwa ni Magufulication of Afrika!
Si Trump, Angel Merkel ,Kagame ,Kenyatta au Putin wote Magufuli amewaburuza kwenye janga la Corona na raia wa nchi zao wanataka Magufuli ndiyo aende akatawale huko.
Kwa sasa Magufuli ni wa kushindanishwa na dunia na siyo hutu tukikaragosi twa mabeberu tu Tundu Lisu.
Wakati South Korea wakiongelea kuhusu kuweka hubs za kuchaji simu kwa ajili ya watu wao mtaani sisi bado hata kila kaya kuwa na bima ya afya bado.
Inawezekanaje raisi wa dunia atoke kwenye nchi kama hii, kama nchi yake tu imemshinda dunia ataiweza?