Kama tungekuwa tunakemea mafisadi na viongozi wabovu kama tunavyowashughulikia mafundi wanaovurunda kazi tunazowapa, Tanzania ingekuwa wapi leo?

Kama tungekuwa tunakemea mafisadi na viongozi wabovu kama tunavyowashughulikia mafundi wanaovurunda kazi tunazowapa, Tanzania ingekuwa wapi leo?

Black Opal

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2023
Posts
233
Reaction score
298
Wabari wakuu,

Nimekuja kwenu na swali la kusindikiza 77.

Ikitokea umempa kazi fundi, inaweza kuwa kukujengea kibaraza nyumbani, kukushonea nguo, kutengeneza kabati, kurekebisha gari lako nk halafu fundi akazingua, tuseme kazi ilikuwa ya wiki mbili, siku ya kukabidhi fundi hajafanya chochote, ndio kwanza ameshika kitambaa alipokuona, au lile kabati ulilotaka akutengenezee ndio anakwambia sasa mbao ndio inaenda kutafutwa!

Tuseme ukweli wakuu, kingeeleweka wapo? Ungemuelewa huyo fundi? Kwa watu wenye roho ndogo wanarusha matusi na ngumi juu, na kwa wale wastaarbu kidogo au wenye mili midogo, wanaojua wakirusha ngumi atapigwa, wanachukua hela yao wanaenda kwa fundi mwingine.

Na tena wanakuwa vinara wa kusambaza taarifa kuwa fundi yule hakuna kitu, ni bure kabisa, usithubutu kumpa kazi yako. Fundi yule kama kazi zilikuwa zinamiminika na umaarufu unashuka, asipojirekebisha na kigenge anafunga, anahama kabisa kwenda ambako hajulikani akaanze upya.

Sasa kama tunaweza kuwakomalia mafundi wanaoharibu kazi tunazowapa, kwanini tunashindwa kuwakomalia viongozi tunaowapa dhamana ya kusimamia mali za umma kwa niaba yetu? Mtu anaiba miaka nenda rudi bado tunashupaza shingo kila wakati kuwachangua muda unapofika na kutetea ujinga wanapofanya ubadhirifu kwa kuwa machawa!

Ina maana hatuna uchungu kabisa na Tanzania yetu kiasi hicho? Tanzania ambayo iko moja tu, sio kwamba kuna nyingine kwamba hii ikiharibika basi kuna nyingine tutahamia huko?

Kwanini hatusimami kidete kuhakikisha mafundi hawa wabovu wanaoharibu Tanzania yetu hawapati tena nafasi ya kufanya uharibifu? Kwanini hatuwapi nafasi mafundi wanaofanya kazi kwa weledi, ambao akifanya kitu wewe mwenyewe unajisikia fahari popote unapokuwa?

Karibuni kwa mjadala wakuu.
 
Sasa ndugu yangu unaanzaje kumuwajibisha Waziri, mkuu wa wilaya, mkurugenzi nk??

Hao wanaoharibu ndio wanaomiliki nguvu (majeshi, polisi nk)
 
kwa huo mkataba hovyo wa bandari ni lazima tutawawajibisha kama tunavyowawajibisha mafundi wa hovyo.
 
Sasa ndugu yangu unaanzaje kumuwajibisha Waziri, mkuu wa wilaya, mkurugenzi nk??

Hao wanaoharibu ndio wanaomiliki nguvu (majeshi, polisi nk)
Kwa Watanzia wote kuwa na mshikamano na kujali rasilimali zetu. Mtu akihiribu watanzania wote tunasema hatumtaki huyu kwa nguvu mojas sio wengine kugawanyika kwa kuwa chawa huku wengine wakinunuliwa na kuacha wachache wanaopigania haki kuonekana wabaya
 
Back
Top Bottom