Kama ujenzi wa barabara ya Morogoro - Dar hauzidi bilioni 300, sioni sababu ya kufanya Private Public partnership, kisiasa italeta kelele

Kama ujenzi wa barabara ya Morogoro - Dar hauzidi bilioni 300, sioni sababu ya kufanya Private Public partnership, kisiasa italeta kelele

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Morogoro Dsm ni kilometa hazizidi 200, hata kama kilometa moja ni bilioni moja, haizidi bilioni 200, hivi kama nchi tunakosa fedha hizi? Na asilimia kubwa ya eneo Hilo fidia ni kidogo.

Tiweke mpango wa miaka minne Kila mwaka tutenge bilioni 100, tutaepuka political issues na pia inawezekana kuijenga.

Iwe njia nne, za Sasa mbili, na nyingine mbili ziongezeke baasi.

Na hii ni nchi Ina historia yake kwa upande wa barabara, hazilipiwi, daraja la kigamboni la wilaya moja tu, kelele za kulipia nyingi, Sasa tuongeze kelele za nchi nzima?

Na hii barabara ndio lango la nchi, italipa ndani ya miaka michache, na sera ya nchi ni kupunguza gharama za biashara na kuifanya bandari yetu ivutie kwa wale wa nchi jirani, kwa Lori zinazopita hapo, ni suala la amri moja, ujenzi uanze kesho
 
Umeanzisha Uzi alafu unacomment mwenyewe. Kwani hii kazi ni ya malipo kulingana na wanaocomment au wanaosoma?
 
Na hiyo barabara ingependeza ikaletwa mpaka Mbezi au Ubungo kabisa
 
Private public partnership ya barabara ya Dar Moro naona kuna dili kwa watu na upigaji ndani yake.mimi sihiamini serikali yangu hata nukta,kila miradi mikubwa naona watu wanatanguliza 10% zao kwanza alafu taifa baadae.
 
Back
Top Bottom