MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Ninamshukuru Mungu kufika tarehe ya leo. Nimeona nitumie huu muda kujikumbusha kwa faida ya wote tabia mbalimbali mbaya tunazopaswa kutoingia nazo 2025 endapo tutajaliwa.
1. Unayesumbuliwa na marejesho ya mkopo kisa ulikopa bila kuwa na mpango imara wa huo mkopo tafadhali mwaka 2025 epuka mikopo kiholela kisa tu unakopesheka.
2. Uliyepoteza hela kwa kuanzisha biashara kwasababu uliambiwa "HII BIASHARA INALIPA" bila kufanya utafiti wako tafadhali sana mwaka 2025 acha huo upuuzi.. Sasa hivi unajipa moyo kuwa "tunajifunza kupitia makosa".... watu makini nyakati hizi hujifunza kupitia makosa ya watu wengine.
3. Ambaye huwa huandiki mahali matumizi yako ingia 2025 na tabia ya kuandika gharama unazotumia kwenye maisha yako. Hii itakusaidia kujisahihisha kwenye matumizi. Hata ukihonga andika sehemu tarehe na kiasi cha hela ulichohonga. Kuna wapuuzi wengi hulalamika kwamba hupata hela nyingi ila hawajui zinapoishia. Kosa lao ni kutokuwa na kumbukumbu za maandishi kuhusu matumizi yao. Siku hizi kuna App za kukusaidia kama hutaki kushika kalamu na karatasi.
4. Uliyetumia pesa nyingi kuwapa wachungaji, manabii, mitume na viongozi wa dini kwa imani kwamba kupitia wao madirisha ya mbinguni yatafunguliwa na kupata baraka uache upumbavu. Hizo hela zako kasaidie watu wa ukoo wenu au hata wahitaji wa hapo mtaani kwenu ili ubarikiwe kuliko kuwapa hao matapeli wa injili.
5. Uliyeumizwa hisia na wanasiasa kwa mwaka huu 2024 ingia 2025 kwa kuacha huo upuuzi wa kuweka matumaini yako kwa wanasiasa hasa wa CHADEMA.
6. Wewe mwanamke uliyemkataa msukuma wa Ngudu na kumkimbilia sharobaro wa Sinza kisha akakuumiza kihisia na pengine kukufanya single mama tubu na uingie 2025 na akili mpya za maisha.
7. Mzazi ambaye huna muda wa kutosha na familia yako jua unakosea. Mwaka 2025 pambana angalau watoto wakusalimie asubuhi kabla ya kwenda shule na pia chakula cha jioni ule nao. Taifa haliwezi kuwa imara bila kuwa na familia imara.
8. Mcheza kamari acha hiyo tabia.
9. Wakataa ndoa badilisheni misimamo yenu mkifanikiwa kuingia 2025. Oeni.
10. Jiongezee maarifa zaidi kwenye kazi unayofanya pia kuwa serious sana na kitu kinachokupa mkate wa kila siku. Wale wafanyabiashara ambao mkipigiwa simu hamjibu kwa wakati, mkitumiwa message hamsomi au wakati mwingine hampatikani kabisa mida ya kazi acheni huo upumbavu.
11. Ishi kulingana na kipato chako. Zile nyuzi za kusema bora Kayumba kuliko English Medium mwisho wake mwaka huu 2024. Usimpeleke mtoto shule ya bei ghali huku kipato cha kutosha huna.