Kama uko Dodoma una laki 6, kila siku nitakuzalishia 10000

Yani nikupe 600,000/= unipe elfu kumi kwa siku nne halafu mtandao uanze kugoma Mara hatusikilizani Mara network inasumbua nyoooo
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Yani nikupe 600,000/= unipe elfu kumi kwa siku nne halafu mtandao uanze kugoma Mara hatusikilizani Mara network inasumbua nyoooo
"Nipo kwenye kelele subiri nitakupigia baadae" hiyo baadae haifiki mpaka unaamua kutuma text "mbona kimya?" Text haijibiwi

Unapiga tena "haloo nipe mda kidogo namalizia hesabu fulani hapa ndg"

Biashara kama hii nimeshaifanya nikiwa chuo, nilikuwa nikipokea boom silitumii maana nilikuwa na hela za ziada za kutumiwa na ndg jamaa na marafiki nikiwapiga vizinga

Sasa nikatokea kuwa na urafiki na jamaa mmoja wa kiduka cha M-Pesa baadae akadai nimpe laki tatu atakuwa akinipa kila mwezi elfu 50 na pesa yangu ikibaki kuwa pale pale

Nikaona isiwe tabu na kuzingatia nilikuwa na kama mia saba ipo tu sikuwa naziona fursa kipindi kile, si nikampa jamaa

Aisee sio tu hiyo elfu 50 kwa mwezi hata hiyo laki tatu sikuipata, hapa ndio nilijua mahakama haina msaada wowote nilipeleka ushahidi wa kutosha ila hakimu anakuja kutoa hukumu jamaa anilipe milion au aende jela miezi sita kwa utapeli

Jamaa alikuwa na madeni mengi sana biashara yake iliyumba si akaamua kutumikia kifungo, na kashatokaga tayari sasa hivi yupo mtaani na mahakama inajua jamaa kashatumikia adhabu yake ila sasa alipoitumikia hiyo adhabu mimi nilifaidika na nini wakati kanipotezea laki tatu yangu?

Nasema tena hata unipe kila siku milioni kwa kiyo hiyo laki sita sikupiiiiiiiiiii
Narudia tena sikupiiiiiiiiiiii
 
Pole sana mkuu, ni mipango tu ya mtu na mtu
 
ila ungesema ni biashara gani...na mchanganuo kidogo,... wazee wa fursa tungejitosa......bank zinafaidika na pesa zetu kifalafala na tunalipia kuzihifadhi huko.......
 
Hiyo biashara ya mtandao sijui jina ila kuna mtu alinidokezea nijiunge chini yake kwa 600k afu kila siku napata 10 kitu kama hicho kwa miezi 6 hivyo nakuwa nimeingiza kama milioni na nusu hivi, (
mambo ya good morning hata kama ni mchana)
 
Ndiyo maana nikataka mtu aliyepo Dodoma ambae tutakaa nakumweleza.. na kumfikisha kwenye biashara husika
 
Hiyo biashara ya mtandao sijui jina ila kuna mtu alinidokezea nijiunge chini yake kwa 600k afu kila siku napata 10 kitu kama hicho kwa miezi 6 hivyo nakuwa nimeingiza kama milioni na nusu hivi, (
mambo ya good morning hata kama ni mchana)
Hapana mkuu sijawahi fanya hizo biashara... Yangu ni biashara ya kila siku
 
Miezi michache baadae tutarajie kusikia kuna mtu huko Dodoma kauawa kikatili sana na watu wasiojulikana kisha wakanyofoa baadhi ya viungo vyake ili kutuliza hasira zao baada ya kutapeliwa na huyo waliyemuua
 
Ni kipi kitaendelea baada ya siku 60 ?

Yaani faida unayonipa kila siku mara sitini inakuwa imefika hio laki sita..., Kwa ushauri kuliko kusumbuka na kutoa hizo elfu kumi kwa siku kwanini usitafute pesa hata robo kwa ndugu zako ili uweke kila kitu kwako ? Hata kama ni miezi mitano upate hio laki sita ili uanze kujipa mwenyewe faida ya 10k kwa siku
 
Back
Top Bottom