Kama ulikua hujui kuwa DAR ES SALAAM kuna TAPELI WA JUICE wacha nikufahamishe;-

Kama ulikua hujui kuwa DAR ES SALAAM kuna TAPELI WA JUICE wacha nikufahamishe;-

Hivi huwa mnakuwa hamna shughuli za kufanya mpaka mnajipitisha mbele ya huyo jamaa, awasimamishe, aanze kuwauliza maswali, na baadaye awape hiyo juisi yake mnywe?

Halafu ni kwa nini wabongo mnapenda sana kula na kunywa hovyo barabarani? Hiyo juisi mnayokunywa barabarani mnayafahamu mazingira ya huko ilikoandaliwa?

Inakuwaje watu tunaowategemea kuwa wajanja mnakuwa wajinga na washamba wa kiwango hiki!
Babu! Kitu ambacho siwezi ni kwenda Kkoo halafu niondoke bila kunywa juice ya miwa na urojo
 
Mi naamini huyo anakadilia wale anao wamudu.
Siku atajichanganya kwa watukazi kama mimi na biashara itaishia hapo.

Na kwa tapeli kama huyo ni kumwendea ukiwa umejipanga. Yaani unapolianzisha uwe na backup ya watu nyuma yako.
Maana kwa kumsoma tu, yeye mwenyewe hafanyi hayo akiwa pekeake, kuna wajinga wenzie wakumpa kampani pindi anapotibua mambo.
 
Kama ulikua hujui kuwa DAR ES SALAAM kuna TAPELI WA JUICE wacha nikufahamishe;-
Katika hali isiyo kuwa ya kawaida kuwahi kutokea TANZANIA,

Mkoani DAR ES SALAAM kuna muuza juice mmoja tapeli,

Ambae hugawa juice kwa kila mtu ambae hupita katika eneo lake la biashara,

Bila kujali kama yeye anakujua au hakujui,

Na baada ya kukupa usipo lipa hukuanzishia ugomvi na kukudai pesa,

Kama vile mulikubaliana kuuziana juice,

Na mtu huyo siyo mwengine ni huyo hapo chini,

Je unataka kujua mtu huyo yupo maeneo gani,

Mtu huyo ukiwa unatokea kariakoo kwenda karume,

Yupo jirani na kiwanda cha bia ambapo ukimaliza tu ukuta wa kiwanda hicho,

Ndipo alipo muuza juice huyo nadhani watu wa dar es salaam munalifahamu hilo eneo,

Sasa anacho kifanya muuza juice huyo ni kwamba,

Ukipita hukusalimia ukiitikia tu hapo ndipo utapeli wake unapoanza,

Ambapo huanza kukuchangamkia kwa kukuuliza maswali kama vile anakujua,

Wakati wala hakujui na wala hamujawahi kuonana,

Lakini yeye hukuuliza maswali kama anakujua,

Utasikia anakuuliza hivi pale umehama au bado uko palepale,

Au anaweza kukuuliza vipi chuo umemaliza au bado,

Na maswali mengine mengi ya kuonesha kama anakujua hivi,

Sasa wakati anakuuliza hayo maswali ukiitikia hukulazimisha usimame,

Na kukuomba usogee anapouza juice yake,

Ukisogea tu anakupa juice bila maelewano yoyote,

Huku akikusisitiza unywe bila shida na bila wasiwasi na uondoe shaka kuhusu malipo,

Wakati unakunywa anaendelea kukupigisha stori kama vile munajuana,

Sasa ukimaliza tu kunywa huanza kukudai pesa,

Tena juice glasi moja huuza buku badala ya jero,

Na ukimwambia huna hela huanzisha ugomvi hapo hapo,

Na wakati mwengine huanza kukusachi mifukoni,

Na wakati mwengine muuza juice huyo hukunyang'anya vitu ulivyo kuwa nazo,

Huku akikuita wewe ni tapeli na umezoea kutapeli watu,

Wakati wewe ulikua unapita zako tu wala hukuwa na mpango nae,

Huyu jamaa amegombana na watu wengi sana,

Na amewanunulisha watu juice zake bila kupenda,

Lakini pia amewanyanganya watu wengi pesa na vitu vyengine,

Kupitia njia hiyo ya utapeli anayoitumia kwa miaka mingi,

Huyo mtu mpaka sasaivi ninavyokuletea makala hii,

Yupo hilo eneo anaendelea na hiyo biashara,

Na ukipita hata sasaivi lazima atakufanyia nilicho kisema hapo juu,

Watu wa dar es salaam kuweni makini sana na huyo mtu,

Kwasababu watu wengi wametapeliwa na huyo jamaa kwa njia hiyo.View attachment 3620361
Anayekunywa juice ya bure ya mtu asiyemjua naye hana akili. Iko siku utanyweshwa sumu kwa uzembe kama huo.
Kwanza unakulaje kitu cha mtu usiyefahamiana naye, ni nidhamu mbaya na yenye madhara makubwa.
 
Back
Top Bottom