Kama ulikua hujui kuwa DAR ES SALAAM kuna TAPELI WA JUICE wacha nikufahamishe;-

Kama ulikua hujui kuwa DAR ES SALAAM kuna TAPELI WA JUICE wacha nikufahamishe;-

Ila mambo ya Dar bwana yanachekesha, huyo mtu nimeanza kumsikia miaka na miaka, lakini hakuna hatua zozote mnazomchukulia. Mtu yupo, mnamjua, mna ushahidi wa uhalifu, alafu kikubwa mnaweza kufanya ni kulalamika mitandaoni, serious?
Umesahau kipindi cha panya road wababa na vitambi vyao walizama uvungu wa vits?
 
Huyo hajakutana na wababe tu au hua anachagua wakuwachezea akili,

Inatakiwa akikupa hiyo Juice unamwagia nayo usoni,kisha unamtwanga makofi mpaka analala chini,halafu hiyo ofice yake unaigeuza kua kuni za kupikia,

Hii stori ya huyo jamaa ni ya kitambo sana,halafu kumbe mpaka leo mnamchekea tu!
 
Wewe unayekunywa kunywa tu mavitu hovyo barabarani kwa kuaminishwa ni juisi ndio una shida hapo...
Inashangaza watu hawajali kabisa afya zao ,mimi hata maji ya kwenye machupa wanayotembeza vijana hata zenye brand kubwa sinywi maana wahuni ni wengi sana mtaani.

Yaani unaitwa unakunywa juice bila kujiuliza hata maswali mawili matatu ,je kama kaweka madawa ya kulevya aniibie ,usalama wa hiyo juice ipo vipi? Wewe unabugia tu.

Kweli kabisa wenye shida kichwani ni hao wanaokunywa juisi na si muuzaji.
 
Lazima mbadilike na kuwabadili watoto wenu kwa kuwafundisha kutoongea na strangers

Hivi kwanini mnapoteza mda wenu kwa kusalimiana na mtu usiemjua? Au mpaka mnafikia mahali anakupa na juice kabisa na wewe unaipokea

Lazima mbadilike na hii tabia ya kusalimiana na kila mtu
Wewe unapita sehemu au umekaa mahali, mtu anaanza kukusemesha kwanini maneno yasiwe mafupi tu
Mimi huwa nawaangalia usoni bila kujibu
 
Back
Top Bottom