Kama ulikuwa unajiuliza ni kwanini Wachezaji wa Azam FC juzi Songea walicheza 'Kikatili' vile kutaka 'Kuua' Wachezaji wa Simba SC jibu hili hapa

Kama ulikuwa unajiuliza ni kwanini Wachezaji wa Azam FC juzi Songea walicheza 'Kikatili' vile kutaka 'Kuua' Wachezaji wa Simba SC jibu hili hapa

Azam Shida si wachezaji ni Azam wenyewe jinsi gani waliaandaa timu na malengo kuanzia scouting
 
Wana Miezi Mitatu hawajapewa Mishahara na si kwamba labda Tajiri 'Mzanzibari' hana Pesa bali kaamua Kuwafanyia 'Kusudi' baada ya Kuwaambia Wachezaji wanamuangusha kwani anawapa kila Kitu hivyo wakitaka Wafurahi basi nao pia Wamfurahishe.

Hivyo basi Wachezaji wengi wa Azam FC sasa kutokana na 'Stress' pamoja na 'Frustrations' zao za Kunyimwa kwa Makusudi 'Mishahara' yao wanaamua Kumalizia 'Hasira' zao kwa Wachezaji hasa wa Timu 'barikiwa' na Mwenyezi Mungu ya Simba SC ambayo nimeambiwa Wachezaji wao (wake) wameshalipwa 'Mishahara' yao ya Miezi Sita (6) ijayo na Tajiri Mohammed 'Mo' Dewji.

Haya GENTAMYCINE namalizia kwa kutoa ANGALIZO kwa Timu Moja hivi Masikini na ya Kishamba inayojiandaa Kufungwa Goli (Bao) Tano (5) kwa Bila (Sifuri) Jumamosi tarehe 3 July, 2021 kuwa Wamiliki na Matajiri wa hiyo Timu wahakikishe wanawalipa 'Mishahara' yao haraka ili nao wasije 'Kutuulia' Wachezaji wetu Simba SC wenye 'Thamani' ya Kuanzia Shilingi Bilioni 1 huku wao 'Thamani' yao ikiwa ni Shilingi Laki Tano mpaka Shilingi Laki Tisa na pungufu unaongea au hata 'Kuwakopa' pia.
Huyu jamaa ana tabia za kidangaji, pesa za Mo ndio zinaipa kiburi Simba? pale aliye na pesa ni Moo siyo Simba, huyu akikaa pembeni Simba haina tofauti na Lipuli.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom