Kwa wale wenzangu na mimi tuliowahi kunywa chai ya kuunguza sukari kama majani ya chai tukutane hapa.
Chai ile ilikuwa inatengenezwa kwa kuchukua Sukari unaiweka kwenye sufuria iliyopo motoni baada ya hapo sukari itayeyuka na kuungua kidogo alafu unachukua maji unaweka basi kitu kinakuwa Cheusi kama umeweka majani ya chai na ilikuwa tamu tu.
Kama ulishawahi kunywa hiyo chai kweli udogoni mwako au ata sasa hivi basi utakuwa umepitia maisha halisi ya mtanzania.
Tuambie hapa kama wewe ulishawahi kuinywa na inakukumbusha wapi kipindi hicho.!?
.