Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sishangai nimeishi hayo maishaUnashangaa mkuu
Noma sana enzi hizo za unga wa Yanga kitu cha njanooo lakini maisha yalikuwa matamu sana jioni bibi anawapoza kwa Hadithi tamu tamu mnasahau yote.80s maisha yalikuwa sio wazee walikuwa wanatuambia hali ya Uchumi ni mbaya kwa kuwa nchi Ilikuwa imetoka vitani nakumbuka shule haikuwa lzm sana kwenda na viatu! wengine mtakumbuka tulifulia Nguo majani ya mpapai ,chai si lzm sana lbd uwe mgonjwa ,hakukuwa na uhakika wa kupatikana sukari Dukani zaidi ya Mara 1 kwa wiki nani lzm ununue na unga wa Muhogo (Ilikuwa haiuzwi pekee) Ilikuwa inasambazwa na RTC na Dukani tulikuwa twaenda na daftari na Mjumbe anathibitisha kama wewe ni mkaaji wa hapo na anasaini kuthibitisha umeshanunua kwa wiki hiyo ili usije ukagushi!
Mambo ya pizA ,bagger wenyewe watoto wa kidigital wanaona wameyapatia kumbeee.We acha tu mambo ya soseji na tumeyakutia ukubwani,nakumbuka Mara ya kwanza kuona kitu chipsi yai kitaa Ilikuwa 80s nilikuwa nakaa kijijini Mwenge nyuma ya Bamaga Petro station ,kuna jamaa alikuwa anaitwa Hamisi alikuwa na banda lake pembeni ya duka la Mpemba opp na Hongera Bar ,jamaa ndio alikuwa mtu wa kwanza kuleta hii kitu mitaa ya Mwenge juu jamaa alikuwa anauza balaa unafika unakuta kuna watu 10 mbele yako wanasubiria
Hii kitu kipindi kile Ilikuwa km bites ukiona hujashiba home unaenda kwa Mpemba na sh 5 au 10 yako mambo yanakaa safi.
Kuna watu huwa nawaangalia siku hizi za usoni nasikitika tu, nimekua ugali na maji ya sukari aisee ndo maana nikijiangalia hapa nilipo sasa naamua kula maisha maana huko nyuma wazee ndo wanajuaMkuu we Acha tu wanaosema dunia inatembea siyo kama gari bali vitendo vinavyofanyika ndani yake
Ha ha ha![emoji16] Foleni za RTC! Huko ndio kwa mara ya kwanza kuona mtu anaweka jiwe kisha kuna my yuko kwenye mstari anamsogezea, ole wako uruke jiwe la mtu![emoji3] Tatitzo ni pale jamaa anapokuwa na mawe matatu hivi anayasogeza....mjini bwana. Ndio tulivyoishi miaka hiyo. Viatu mzee alikuwa ananipeleka jamaa fulani hivi Wapare pale soko kuu Arusha, unapimwa mguu kwa kuweka mguu chini juu ya karatasi halafu jamaa anazungusha kalamu kufuatiza mguu-hapo inachongwa Safari Boot(Buti)[emoji3] Hiyo unavaa mpaka inakauka na kupinda katikati hapo inaitwa "Mbwa", ile ngozi inababuka na kuisha nywele, ukisikia mbwa wanacheka manake zimefumuka mbele vidole vinachungulia[emoji38][emoji38]80s maisha yalikuwa sio wazee walikuwa wanatuambia hali ya Uchumi ni mbaya kwa kuwa nchi Ilikuwa imetoka vitani nakumbuka shule haikuwa lzm sana kwenda na viatu! wengine mtakumbuka tulifulia Nguo majani ya mpapai ,chai si lzm sana lbd uwe mgonjwa ,hakukuwa na uhakika wa kupatikana sukari Dukani zaidi ya Mara 1 kwa wiki nani lzm ununue na unga wa Muhogo (Ilikuwa haiuzwi pekee) Ilikuwa inasambazwa na RTC na Dukani tulikuwa twaenda na daftari na Mjumbe anathibitisha kama wewe ni mkaaji wa hapo na anasaini kuthibitisha umeshanunua kwa wiki hiyo ili usije ukagushi!
Enzi hizo primary ilikuwa kawaida sanaKwa wale wenzangu na mimi tuliowahi kunywa chai ya kuunguza sukari kama majani ya chai tukutane hapa.
Chai ile ilikuwa inatengenezwa kwa kuchukua Sukari unaiweka kwenye sufuria iliyopo motoni baada ya hapo sukari itayeyuka na kuungua kidogo alafu unachukua maji unaweka basi kitu kinakuwa Cheusi kama umeweka majani ya chai na ilikuwa tamu tu.
Kama ulishawahi kunywa hiyo chai kweli udogoni mwako au ata sasa hivi basi utakuwa umepitia maisha halisi ya mtanzania.
Tuambie hapa kama wewe ulishawahi kuinywa na inakukumbusha wapi kipindi hicho.!?
.
Kuna kipindi kulikuwa na uhaba wa majani tulifanya hivyo miaka ya 80s
Ile chai mbona ilikua tamu sana, Mimi nimeinywa sana toka miaka ya 1984 kwani ndio kipindi ambacho nilikua nawai shule kama hakuna majani, mother anakaanga sukari faster kitu na box, umesahau pia ugali wa mboga ya kitunguu kitupu kinakaangwa, duh maisha haya yametoka mbali sanaKwa wale wenzangu na mimi tuliowahi kunywa chai ya kuunguza sukari kama majani ya chai tukutane hapa.
Chai ile ilikuwa inatengenezwa kwa kuchukua Sukari unaiweka kwenye sufuria iliyopo motoni baada ya hapo sukari itayeyuka na kuungua kidogo alafu unachukua maji unaweka basi kitu kinakuwa Cheusi kama umeweka majani ya chai na ilikuwa tamu tu.
Kama ulishawahi kunywa hiyo chai kweli udogoni mwako au ata sasa hivi basi utakuwa umepitia maisha halisi ya mtanzania.
Tuambie hapa kama wewe ulishawahi kuinywa na inakukumbusha wapi kipindi hicho.!?
.