Kama ulishawahi kunywa chai ya kuunguza Sukari tukutane hapa

Kama ulishawahi kunywa chai ya kuunguza Sukari tukutane hapa

Huku mikoani life hilo lipo mpaka kesho.
Kuna hii nyingine:
Kama kupika pilau unaona litakupotezea muda, pika wali wa kawaida wa maji, halafu vaa miwani ya jua. Hapo utakuwa unaona pilau.
hahaaaaaa hahaaaa daaahhh manina hahaaa
 
Ohhk nmelima sana mpunga mkiwa darasa la tatu hapo,hapo chimala unapajua wa mjerumani walikuwa wanamuita,nmekaaa pale ulikuwa unaingiaa ndani kidogo.....shule ya chimala Msingi nmesoma....hapo
Unakufahamu pale kwenye uwanja wa helikopta ya kajima .......jirani na hapo
Hivi ile hospital ya mmarekani bado ipo hapo

Ova
Hahaaa kwetu ila sijakaa

Unamfahamu mzee Salmin ?
 
Maisha ya bongo ndiyo yale yale Mkuu ila nawashukuru sana Wazazi wangu. They are my role models.

[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
Mkuu utakuwa ulipitia kwenye maisha safi.
 
Umewahi kunywa chai ya juice ya miwa? Unachonga miwa, unakata vipande vidogo dogo then unatwanga kwenye kinu hakafu unakamua kupata juice then inachemshwa na maziwa, majani ya chai na iliki juu. Pembeni ugali wa kuchoma uliobaki jana...Hahahaaaa
 
Nimekunywa sana hiyo chai shule fulani kule Ludewa.
Halafu unachangannya unga na maji unakoroga then unakaanga kwenye mafuta. Ndio kitafunio hicho.
Ukijisikia kula pilau basi unakaanga nyanya na kitunguu, kikishaiva, badala ya kutia mboga unatia mchele. Basi linatokea pilau jekundu tamu balaa. Kipolo kikibaki unanywea chai asubuhi.
Tumeshakula Mikate na uji wa kuchanganywa na ulanzi wa asubuhi ule mtogwaaaa kabisa unaitwa nyamtutu.
 
daahh mkuu umenipeleka mbali mnoo kifikra..kuna watu tumepitia msoto aisee

chai ya kuunguza sukari ..ugali kwa chumvi .majani ya mti wa mbamia yanafnywa kuwa mlenda yakiwa mateke ..mboga kama hakuna unapikwa mchuzi wa nyanya tu kisha mnakula na ugali ama wali .. enzi sukari guru hizo ..

ndio maana huwa tunasema maisha tuliyopitia sis hatutaki watoto wetu waje kupitia tena..
MUNGU SAIDIA HILO
 
huwa unafanya mpka leo aiseee ..ckuwezi mkuu
Ndio lakini sio hiyo ya kupaka sabuni, nakumbuka kuna sabuni ziliingia kutoka
kenya tulikuwa tunazificha balaa maana ukionwa nazo unaitwa mlanguzi
basi ukipaka shule au chuoni hizo ulikuwa unaheshimika sana kwa harufu yake
mzuri
 
Hahaaa kwetu ila sijakaa

Unamfahamu mzee Salmin ?
Duh nawajua baadhi wa waburushi pale
Chimala,nlikaa miaka miwili maana nlifukuzwa shule pale maana Nlikuwa mtata sana kila siku Mzee mjerumani analetewa Kesi.....kipa imara nlipatia pale kanisani roma chimala ujue(choice)
Unawakumbuka Wale wachuna ngozi(nyambuda)walisumbua sana pale
Wee waulize wazee wako hapo mnapahamu kwa mjerumani lazima watamjua tu alikuwa famous sana pale ila ni marehemu alikuwa chotara alikuwa mkulima mzuri sana na ana cheo pale kijijini alikuwa na undugu na Wakina black mamba

Ova
 
Hebu akilini mwako jenga picha ya mtu aliyeamka asubuhi akapiga mswaki wa mti kwa kutumia povu la sabuni ya kufulia kama dawa yake ya meno, ndani kavaa underwear aina ya VIP, shati la kuvutika, suruali buga, viatu vya laizon huku anakunywa hiyo chai ya sukari ya kuunguza!
Picha inatisha mkuu
 
Nimekunywa sana hiyo chai shule fulani kule Ludewa.
Halafu unachangannya unga na maji unakoroga then unakaanga kwenye mafuta. Ndio kitafunio hicho.
Ukijisikia kula pilau basi unakaanga nyanya na kitunguu, kikishaiva, badala ya kutia mboga unatia mchele. Basi linatokea pilau jekundu tamu balaa. Kipolo kikibaki unanywea chai asubuhi.
Tumeshakula Mikate na uji wa kuchanganywa na ulanzi wa asubuhi ule mtogwaaaa kabisa unaitwa nyamtutu.
Wali nyanya huo
 
Hayo ndo maisha halisi ya mtz,
siyo haya kuiga iga wazungu kama enzi za kikwete,

juzi nilikutana na mrusha sigara,akanikumbusha mbali sana,
bora sasa tunaanza kurudi kwenye jadi yetu
 
Kanda ya ziwa hii kitu Ilikuwa inaitwa Strungi,tumeipiga sana lkn nilikuwa siifagilii,asikudanganye mtu Hakuna mbadala wa majani wa chai ikawa chai!ni Sawa na kusema unakunywa soda au juisi kukata kiu ya maji, soda ni soda na maji ni maji!
 
Hebu akilini mwako jenga picha ya mtu aliyeamka asubuhi akapiga mswaki wa mti kwa kutumia povu la sabuni ya kufulia kama dawa yake ya meno, ndani kavaa underwear aina ya VIP, shati la kuvutika, suruali buga, viatu vya laizon huku anakunywa hiyo chai ya sukari ya kuunguza!
We acha tu mambo ya soseji na tumeyakutia ukubwani,nakumbuka Mara ya kwanza kuona kitu chipsi yai kitaa Ilikuwa 80s nilikuwa nakaa kijijini Mwenge nyuma ya Bamaga Petro station ,kuna jamaa alikuwa anaitwa Hamisi alikuwa na banda lake pembeni ya duka la Mpemba opp na Hongera Bar ,jamaa ndio alikuwa mtu wa kwanza kuleta hii kitu mitaa ya Mwenge juu jamaa alikuwa anauza balaa unafika unakuta kuna watu 10 mbele yako wanasubiria
Hii kitu kipindi kile Ilikuwa km bites ukiona hujashiba home unaenda kwa Mpemba na sh 5 au 10 yako mambo yanakaa safi.
 
80s maisha yalikuwa sio wazee walikuwa wanatuambia hali ya Uchumi ni mbaya kwa kuwa nchi Ilikuwa imetoka vitani nakumbuka shule haikuwa lzm sana kwenda na viatu! wengine mtakumbuka tulifulia Nguo majani ya mpapai ,chai si lzm sana lbd uwe mgonjwa ,hakukuwa na uhakika wa kupatikana sukari Dukani zaidi ya Mara 1 kwa wiki nani lzm ununue na unga wa Muhogo (Ilikuwa haiuzwi pekee) Ilikuwa inasambazwa na RTC na Dukani tulikuwa twaenda na daftari na Mjumbe anathibitisha kama wewe ni mkaaji wa hapo na anasaini kuthibitisha umeshanunua kwa wiki hiyo ili usije ukagushi!
 
Ndio lakini sio hiyo ya kupaka sabuni, nakumbuka kuna sabuni ziliingia kutoka
kenya tulikuwa tunazificha balaa maana ukionwa nazo unaitwa mlanguzi
basi ukipaka shule au chuoni hizo ulikuwa unaheshimika sana kwa harufu yake
mzuri
owky "" hapo nimekupata mkuu
 
Back
Top Bottom