Kama ulishawahi kunywa chai ya kuunguza Sukari tukutane hapa

Mpaka sukari guru niliisha kunywa chai yake mkuu.
 
Aisee! Chai ya kuunguza sukari tena ndio chai gani?
 
hiyo sometimes ukibugi unaharibu sufuria ipo ile unachukua karatasi ((gazet n.k sio nylon) unafunga sukari then unachoma ikishaanza kuungua kama inatoa povu hivi inwekwa kwenye maji ya moto... Ila harufu yake ndio ya kipuuzi kweli yaan ila hamna namna ilibidi iwe ili life lisonge
 
Chai sio rangi.
Chai ni majani ya chai.
Ukiunguza sukari unapata rangi inayofanana na ile inayopatikana ukiweka majan ya chai, basi tunajidanganya ni chai!

Aisee kama uliwah kunywa chai ya kuunguza sukari wewe ni MUHENGA !
Chai ni rangi, mimi nyumbani tulishasahau hata bei ya majani. Unaweka mchaichai, hiliki, unaponda karafuu, tangawizi. Unapata chai maridadi kabisa.
 
Ndio, ilikuwa sukari inaunguzwa inapatikana chai maridadi sana
kisha unapaka sabuni mwilini yaani mbadala wa mafuta
safari ya shule inaanza. Mimi mara moja moja huwa nafanya mpaka leo
Duh! Unakumbushia mhenga!
 
Harufu yake aaargh, huwa sio nzuri...mi nilikuwa naikata kwa kutilia limao. Enzi za chuo.
 
Sukari kilo 2000/=+ Wakati majani pakiti nzima 500/=....... Nadhani hapa ndo jina la sub-Sahara countries linapopatia nguvu....
 
Nilikua natafuta uzi wa green tea nikakutana na huu. Dah. Haya maisha haya ngoja nikae tu kimya.
 

Ilikua ikikosekana sukari ya kuchoma basi utanywewa uji wa chumvi mradi siku ipite na mkono uende kinywani [emoji848][emoji3526][emoji3526][emoji17][emoji17]. Tulikotoka ni mbali sana, Mungu katuvusha katika mengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…