Kama ulishawahi kusweka mahabusu unakumbuka kituko gani au kimbwenga gani ulichokutana nacho huko ndani?

Kama ulishawahi kusweka mahabusu unakumbuka kituko gani au kimbwenga gani ulichokutana nacho huko ndani?

Slim

Senior Member
Joined
Nov 12, 2008
Posts
145
Reaction score
179
Salaam Wakuu! Kwa wale walioshawahi kukaa mahabusu ni kituko gani unakumbuka au tukio gani unalikumbuka ulikutana nalo huko ndani wakati ukiwa unanyea ndoo na uliingia kwa kosa gani? 😊 😊

Tupieni uzoefu🤭
 
Vituko ni vingi, kuna vibaka wavuta bangi kuandika matusi au kuchora michoro ya ajabu kwenye kuta za selo kwa kutumia damu zinazochuruzika kutoka kwenye majeraha yao au damu za mbu wanazozibamiza ukutani
 
Tulikamatwa sinza kwa kosa la kununua malaya wakati tunaakindikishwa na kusachiwa kwenye dawati kabla ya kuwekwa selo, mwamba niliekamatwa nae akakutwa na kilainishi pamoja na vumbi la kongo ilibidi watu wote wacheke sana, alafu jamaa alikua anaomba msamaha maana asiporudi nyumbani ingekua kesi kwa mkewake hahaaaa
 
Vituko ni vingi, kuna wanaokamatwa usiku wakiletwa selo wanatukana polisi usiku kucha hawalali. Watuhumiwa wengine huwa haijulikani kama akili zao ziko sawa, wanawaropokea polisi maneno ya ajabu, selo zingine zinatazamana, za wanaume na wanawake, maneno ya wanawake na wanaume ni mitongozo tu japo haiwezekani kukukutana ili kukamilisha mitongozo ya usiku. Kituko kingine ni baadhi ya polisi nao kula chakula pamoja na hao watuhumiwa waliopo selo wanacholetewa na ndugu zao
 
Salaam Wakuu! Kwa wale walioshawahi kukaa mahabusu ni kituko gani unakumbuka au tukio gani unalikumbuka ulikutana nalo huko ndani wakati ukiwa unanyea ndoo na uliingia kwa kosa gani? [emoji4] [emoji4]

Tupieni uzoefu[emoji2960]
Anza kwanza wewe mwenyewe na sie ndio futuate
 
Nilikuwa moja ya kituo maarufu Dar,aliwekwa selo kijana ambaye alikuwa na upungufu wa akili,alichota mavi chooni na kuanza kuwatupishia watu na kutupia counter pia.

Pili,Nilishangaa kuona Mateja wakiteseka wakitaka "Kujamba" eti wamekosa unga kwa siku kadhaa hii iliniacha hoi Yani teja anahangaika utasema tumbo linamkata kumbe anataka kutoa "Ushuzi"
 
😀😀 hatari sana
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]umenifanyaaaa nichekeee kingeseeee,acha ufalaaa n bangi ya wapi hii umekulaaa
Ha ha haaa,humu ni full kufurahi mkuu
 
Back
Top Bottom