lamalu
JF-Expert Member
- Jan 6, 2014
- 612
- 775
Mwanza hiyo kama miaka minne hivi imepita maeneo ya nyasaka, nilikuwa na pub yangu kali tu, basi kipindi hicho kufunga mwisho saa sita, mi nikatoka kazini nikaja na washakaj zangu tukaanza kupiga vyomba mara saa sita hii hapa[emoji3] wahudumu wangu wawili wamelewa vibe kubwa tunaukata mziki kama hatuna akili sawa sawa, mara wazee hawa hapa na difenda yao, wakatusomba kona ya kwanza kona ya pili wakataka hela watuachie, watu tupo vibe tukasema hatutoi kitu! Kufumba na kufumbua kirumba hii hapa tukavuliwa mikanda viatu, sasa vitambulisho tulipotoa wakadata ila wakakomaa oooh ingieni tu kesho mtatoka, daaah kwanza mle ndan tulimkuta mwamba mmoja anaimba mapambio balaa, dakika kama kumi hivi wakaletwa washkaj wawili wananuka mafuta ya taa kumbe walikoswakoswa kuchomwa moto,siwezi kuisahau ile siku pombe zote ziliisha, hadi asubuh tunatoka mle tupo hoi, na pub yenyewe niliifunga