Kainetics
Senior Member
- Jun 20, 2022
- 135
- 276
Habari wana JF, sipendi ongelea sana sana mambo ya siasa, lakini kadri siku zinavyokwenda na mwelekeo wa maisha yetu in general unavyozidi kuyumbishwa, nazidi kujenga parallels na plot nzima ya moja ya vitabu vyangu pendwa, 'Animal Farm' kilichoandikwa na George Orwell.
Yaani ni kama uongozi wetu wameamua kufanya live action addaption ya plot nzima, jambo ambalo linatia hasira na kusikitisha. Inapokuja kuumiza zaidi, ni kuwa wachache mno wanajali, maana masses zinapumbazwa na mainstream media kufuatilia mipira, udaku wa ajabu ajabu na nyimbo zisizokuwa na tija.
Siwezi sema haya mambo yameanza leo, ila yamekithiri. Kumcheck huyo Waziri anaongea confidently kuwa watu wako dillusional na gharama za vifurushi zimepunguzwa, imefika hatua nkajiuliza, hawa watu wanatuchukuliaje?
Gharama za maisha in general zimekua juu mno kwa mwananchi wa chini, na kama kumekuwepo wakati mbaya wa kujikwamua kibiashara kwa kujiajiri ni wakati huu...maana karibia kila aspect ya maisha uanze kwenye umeme, kuchukua frame ya jengo, bank, simu, kufuatilia vibali kadha wa kadhaa kama Leseni na TIN's kuna makato ya kila aina. Ni kama kazi ya hawa viongozi imekua ku brainstorm aina mpya ya Tozo, na zinakua introduced kimya kimya.
Kuona haya yote yanafanywa wazi, na wengi wanatoa kero, lakini bado wanakuwa suppressed kwa data za uongo uongo, ni kama uongozi in general wamefikia conclusion kuwa wananchii ni wapumbavu. Hii haijalishi wewe una support rulling party au lah.
Anyway, kama hujawahi soma hicho kitabu, summary yake iko kama ivi; unaweza pitia then uone mambo gani humo yanafanana na yale yanayozidi kuendelea kwenye hii Tanzania yetu;
Animal Farm Summary
[Spoiler Alert]
Kitabu kinaanzia usiku mmoja ambapo wanyama wote kwenye shamba la Bwana Jones wanakutana kumsikiliza mnyama mkongwe zaidi kuliko wao, ambae ni nguruwe walokua wakimuita Old Major. Huyu nguruwe anawaelezea ndoto yake ambapo wanyama wote wataishi kwa uhuru bila mateso ya binadamu(wamiliki wa shamba).
Siku chache baadae, huyo Old Major anafariki ila wanyama wote shambani wanatiwa moyo na hotuba yake, hivyo wanapanga rebellion dhidi ya mmiliki wao, Bwana Jones. Kwenye kupanga huo mgomo, nguruwe wawili Snowball na Napoleon wanaonekana ndio wenye akili zaidi hivyo wanaachwa kuupanga mgomo wenyewe na kuwa viongozi. Inatokea siku moja, Bwana Jones anasahau kuwalisha wanyama hivyi mgomo unatokea na huyo Bwana Jones na wafanyakazi wake wote wanatimuliwa shambani. Shamba lililokua linaitwa 'Manor Farm' wanalibadili jina na kuwa 'Animal Farm' yaani 'shamba la wanyama.'
Na kanuni zao 7 zinaandikwa ukutani kwa ajili ya kila mnyama kuzipitia na kuziheshimu (Tunaweza sema wanyama wanapata uhuru wao 👐)
Baada ya mgomo na mapinduzi kufanyika, wanyama wanafanya mavuno ya shamba lao na kukutana kila Jumapili kujadiri sera mbali mbali za humo shambani na kwa kuwa nguruwe wanaonekana ndio wenye akili, basi mambo yote ya uongozi yanaachwa kwao, huku viongozi wakuu wakiwa Snowball na Napoleon.
Kadri siku zinavyokwenda huyo nguruwe mmoja, Napoleon anaonekana ni mwenye uchu wa madaraka maana anaanza kuiba maziwa ya Ng'ombe na kuyanywa na nguruwe wenzake. Pia anamuajiri nguruwe mmoja, Squeleer, ambae ana nguvu ya ushawishi ili kuwahubiri wanyama wengine mara kwa mara kuwa Nguruwe ndio wana akili zaidi hivyo maamuzi yao yasikilizwe bila kupingwa.
Baada ya misimu kadhaa kupita, Bwana Jones na wenzie wanarudi kujaribu kulichukua shamba upya , lakini kutokana na akili za Snowball, vita hiyo (ambayo inakuja kuitwa Vita Kuu ya Zizini) wanyama wanaishinda na kubaki shambani. Baadae, Snowball anaanza kuunga mpango kazi wa kuanzisha WindMill ambayo itasaidua kutengeneza umeme shambani hivyo kuwapa wanyama wote muda mchache wa kufanya kazi na muda mwingi wa kupumzika. Napoleon(mwenye uchu wa madaraka) kwa upande wake anapinga kua wakianza kujenga hio WindMill watakosa muda wa kutosha wa kulima chakula ila mwisho wa siku inaachwa, ili ipigiwe kura Jumapili.
Napolean kwa kuhofia kushindwa, anakusanya kundi la mbwa wakari ambao wanamkimbiza Snowball ambae anakimbilia nje ya shamba. Napoleon anahairisha zoezi zima la kupigia kura, hio WindMill na kuwaambiwa wenzie kuwa itajengwa. Pia anawaambia wazo lilikuwa lake na huyo Snowball aliliiba. Kwa mwendelezo uliobakia wa kitabu kizima, Napoleon na serikali yake ya nguruwe wanamlaumu Snowball kwa kila tatizo linalojitokeza shambani.
Muda mwingi wa mwaka unaofuata, unatumiwa kujenga hio Windmill ya kuzalisha umeme na farasi mwenye nguvu, Boxer , anakuwa mchapakazi kuliko wanyama wengine wote kwenye zoezi la ujenzi wa hio Windmill. Upande wa pili, Bwana Jones anaamua kuachana na shamba lake na kuhamia kijiji kingine.
Kwa kuwa Napoleon ndie nguruwe aliebaki kama kiongozi, anasimamia shughuri nzima kiukandamizaji, na anafikia kumuajiri binadamu awasaidie kufanya biashara na mashamba mengine(kwa kuuza mayai, maziwa, na ndama wan ng'ombe wengine. Mambo ambayo yalikua yanafanywa na binadamu na yaliowafanya wawapindue in the first place) ila wanyama hawabishi maana kuna mi mbwa hio mikari, anaebisha analiwa mbele ya wenzake. Wakiwa kati kati ya ujenzi, inatokea mvua kubwa na kusambaratisha windmill yote, ila Napoleon anawaambia wanyama wake kuwa Snowball aliingia shambani usiku na kuiangusha. Ujenzi unaanza na moja.
Kadri siku zinavyoendelea na uchu wa madaraka wa Napolean kukua, anaanza lazimisha wanyama kukiri makosa ambayo hawajafanya na kuchinjwa mbele ya wenzie, pia share ya chakula kwa wanyama shambani inazidi kupunguzwa kila siku huku nguruwe wakizidi kunenepa.
Uhuni unazidi, maana nguruwe wanaacha kuishi na wanyama wenzao na kuhamia kwenye nyumba ya Bwana Jones, na kuanza kulala vitandani. Windmill inakamirika na nguruwe wanamua kuuza mbao kwa mkulima jirani ili waweze nunua generator 😂 lakini mkulima mwenyewe anawalipa kwa hela feki na kufanya njama za kuvamia shamba. Inatokea vita nyingine na kwa mara nyingine tena, Windmill inabomoka lakini huyo mkulima anashindwa lichukua shamba.
Pia taratibu...sheria zao saba Nguruwe wanazidi zibadilisha kila siku, mfano kuna siku Nguruwe wanapoanza kunywa pombe, wanabadilisha sheria inayosema 'Hakuna mnyama atakae kunywa pombe' na kuifanya kuwa 'Hakuna mnyama atakae kunywa pombe kupita kiasi'
Unamkumbuka yule farasi mchapakazi? (Boxer) Afya yake inadhohofika, kwa sababu ya uzee na siku moja akiwa anajaribu pandisha matofari kileleni, anaanguka. Nguruwe wanamuuza kwa mpika supu, na gari linapokuja shambani kumchukua, wanyama wanadanganywa kuwa alipelekwa kwa afisa mifugo, na alifia kitandani akiwa anatabasamu - ujimga ambao wanyama wengine wanauamini.
Miaka inasogea, na shamba linatajirika, na nguruwe wanazidi kunenepa huku wanyama wengine wote wakiishi kwa taabu mno. Nguruwe wanazidi kuvunja sheria zote walizoweka mwanzo na kuanza kuvaa nguo, na kutembea kwa miguu miwili badala ya minne. Inafika hatua kanuni zote zinafutwa na inawekwa kanuni moja kuwa 'Wanyama wote ni sawa ila Wanyama Baadhi ni Sawa Kuliko Wengine' 🤓
Kitabu kinaishia kwenye wakati ambapo Nguruwe wamaweza nunua shamba la mkulima mwingine wa karibu, Bwana Pilkington , na amekaribishwa shambani kusign makaratasi. Scene ya mwisho ni Nguruwe wako ndani, na Bwana Pilkington wakicheza karata na kubishana huku wanakunywa pombe na kucheka, huku wanyama wengine wanachungulia madirishani wakishindwa tofautisha nani ni Nguruwe na nani ni Binadamu.
Paralles unaziona?
Nawasilisha.