Siasa za Tanzania zimekuwa za ajabu sana, yaani kiongozi mkuu analazimishiwa umati ili aonekane amejaza watu na ipeleke picha kwamba anakubalika kumbe kiuhalisia ni uongo mtupu.
Jiji la Mwanza linahitimisha shughuli za mwenge wa taifa tarehe 14/10/2024. Lakini cha ajabu maandalizi yote kwa ajili ya kupokea mwenge huu yameleta adha kubwa kwa wanafunzi na watumishi kwa sababu masomo yanabidi kusimamishwa ili wanafunzi na walimu waende kupokea mwenge huu na kuhudhuria siku ya tukio husika. Kwa kipindi kama cha mwezi mzima watoto wamekuwa wakichukuliwa mashuleni kwenda kufanya mazoezi ya Alahiki kwa ajili ya shughuli hiyo. Watoto wanakatiza mabarabarani kwenda CCM Kirumba kwa ajili ya siku hiyo huku mvua na jua likiwa ni halali yao.
View attachment 3123191
Nini faida kiongozi mkuu unapata unapoona watu wamejaa kwenye mkutano wako kinafiki, huku mioyo yao ikibubujikwa machozi kutokana na kulazimishwa kuhudhuria kwenye mikutano hiyo pasipo mapenzi yao?
View attachment 3123200

Last edited: