Kama umejenga nyumba, na hili ombi huliombi itakula kwako

Watu wengi wanajenga nyumba lakini hawafaidi. Nyumba inakuwa ya moto inabidi ashinde bar aje amechelewa.

Wengine tangu wajenge hawajawahi kuingia ndani ya hizo nyumba.

Mwingine anamaliza kujenga tu anapata uhamisho anaishia kupanga wakati ananyumba sehemu.

Wengine wanajenga nyumba lakini maisha yanakuwa kama anatembea peku kwenye shubiri au ngutu (mina flani yenye sumu).

Kama ni mkristo wengine sijui, kuna hii kitu huwa haufanyi. Kuomba maombi ya kukiri ahadi ya kukaa kwenye nyumba uliyoijenga.

Watu watajenga nyumba na kuishi humo; watalima mizabibu na kula matunda yake.
Isaya 65:21

kumbuka kujenga nyumba ni amri ya Mungu.
Mithali 24:27
Tengeneza kazi yako huko nje, Jifanyizie kazi yako tayari shambani, Ukiisha, jenga nyumba yako.

Kwa hiyo unapoona unaishi kwa hofu na wasiwasi ndani ya nyumba, umejenga lakini huishi kwenye nyumba uliyojenga. Unatamani kuishi kwa amani ndani ya nyumba yako bila mafanikio. Tangu umejenga huoni matunda yoyote.
Mshukuru Mungu kwa nyumba lakini mwambie sawasawa na neno la Isaya na mimi nataka kukaa nilipopajenga. Jitamkie kwa imani inakuwa tena kwa haraka.

Ni hayo tu
Mtumishi Matunduizi
Nzuri sana
 
mkuu!
Yaani kwenye uzi wowote unaomhusu mungu au uwepo wake ni lazima uwe wa kwanza kucomment,

Unazigunduaje hizo nyuzi na kuwahi hivi?
Humu sio kanisani , kwamba kila mtu afuate tu bila kuhoji , ingekua ipo jukwaa la dini wala usingeniona
 
Watu wengi wanajenga nyumba lakini hawafaidi. Nyumba inakuwa ya moto inabidi ashinde bar aje amechelewa.

Wengine tangu wajenge hawajawahi kuingia ndani ya hizo nyumba.

Mwingine anamaliza kujenga tu anapata uhamisho anaishia kupanga wakati ananyumba sehemu.

Wengine wanajenga nyumba lakini maisha yanakuwa kama anatembea peku kwenye shubiri au ngutu (mina flani yenye sumu).

Kama ni mkristo wengine sijui, kuna hii kitu huwa haufanyi. Kuomba maombi ya kukiri ahadi ya kukaa kwenye nyumba uliyoijenga.

Watu watajenga nyumba na kuishi humo; watalima mizabibu na kula matunda yake.
Isaya 65:21

kumbuka kujenga nyumba ni amri ya Mungu.
Mithali 24:27
Tengeneza kazi yako huko nje, Jifanyizie kazi yako tayari shambani, Ukiisha, jenga nyumba yako.

Kwa hiyo unapoona unaishi kwa hofu na wasiwasi ndani ya nyumba, umejenga lakini huishi kwenye nyumba uliyojenga. Unatamani kuishi kwa amani ndani ya nyumba yako bila mafanikio. Tangu umejenga huoni matunda yoyote.
Mshukuru Mungu kwa nyumba lakini mwambie sawasawa na neno la Isaya na mimi nataka kukaa nilipopajenga. Jitamkie kwa imani inakuwa tena kwa haraka.

Ni hayo tu
Mtumishi Matunduizi
Nilimaliza Kujenga lakini Mke wangu hataki kuhamia😅😅
 
😁😁 hiyo ni namna tu ya kujihami tu , watu ambao hawaamini Mungu wala shetani wala sala za namna yoyote, na wanajenga na kuishi vizuri tu hao unawaweka kundi lipi?
Siri za nyumba ni kubwa Mkuu.
.Usione mtu anatoka kwenye nyumba nzuri siku akisimulia utashangaa.
Mimi kuna jamaa yqngu aliniambia akilalia mto tu basi asubuhi anamka sura kama imegongwa na Hice
 
Kwamba nisijue siri za nyumba kuwa mimi ninaishi kwenye pango😁😁😁 huwa mnachekesha sana walokole 😅😅😅
 
Unajua kusoma lakini? Sijasema kafanye utafiti.
Kwa walionielewa nimesema "nyumba zina siri"
Kuna wengine watoka ndani lakini yaliyomkuta ni siri yake.
.Nimetoa mfano wa rafiki yangu anayeishi ndani ya nyumba lakini kwake mto umekuwa tatizo.

Kahangaika jinsi ya kulitatua kaambulia patupu.
Lakini naye asubuhi anatoka ndani ya nyumba.
 
Sijui kusoma, hizo ni blabla tu hazina uthibitisho wowote zaidi ya mawazo hafifu mda mwingine tatizo la afya ya akili linaweza kuchangia hallucinations na illusion, na mtu akasimulia mkaona ni hivyo mnavyoita mapepo au ushetani.
 
Nyie kina min -me na huyo utopolo wako KENZY yani hamuamini maneno simple tuu kama hayo?? Yani hamna hata chembe kiduchu ya imani aisee....mbona mistari ipo clear kabisa...ni ukweli mtupu...bariki ardhi yako na nyumba yako ukae na uzae humo uongeze dunia...
Mimi sio mlokole ni mkatoliki pyuaaa...kabla hatujaanza kujenga huwa tunamuita Padri anabariki ardhi yetu then tukitaka kuhamia anabariko nyumba...neema na baraka tunaziona ulinzi wa Mungu upo...
 
Nyie kina min -me na huyo utopolo wako KENZY yani hamuamini maneno simple tuu kama hayo?? Yani hamna hata chembe kiduchu ya imani aisee....mbona mistari ipo clear kabisa...ni ukweli mtupu...bariki ardhi yako na nyumba yako ukae na uzae humo uongeze dunia...
😁 wewe sitakujibu, unaendelea vipi lakini?
 
Sijui kusoma, hizo ni blabla tu hazina uthibitisho wowote zaidi ya mawazo hafifu mda mwingine tatizo la afya ya akili kuchangia hallucinations na illusion, na mtu akasimulia mkaona ni hivyo mnavyoita mapepo au ushetani.
Ndivyo unavyoamini.
Miaka niliyokuwa napanga kuna Bwana alikuwa anapigwa viboko nyumba ya jirani na vinasikika ikiwa ni pamoja na kelele za kilio.
Akitoka ndani mwili mzima ulikuwa unakuwa na alama za fimbo.

Na kitendo hicho kinafanyika ndani ya nyumba. Na ndiye anayetekeleza adhabu hiyo alikuwa haonekani.
Matokeo tulikuwa tunayaona kwa muadhibiwa kwa majeraha ya kupigwa.

. Hapo unasemaje mwelevu?
N sehemu ya afya ya akili?
 
Hakuna kitu kama hicho , ukijenga imani ya kufikiri uchawi mara sijui mapepo ubongo una tabia ya kukuletea illusion za ajabu .

Nilisha kaa nyumba ambayo kila mtu aliamini ina mapepo sikuona chochote mpaka nilipomaliza kilichonipeleka pale,zaidi watu waliishia kuniita jini mara freemason na ujinga mwingine.

Note, sipingi mtu kuamini anavyotaka ila unaposema jambo hili ni kweli na ndivyo inatakiwa kwa kila mtu lazima uwe na uthibitisho .
 
Back
Top Bottom