Kama umejiajiri unapaswa kufanya kazi kwa bidii, ukiajiriwa acha sifa fanya jukumu lako tu

Kama umejiajiri unapaswa kufanya kazi kwa bidii, ukiajiriwa acha sifa fanya jukumu lako tu

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Hello!

Ndio hivyo wazee, kama umejiajiri fanya kazi kwa bidii maana biashara ikifilisika na wewe umefilisika automatically bila kipingamizi.

Ila kama umeajiriwa neno bidii halikuhusu, kumbuka kuwa kama ulijaza mkataba wa kuanza kazi ni vyema ujue kuna mkataba wa kumaliza kazi.

Watu wengi wameumia sana baada ya kufanya kazi kwa sifa na baadaye termination ikawakumba.
Work easy.

Fanya jukumu lako tu acha kimbelembele. Kuna watu ni vimbelembele mpaka wanavamia majukumu ya wengine.

Weka akiba kidogo kidogo usije ukachanganyikiwa siku utakayogeukwa na huyo bosi wako anayekusifia leo.
 
Akili za Kitanzania hiz. Popote utakapokuwepo fanya kazi kwa nguvu moyo na maarifa yote. Mpaka ifike mahali wenye kazi wakuhtaji wewe sio wewe unawahtaji.
 
Back
Top Bottom