Kama Umeona Maafisa Ugani Wenye Vishkwambi, Pikipiki na Vipima Udongo, Njoo Hapa

Kama Umeona Maafisa Ugani Wenye Vishkwambi, Pikipiki na Vipima Udongo, Njoo Hapa

Kati ya mwezi Machi na June Waziri wa Kilimo aling'ara sana na kuimarisha huduma za Kilimo Vijijini. Wengi tulimsifia kuwa anaupiga mwingi na yeye ndiye mfano kwa mawaziri wengine. Moja ya mikakati yake ilikuwa ni kuwa wezesha Maafisa Ugani na vitendea kazi kama Pikipiki, Vishkwambi na Vipima Udongo.

Mimi maeneo niliyopita sijakutana na hawa wataalamu na sasa ni miezi 6 yoka wamaegawa vifaa tajwa. Kama wewe kijijini kwako umewaona, tafadhali njoo hapa utoe ushuhuda.

View attachment 2447736View attachment 2447735
Maafisa Kilimo/ Mifugo ni moja wapo ya kundi la watumishi serikalini lisilo na mtetezi.Mimi nipo halmashauri ya mkoa mojawapo nyanda za kusini. Ukweli ni kwamba kupitia vikao vya halmashauri ilielezwa kwamba pikipiki hizi zingeletwa lakini hadi leo hakuna hata pikipiki moja ya afisa ugani iliyofika.

Mtaani wananchi wanawalaumi maafisa kilimo bila kujua ukweli. Nimefatilia halmashauri zingine km wamepata wengi hawajapata. Ni halmashauri chake sana ambazo zilipatiwa zile pikipiki chache zilizokuwa zikipigwa na jua pale Wizarani baada ya Waziri mkuu kuingilia kati.

Tatizo kuna picha mbaya imejengwa na wakulima/wananchi ya kuwaulumu maafisa kilimo kitu ambacho si kuzuri. Kabla ya kulaumu fanya kwanza utafiti.
 
Back
Top Bottom