Kama Umeona Maafisa Ugani Wenye Vishkwambi, Pikipiki na Vipima Udongo, Njoo Hapa

Maafisa Kilimo/ Mifugo ni moja wapo ya kundi la watumishi serikalini lisilo na mtetezi.Mimi nipo halmashauri ya mkoa mojawapo nyanda za kusini. Ukweli ni kwamba kupitia vikao vya halmashauri ilielezwa kwamba pikipiki hizi zingeletwa lakini hadi leo hakuna hata pikipiki moja ya afisa ugani iliyofika.

Mtaani wananchi wanawalaumi maafisa kilimo bila kujua ukweli. Nimefatilia halmashauri zingine km wamepata wengi hawajapata. Ni halmashauri chake sana ambazo zilipatiwa zile pikipiki chache zilizokuwa zikipigwa na jua pale Wizarani baada ya Waziri mkuu kuingilia kati.

Tatizo kuna picha mbaya imejengwa na wakulima/wananchi ya kuwaulumu maafisa kilimo kitu ambacho si kuzuri. Kabla ya kulaumu fanya kwanza utafiti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…