Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

digba sowey

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
8,926
Reaction score
17,880
Wakuu habari zenu, ni matumaini yangu kuwa hamjambo.

Leo nataka kuweka ushuhuda wangu kwa niliyoyashuhudia live juu ya nguvu za giza, kwa wasioamini nadhani uzi huu hautakuwa na thamani kwao, kama na wewe unao ushuhuda usisahau kushea nasi.

1. Ushuhuda wangu unaanzia mwaka 1992 nikiwa nafundisha shule X wilaya ya Sengerema, kuna mwalimu nilikuwa nafundisha naye kituo kimoja.

Siku hiyo kuna kamvua kalinyesha sana, baada ya kupungua mwalimu mwenzangu alimuagiza mtoto wake wa kiume aliyekuwa akisoma darasa la kwanza kwenda kuchuma maharage shambani.

Bahati mbaya mtoto akiwa shambani aligongwa/aliumwa na nyoka na kupeleka kifo, tulifanya taratibu za mazishi na kumsitiri mtoto huyo.

Cha kushangaza mwaka 2008 mtoto huyo alionekana akiwa uchi na nywele ndefu sana alikuja moja kwa moja nyumbani na kupitiliza ndani nyumbani kwao, alikuwa ameshakuwa baba mzima, nywele zilikuwa ndefu sana pamoja na mikono iliyofikia usawa wa magoti.

Watu walistaajabu sana lakini hakudumu sana alifariki baada ya kukaa uraiani kwa wiki mbili.

2. Ushuhuda wangu bado unabaki huko huko Sengerema katika kijiji cha Bubandwamhela.

Nikiwa nafundisha shule X, kuna binti kijijini aliyekuwa akisoma darasa la saba aliugua ghafla baada ya kutoka shuleni.

Wazazi wake walipompeleka hospitali daktari aliwaambia mtoto hana ugonjwa, wazazi waliamua kujiongeza na kumpeleka kwa mganga wa jadi.

Cha kushangaza kesho yake shangazi ya binti alikutwa kwa mganga akiwa uchi, huku akiweweseka na akili zimemruka, shangazi mtu alikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi lakini kwa kuwa serikali haiamini ushirikina aliachiwa huru, lakini hadi leo hii alishakuwa chizi. Binti yeye alipona kabisa.

3. Kisa cha tatu na mwisho ni hiki kilichotokea Liwale shule ya sekondari X nikiwa na walimu wenzangu ambao tulikuwa tunasoma chuo cha SAUT-Mtwara.

Tulipangiwa field katika wilaya ya Liwale ilikuwa mwaka 2009, mwanachuo mwenzetu akiwa zamu siku hiyo alikumbana na mtoto ambaye kwao iliaminika kuwa bibi yake alikuwa mtaalamu wa mambo ya giza.

Mwanafunzi huyo alichelewa kufika shule, mwalimu alipotaka kumuadhibu aligoma, wakasumbuana sana mwisho wa siku akamuadhibu yakaisha, jioni tukiwa uwanjani tunafanya mazoezi yule mwanachuo mwenzangu alianguka na kupoteza fahamu, ikawa jumla hadi kifo.

Kama na wewe umewahi kukutana/kushuhudia live ushirikina share nasi kisa chako watu tupate ilimu.

Mungu ni mwema siku zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka ya nyuma tunatoka mererani usiku wa manane tuko na pikipiki almaarufu baja tullikutakana na moto mkubwa ukiwa umetanda barabarani kama vile unavuka ,tulikuwa sita tukajishauri sana lakini kwasababu tulikuwa wengi tulipata ujasiri wa kupita ila cha kushangaza tulivuka na hatukuungua wala kuhisi chochote kuangalia nyuma baada ya kuvuka moto uko vile vile
 
Nishawahi sikia kisa kinschohusishwa na uchawi

Kuna masela wawili walienda kwa mganga ili wapate utajiri

Mganga akawapa dawa akawaambia wakaoge usiku makaburini na wakitoka mlangoni kwa mganga hawatakiwi kugeuka nyuma

Basi unaambiwa safari yao iliandamwa na misukosuko yakutisha, mara wasikie muungurumo wa simba akiwa nyuma yao na vimbwenga vingi lakini walijitahidi kukaza ili kutovunja sharti la kugeuka nyuma

Sasa ulipofika usiku majira ya saa 8 ikabidi waende makaburini kuoga ili kumalizia zoezi lao la mwisho ili wawe mamilionea

Walipofika makaburini wakavua nguo wote nakubakia uchi kisha wakapanda juu ya kaburi ili waoge

si unajua ukiwa katika ile mood flani hivi unaoga halafu umefumba na macho ili maji yasiingie machoni.

wakastukia tu paap! wameshikwa makalio kwa nyuma.

Aaah unaambiwa wote ilibidi wageuke nyuma kwa haraka huku wanakimbia na kupiga makelele

Kesho yake kijiweni wakaanza kulaumiana "aaah wewe ndiye ulizingua, we ungekausha bila kupiga mikelele mi nisingechochora kwani kushikwa tako kitu gani bwana" yani leo nisingekua nakunywa kahawa hapa ningekua nimejikoki huko kwenye hotel zinazotambulika na dunia"
 
Kisa kingine nilikisikia kilitokea maeneo ya sumbawanga

Kuna mzee wamakamo alikua ni tajiri sana, pesa zake haweki benk na hata akienda kufanya manunuzi hua haweki kwenye wallet kuzistiri zisionekane yeye hua anazishikilia tu kama wanafunzi wanavyoshika vitini vyao mikononi

Siku moja kuna kosi la majambazi lilijipanga kwenda kumvamia

Walimkuta yuko nyumbani kwake ameshikilia pesa akipata upepo kwenye garden yake

Wakamnyooshea bastola na kumwambia atulie kimya kisha atoe kila kitu alichonacho

Yule mzee akachukua zile pesa akazibana kwenye kwapa lake huku akitetemeka kwa woga

majambazi wakamsisitiza kua anyanyue mikono juu, mzee akatii amri kwa kunyanyua mikono juu kisha pesa alizozibana kwapani zikaanguka chini majambazi wakaziokota

Wakamwambia tena "toa kila kitu ulichonacho"

Round hii unaambiwa mzee alichomoa kichwa chake akakishika mkononi halafu kile kichwa kikiwa mkononi kikatoa sauti ikisema

"sina chochote jamani nina kichwa tu hapa"

FB_IMG_15787335109795675.jpg
 
Nipo Njombe huku!! Kuna mwanafunzi alikuwa anafanya mtihani kabla hajamaliza mkono ukaanza kuvimba ghafla hivyo ikashindikana kumalizia mtihani huo! Ikabidi tuwasiliane na Mzazi wake akasema tusimpeleke popote anakuja mwenyewe basi wakaja hapo shuleni na mchungaji baada ya maombi kama dakika 5 tu mkono ulijirudi na kuweza kuandika vizuuuuuuri! Daaa Kweli uchawi upo!! TUMWOMBE MUNGU DAIMA!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kisa cha kwanza ambacho kinanivutia hadi leo ilikua mwaka 1998, Niko na jamaa yangu, Tunatokea Shule ya Wasichana Kifungilo tunarudi shuleni kwetu Magamba Secondary (now Sebastian Kolowa University)! Usafiri miaka ile usafiri ulikua wa shida sana, tukawa tunasubiri usafiri pale Mkuzi, SAA Tisa au kumi hivi jioni. Mvua ikaanza kunyesha, wenyeji wakasema kuwa Mvua haitanyesha kwa kuwa Mzee Fulani yuko shambani kwake anauza mapeasi yake.

Ghafla yule Mzee akawa anapita, aiseee seriously kwa Mara ya kwanza tangu nizaliwe sijawahi kuona MTU hanyeshewi na mvua! Yaani mvua inanyesha lakini yeye hanyeshewi kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kisa cha pili

Mwaka 2008 nafanya kazi Makambako kwenye mradi wa UKIMWI! Sikumoja mchana wa saa nane tulikua ofisini kama watatu hivi, nakumbuka nje jua lilikua Kali sana, ile nyumba ilikua na madirisha makubwa Na geti kubwa nje! Gahfla geti likagongwa na akaingia mwanamke mnene mrefu wastani amevaa gauni jekundu na handbag! Basi tukawa tunasubiri agonge sasa mlango wa ofisi aingie! Dakika kadhaa zikapita, kimya! Tukaulizana, mgeni kaishia wapi?

Nikatoka nje, hakuna MTU, nikazunguka jengo zima hakuna MTU! Nikarudi ndani nikawaambia mwenzangu, dah sitakaa nisahau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka kipindi hicho nikiwa na umri wa miaka 6. Usiku wa saa saba, mkojo ukanibana sawa sawa, ikabidi nimwamshe Mamdogo anitoe nje ili nitoe hiyo haja ndogo

Kwasababu Mamdogo alikuwa na usingizi kwa kutosha, ikabidi anipige biti la hatari na kufoka sana. Tukatoka, yeye akasimama mlangoni mie nikasogea kama mita nne hivi ili nijisaidie. Zile kelele za mother kufoka usiku akiwa mlangoni, tulisikia sauti ya kike kutoka nyuma ya jiko ikisema "MUACHE AKOJOE NAWEWE". Hahahahah! Sikutambua Mamdogo kaingia ndani sangapi maana kugeuka nyuma sioni mtu mlangoni. Kwakuwa nilikuwa mdogo niliendelea na haja yangu then nikarudi ndani.
 
Back
Top Bottom