Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Nawasilisha kama ilivyosimuliwa :

Kuna mwalimu Shule X, huko kanda ya ziwa, aliamka saa tisa usiku kuwahi usafiri asubiri gari kwenda mjini, kijiji cha ndani huko mkoa mpya uliopo ziwani.

Akasubiri gari na baada ya mda likaja, akasimamisha na kuingia. Gari ikaondoka, kakaa baada ya mda kumcheki abiria mwenzake kainama, akahisi labda ni usingz, lakini alipocheki waliopo nyuma pia dizaini kila mtu kainama. Akaona isiwe shida akamsemesha jamaa kainama tu kwa siti yake.

Sasa na yeye akatulia, gari imeenda lakini ghfla kama kausingz kakamwingia, akshtuka ghafla ni saa kumi na mbili asubuh na amesimama pale pale alipokuwa saa tisa kituoni.

Akapanic, kachukua baiskeli hadi wilayani hakurudi tena, ikabidi afisa elimu aende kule na timu yake kuongea na waalimu na wananchi ila jamaa hakuweza kukubali kurudi kituoni. In short walimpa uhamisho.

Nyingine mwalimu kapangiwa kituo Shule X huko kanda ya nyonyo. Kama ujuavyo vita ya kugombea mwalim binti mpya kati ya wanakijiji na wafanyakazi wenzake. Kumbe akawa kawakatalia, ikawa nongwa!

Siku moja anaosha ndizi kamaliza vizuri kwa sufuria, ghafla kikashuka kinyesi kingi kika replace ndizi zote, kinyesi fresh kinatoa hadi Moshi. Madam yule alikimbia kwenda kwa Bro nae ni mwalimu jirani Yake. Hakurudi tena kwa ile nyumba anaogopa.

Nina visa kama 10 kidogo ila mzembe kuhadithia.

Haya Mambo yapo kanda ya Nyonyo hasa kwa tuliokulia Bush huwa hata hatutetereki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh ,kama una presha lazima uzimie
Nakumbuka kipindi hicho nikiwa na umri wa miaka 6. Usiku wa saa saba, mkojo ukanibana sawa sawa, ikabidi nimwamshe Mamdogo anitoe nje ili nitoe hiyo haja ndogo

Kwasababu Mamdogo alikuwa na usingizi kwa kutosha, ikabidi anipige biti la hatari na kufoka sana. Tukatoka, yeye akasimama mlangoni mie nikasogea kama mita nne hivi ili nijisaidie. Zile kelele za mother kufoka usiku akiwa mlangoni, tulisikia sauti ya kike kutoka nyuma ya jiko ikisema "MUACHE AKOJOE NAWEWE". Hahahahah!!! Sikutambua Mamdogo kaingia ndani sangapi maana kugeuka nyuma sioni mtu mlangoni. Kwakuwa nilikuwa mdogo niliendelea na haja yangu then nikarudi ndani......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kijiji kimoja mkoa X, mzee mmoja alipowaona kuku wa jirani wanashambulia mahindi shambani mwake akaamua kuwatimua kwa kuwapiga na mawe.
Alipoamka asubuhi akajikuta mguu mmoja umetoka uko pembeni hakuna damu wala nini, akiwa katika taharuki nini afanye akalala tena kuamka kesho yake mguu wa pili pia umetoka uko pembeni.
Mpaka leo huyo jamaa yuko na ameshakuwa mzee haelewi nini kilimkuta anatumia wheel chair, uchawi upo.
 
Sure mkuu

2010 nipo ndani ya fuso, natokea Ifakara kwenda dsm. Kufika Maseyu mida kama saa 8 usiku dereva akapaki, akasema amechoka anapumzika kidogo. Akatuambia saa 10 tumwamshe tuanze safari.

Sijui kama ni uchawi au ni nini, tulipitiwa na usingizi mzito, na wote, tulikuwa watatu tuliota ndoto ya aina moja. TUNAPIGA MECHI. tumejipiga mabao wote, kuangali saa ni dk 20 tu zimepita. Nilichowaeleza wenzangu ndio walichoota. Mwanamke niloyeota namgonga ndio huyo huyo wenzangu walikuwa wakiota wanamgona.

Niliota vipele vya baridi kwa uoga. Tukaondoka kuendelea na safari. Tangu siku hiyo sipandi tena malori ya mzigo yanayosafiri usiku.

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Nakumbuka kipindi hicho nikiwa na umri wa miaka 6. Usiku wa saa saba, mkojo ukanibana sawa sawa, ikabidi nimwamshe Mamdogo anitoe nje ili nitoe hiyo haja ndogo

Kwasababu Mamdogo alikuwa na usingizi kwa kutosha, ikabidi anipige biti la hatari na kufoka sana. Tukatoka, yeye akasimama mlangoni mie nikasogea kama mita nne hivi ili nijisaidie. Zile kelele za mother kufoka usiku akiwa mlangoni, tulisikia sauti ya kike kutoka nyuma ya jiko ikisema "MUACHE AKOJOE NAWEWE". Hahahahah!!! Sikutambua Mamdogo kaingia ndani sangapi maana kugeuka nyuma sioni mtu mlangoni. Kwakuwa nilikuwa mdogo niliendelea na haja yangu then nikarudi ndani......
Haaaaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]huyo alikuwa kibaka anakula Mingo aibe chochote. Itabidi akutete na ahirishe kuwaibia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutokana na hii Hali. Napenda kujua mchawi na mganga.je ni halali kwenda kwa mganga sababu unahisi mauzauza au kuchzewa kichawi?na je ni uchawi kweli unaweza kumfanya mtu awe chizi?tusaidiane kwa hili kwani sikuwa napenda kuamini kuwa ushirikina upo. Pili waubiri wengi wa Sasa hutupelekea kuamini uchawi upo na kulogwa kupo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jamaa angu alifumaniwa na mke wake,ugomvi ulikua mkubwa kiasi ya kwamba mwanamke alishaanza kufungasha mizigo yake aondoke,jamaa alichofanya alimpgia mtalaam wake simu aisee,baada ya masaa 5 mwanamke amesahau kila kitu,hali ikawa shwari

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Naomba namba za huyo mganga pls

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 1989 nilikwenda kijiji cha jirani nikanywa pombe sana.
Nilipokuwa narudi nikapita sehemu ambayo inasifika kwa mauza uza nikawa mbishi vile nimelewa siogopi.

Nikafika kichaka flani nikasikia nywele zimesimama nikahisi joto kali sana nikasikia harufu ya marashi mara ukawaka mwanga mkali pombe yote ikaisha.

Kesho yake nikamuhadithia bibi yangu akaniambia bahati yako pale kulikuwa na jini lipenda dini liivyoona unanuka pombe likaona ngoja huyu mchafu aende zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiki ni kama nilivyosikia kinasimuliwa juzi Kati.

Kuna jamaa walikuwa wanatoka dar kuelekea Mtwara,wakiwa njiani wakafika Lindi maeneo ya mandawa kuna kimlima hivi gari ikazingua kitu kidogo cha kurekebisha waendelee na safari mmoja wao akabanwa na haja ndogo akasogea akajisaidia basi tenngeneza gari likagoma.Dereva akapigiwa simu na dereva mwenzake akamueleza mahali walipo huyo dereva akasikitika aisee mmeharibikiwa hapo msala.

Gari likagoma ikabidi walale saa nane usiku wakashangaa dogo kama ana miaka 6 akatokea akasimama mbele ya ile gari akacheka sana Kwa nguvu akapotea jamaa uoga ikabidi wachune Tu ndani ya gari wanajisaidia kwenye chupa saa 12 asubuhi akaja jamaa kama chizi hivi akawa anaizunguka ile gari akasikitika anaongea mmepata tabu sana anazunguka tu, akaondoka akaja mbibi akasimama akaawangalia akaondoka kukawa kumekucha sasa wanapiga hesabu wafungue kifaa kilicho haribika wapeleke Kwa fundi,mmoja wao akataka kujisaidia tena ikatokea sauti ya mzee hakuna kujisaidia hapo ondokeni haraka huyo mzee akatokea wakamwambia gari ni mbovu akasema gari sio mbovu ondokeni dereva kuwasha gari nzima wakaendelea na safari kumbe kosa ni jamaa alivyojisaidia bwana.
 
Hii ilitokea Tanga wilaya M. Kuna mganga fulani alikua mganga akaona akatoe huduma za kiganga wilaya M akitokea wilaya K. Basi alifikia nyumba ya jamaa mmoja na kumueleza kwamba amekuja hapo kutoa huduma kama kuna mwenye tatizo lolote aje. Basi mganga akapewa chakula akala na kupewa mahali pa kulala. Muda kufika akaenda kulala na mikoba yake. Kulipokucha adibuhi mganga alijikuta yuko nyumbani kwake wilaya K na mke wake na mikoba yake
 
Kuna yoyote ambaye anakumbuka kipindi cha USWAZI cha Musa akiwa na Manyau Nyau? Manyau Nyau aliingia nyumba moja hivi Musa akawahoji tatizo ni nini hapa?

Wapangaji wakamwambia kuna ambaye anaishi kwenye hiyo nyumba ila hawamuoni.

Muda mwengine wakijisaidia haja kubwa wake kwa waume wanashangaa ghafla wanachambishwa halafu hawaoni mtu wala huo mkono uliyowachambisha!
 
Back
Top Bottom