Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kijiji kimoja mkoa X, mzee mmoja alipowaona kuku wa jirani wanashambulia mahindi shambani mwake akaamua kuwatimua kwa kuwapiga na mawe.
Alipoamka asubuhi akajikuta mguu mmoja umetoka uko pembeni hakuna damu wala nini, akiwa katika taharuki nini afanye akalala tena kuamka kesho yake mguu wa pili pia umetoka uko pembeni.
Mpaka leo huyo jamaa yuko na ameshakuwa mzee haelewi nini kilimkuta anatumia wheel chair, uchawi upo.
Hahahaha,duh Kuna watu wanakufuru yaani Kama dunia wameitengeneza wao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka flani wilaya ya rombo nimetoroka zangu shule usiku wa giza nene kias kwamba hata miti unaiona kwa tabu sana ,nikakatiza mitaa flani ilikua kipindi cha baridi lakini ghafla nikaanza kuhisi joto la hatari mara paaap kumekua kweupe kama mchana wa saa sita na jua kali aiseee nilitimua mbio ile hali ilidumu kama dk moja hivi

Ikawa mwanzo na mwisho kutoroka shule usiku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WANAODHANI HAKUNA UCHAWI , HAYAJAWAKUTA;
Miaka michache iliyopita nilikwenda RUKWA wilaya ya Nkasi nikiongozana na wenzangu tukiwa na watu Dr Livingstone Expedition waliokuwa wanafuatikia njia aliyotumia Dr Livingston toka Ujiji Kigoma hadi Zambia alipopata umauti.

Tulupofika kijiji kimoja kinaitwa Ntuchi (Nakikumbuka kwa tukio hili) tulikutana na kisa cha kustaajabisha kilichowakuta Maafisa toka Wizara ya Elimu Dsm waliokwenda kukagua shule za Sekondari Nyanda za juu na walipofika kwenye shule hiyo wakakutana na malalamiko ya Walimu juu ya vitendo vya kishirikina wanavyofanyiwa na wenyeji.

Maafisa wale wakawaita viongozi wa kijiji na wazee maarufu kuwakemea sana huku wakitishia kuwaondoa walimu wote endapo vitendo hivyo vitajirudia. Baada ya kumaliza kukemea jambo hilo wakiwa ofisini, walipotoka nje wakakuta gari lao halina upepo kwenye tairi zote 4, wakabaki wanashangaa. Walimuuliza dereva kimetokea nini naye akabaki anashangaa maana hajaona mtu yeyote akitoa upepo.

Walimwita fundi aangalie lakini kila alipojaribu kujaza upepo haukuingia. Walilazimika kuita baadhi ya wazee wakawaomba radhi na ghafla tairi zikawa na upepo kama awali. Waliapa kutorudi mkoa ule na sisi tukaendelea na safari yetu huku tukiwa na hofu kubwa.

Maafisa wale kama wamo humu JF watashuhudia tukio hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka ya nyuma tunatoka mererani usiku wa manane tuko na pikipiki almaarufu baja tullikutakana na moto mkubwa ukiwa umetanda barabarani kama vile unavuka ,tulikuwa sita tukajishauri sana lakini kwasababu tulikuwa wengi tulipata ujasiri wa kupita ila cha kushangaza tulivuka na hatukuungua wala kuhisi chochote kuangalia nyuma baada ya kuvuka moto uko vile vile
Jombaaa hii ilikuwa bangi zenu mlizovuta
 
digba sowey, Nina maswali
1. 1992 ulikuwa unafundisha shule X ila field ya kuwa mwalimu ukifanya mtwara sijui 2006...ulienda kujiendeleza?
2. Huyo aliyerudi na kuishi kwa wiki mbili aliokelewaje na familia yake na kijiji kwa ujumla?kwa hiyo aliwekewa tanga mara mbili?alizikwa mara mbili?
3. Huyo mwalimu mwenzio mlimchukuliaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali Namba jibu lake ni kuwa elimu haina mwisho,tambua kuna walimu wa cheti,diploma,shahada,masters NK.namimi katika andiko langu sijataja elimu yangu

2,swali lako la pili ni kuwa alipokufa tena Mara ya pili kwanza hakuzikwa nyumbani kwao ila alizikwa polini na hakukua na matanga tena,
Nina maswali
1. 1992 ulikuwa unafundisha shule X ila field ya kuwa mwalimu ukifanya mtwara sijui 2006...ulienda kujiendeleza?
2. Huyo aliyerudi na kuishi kwa wiki mbili aliokelewaje na familia yake na kijiji kwa ujumla?kwa hiyo aliwekewa tanga mara mbili?alizikwa mara mbili?
3. Huyo mwalimu mwenzio mlimchukuliaje

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mkaka alimaliza form 6 miaka hiyo ya 84
Akatafutiwa kazi lkn kila akiwa kazini akiandika mikono haiandiki inakuwa km mtoto wa miaka 2 au mmoja jinsi anavyojichorea hovyo,lkn akiwa home kwao au mishe za kikawaida sio za kazi anaandika vzr,basi ameishia kuwa fundi mafriji

Kuna mdada kipindi hicho sasa mmama,alikuwa amelala chumbani kwake karibu na dirisha akahisi kitu nje akachungulia na kumuona mtu mrefuuuu kavaa nguo nyeupe,kila akijitahidi aone sura yake yule mtu anazidi kurefuka,alikuwa amepata tungi mbona liliisha na kulala fasta

Mmama mwingine alikuwa anachelewa kurudi kazini na kuondoka mapema,saa 7 usiku akaamua kufua nguo zake,alikua anafulia uwani kwake,ghafula akahisi mwili na mywele kusisimuka,na kuhisi km mtu kamsimamia,kuinua shingo hamna mtu,lkn kamba inatingishika sana km mtu anaitingisha,akaamka na kuanza kusali
Akaingia ndani akasali sana,maana yeye ni kama mlokole,akomba mpk kutetemeka,usingizi ukampitia km dk 10,akaota anampigana na mwanamke jirani yake,akajiona kucha zake zimekua na kuziingiza ndani ya macho ya huyo mwanamke,mwisho mwanamke akauimia na kukimbia.
Baada ya siku 3 akapata taarifa huyo mama anaumwa sana mpk kapelekwa kwa ndg zake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu, mimi huwa nawashangaa sana watu wanaokana uwepo wa nguvu za giza (uchawi na ushirikina). Nadhani ni kwavile hawajawahi kukumbana na ushirikina. Na Mshana Jr huwa anapata wakati mgumu sana kuwaelewesha watu kuhusu mambo hayo.

Si ajabu hata comments tuzopandisha kwenye uzi huu wengine watafikiri ni story za kunogeshea baraza, la hasha! Mimi nina visa kadhaa nilivyoshuhudia:

1.Wakati nikiishi mkoani Mwanza, alikokuwa anafanyia kazi Mzee wangu, na nikiwa na miaka 11 tu, kuna siku wazazi wangu wakiwa wamelala huku wamefunga milango na madirisha yote, walikuja kugutuka kutoka usingizini mishale ya saa 9 usiku na kukuta madirisha yote ya chumbani kwao na mlango yamefunguliwa. Na kwavile kulikuwa na mbalamwezi, waliweza kuwaona bundi 4 wamesimama katika madirisha 2 ya chumbani huku wakiwatazama wazazi wangu waliolala kitandani. Baba alivaa ujasiri wa kuwatimua, ila baada ya kuamka watu 4 ndani ya familia tuliamka tukiwa tumechanjwa chale mwili mzima. Ilibidi familia iingie 'gereji' ndo mambo yakawa shwari.

2.Mwaka 1993 tukiwa tulipanga nyumba moja kule Tandika Mabatini, Dar es Salaam. Mwenye nyumba alitupa masharti kadhaa, kubwa kabisa likiwa ni katazo la kuingia nyumbani baada ya saa 6 usiku, au kwenda chooni/bafuni baada ya masaa hayo. Tulijitahidi kutii! Siku moja, mpangaji mwenzetu mmoja alikiuka masharti akaenda msalani saa 6 na ushee, tulisikia kelele za kuomba msaada, lakini hakuna aliyethubutu kwenda kutoa msaada. Kesho yake alfajiri tulimkuta jamaa bado ameanguka chooni. Mwenye nyumba alimfokea kwa 'kuyataka mwenyewe'. Ilibidi jamaa ahame nyumba baada ya siku 4. Ilikuja kubainika kuwa, Mwenye nyumba alikuwa anafuga majini na huwa anayafungulia masaa hayo yanaingia kazini, hivyo jamaa alikumbana nayo yakamshughulikia. Sisi nasi kwa uoga ilibidi tuhame kabla kodi yetu haijaisha.

3.Muda haunitoshi kusimulia nilivyokutana na wachawi ' live' mara mbili, wakati nikiishi huko Kanda ya Ziwa.
 
Aisee wadau wanamroga had mganga
Hii ilitokea Tanga wilaya M. Kuna mganga fulani alikua mganga akaona akatoe huduma za kiganga wilaya M akitokea wilaya K. Basi alifikia nyumba ya jamaa mmoja na kumueleza kwamba amekuja hapo kutoa huduma kama kuna mwenye tatizo lolote aje. Basi mganga akapewa chakula akala na kupewa mahali pa kulala. Muda kufika akaenda kulala na mikoba yake. Kulipokucha adibuhi mganga alijikuta yuko nyumbani kwake wilaya K na mke wake na mikoba yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii niliambiwa na jamaa yangu na ilimtokea Dar miaka ya hivi karibuni.

Jamaa waliitwa kwenye interview ya driving! Wakapita, wakaitwa kwenye second interview ambayo ndio angepatikana dereva sasa!

Jamaa akawapoteza wenzie yaani siku ya interview kaenda alone, wenzie hawajaja! Jamaa akapata kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah, hii ni hatari sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka kadhaa nyuma, bibi yangu mzaa mama, katika umri wake wa makamo, mrembo na mwenye kinywa kilichosheheni meno imara na meupeeee, aliamka asubuhi moja tusiyoisahau mpaka leo, kinywani akiwa hana jino hata moja. Alikuwa kibogoyo kabisa kama alizaliwa na kukua bila meno.

Wakati ukoo mzima tumetunduwaa kwa mshangao, jamii ilitutuliza kwa kutuambia kuwa tuwe wapole na habari ndiyo ilikuwa imekwisha hivyo. Kuwa bibi yangu eti alifanya uzembe wa kuamka na kupiga kelele akidai meno yake hayamo kinywani.

Kumbe ilimpasa, baada ya kuona kinywa chake kitupu, angerudi kimya kimya kulala. Meno yake yangerejeshwa na walioyaazima kwenda kutafunia nyama na bisi!! Ni juzi tu tumemzika bibi yetu akiwa kibogoyo kwa miaka kibao, kwani meno hakurejeshewa tena. Uchawi wa migombani Unyakyusa huu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom