Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Chukua weed (bangi) Choma humo ndani
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuh

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kuna watu wanajua kutesa binadamu wenzao, halafu unakuta wengine wamekuzidi kila kitu , ila hawataki kabisa mambo yako yawe mazuri, Sijui hyu uchawi wa aina gan


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli, ukiwa na imani Kali sana , na usiwe na dhambi , ila ushirikina una nguvu sana

Usichukulie poa nguvu za giza , Mimi nimejionea nyie mnasikia tu kwa watu[emoji16]


Sent from my iPhone using JamiiForums
Ndoto za ajabu naota mara chache sana kwa mwaka.
Wiki iliyopita niliota ndoto ya ajabu sana! Niliota nipo kwenye hekalu la kuabudu, ndani ya hilo hekalu walikuwemo watu wawili tu mimi ni watatu wao. Mmoja amesimama kwa mbali na mwili wake una mawimbi mawimbi. Mwengine alikuwepo karibu yangu.
Aliye karibu yangu alikuwa ananikaribia pembeni yake kulikuwa na kivuli kizito na chenye umbile tofauti na la kwake. Akakivua kile kivuli kwenye mwili wake kama mtu anavyovua nguo halafu akielekezea kije kwangu.

Kile kivuli kilinivaa mwili mzima! Mwili wangu niliusikia tofauti ya mwili wote ambao sikuwahi kuusikia. Halafu kikawa kinanivaa kuniingia mwilini huku nahisi maumivu, na kikanivaa mwili mzima!

Licha ya mapungufu yangu mengi ila najifahamu na Mungu ndiye anayejua zaidi. Mtume anasema Uislam una twariqah 360, yeyote atakayepita moja ya hizo twariqah yupo salama. Mi ni sunni, ni mtu wa twariqah! Nafuata twariqah ya Sheikh Abdul Qadir Al Jeilan. Ambayo hiyo twariqah ni moja ya 360. Huyu Abdul Qadir Al Jeilan ni kiongozi wa Mawalii(sage) wote. Atakayeifuata twariqah yake aliyeipitia yeye (twariqah ni njia) anasema ukiwa na shida uwe magharibi au mashriki ya Dunia au Kas au Kus ukimuita kwa kutaja jina lake tu atakusaidia.

Kwenye hiyo ndoto nikalikumbuka jina lake. Nikalitaja jina lake kama alivyosema atakusaidia, kilichotokea nikashindwa kutamka jina nikawa kama mwenye kigugumizi. Huku kivuli kikawa kimenivaa, mwili unaniuma nikawa nachoka nakihisi kabisa kinaingia mwilini. Nikataja jina lake kwa kumaanisha, sauti mdomoni hainitoki nikamtaja kwa moyo. Kile kivuli kikaanza kunitoka.

Maumivu ambayo niliyasikia yaliniumiza. Navuliwa kitu ambacho kinaniumiza ni kizito lakini ni kile kivuli kilichonivaa! Kilinitoka chote mwilini nikawa nahisi maumivu na nikawa nahema sana ila bado nipo kwenye ndoto. Aliyenitupia hicho kivuli kumuangalia yupo nje ya hekalu amesimama huku ananingalia. Lakini kile kivuli kilichonitoka kikawa kipo mbele yangu kimesimama kikamfuata aliyenitupia. Yule mwengine ambaye mwili wake una mawimbi mawimbi mda wote alikuwa amesimama tu! Kisha akawa ni mwenye kuondoka. Lakini bado mimi nilikuwa nahema sana huku nimeinama chini. Kwa ghafla akasimama na akanifuata huku akiniangalia.

Nikashtuka kutoka usingizini mwili ukawa unauma. Nikawa na wasiwasi nililala vibaya kuhusu haya maumivu ya mwili ama laa!
 
Uzuri uliishinda vita
Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji849][emoji849][emoji849] hii noma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya mambo ni masuala ya imani tena imani inayohusisha mtu mmoja mmoja. Na huwezi jua undani kama hayajakukuta.
Mchawi na baadhi ya waganga wanashirikiana. Kuna waganga hula rushwa kwa wachawi ili waachiwe mtu wanaemtaka,lakini pia wapo waganga wanaosaidia na wanakuwa kweli wamejaaliwa karama hiyo na wanakuwa hawali rushwa.
Si lazima kwenda kwa mganga kwa kuwa tuu unahisi mauzauza, unaweza zungumza na Mungu kwa njia ya sala tuu a ukapata uponyaji japo hapa inategemeana saana na imani yako iko kiwango gani. Hata kwa waganga pia haswa wale wanaotu miti kutibu.
Uchawi ama mchawi anaweza kukufanya ama kukutupia baya lolote analoweza kukunuia ww, binafsi almanusura niwe kichaa yaani nilikuwa hatua za mwisho kabisaa dah sitasahau maishani mwangu natembea kwa mguu mbezi kariakoo nenda irudi.
Wahubiri wengi wa kisasa hawakosei kuhusu wachawi kwani hata vitabu vitakatifu vimeeleza wazi kuhusu hili ila wameenda mbali zaidi wanatumia kujinufaisha na hapo ndipo wanapokosea sasa.
 
Duuh mkuu pole sana na ahsante kwa ufafanuzi pia uliponaje huo uchizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…