Hebu nisimulie hiki kisa changu...
Jumanne 23-08-2019.
Ilikuwa saa nne na nusu usiku nikiwa nimeketi sebuleni,mara gafula mzee akatoka chumbani na kuanza kunitukana matusi ya nguoni...
"Kijana gani wewe kazi kula na kujaza choo,huoni wenzio wanafanya kazi na wanategemewa na wazazi wao...ni bora ningezaa hata mbuzi ningefaidi mchuzi.."
Mara ghafula nashutuka kofi hili hapa sijakaa vizuri ngumi hii hapa,nikasimama imara na kumkazia tu macho...wadogo zangu na mama yangu wakitazama tu pasi na kusema neno.
Nikageuka taratibu na kutoka nje,chozi la uchungu likanitoka ilikuwa ni siku mbili tu toka nifukuzwe shule moja niliyokwenda kuomba ajira ya kujitolea..ati hawawezi kuajiri kiziwi!.
Nilitazama anga jeusi lililosheheni nyota nyingi,mwezi uliotoa nuru angavu nikajiuliza "Mungu upo wapi?".. Nikaingia chumbani na kuvaa viatu.. Nikatoka naenda wapi? Sijui!
Nikaambaa nisijue kama nakanyaga ardhi au ninapaa,napishana na mtu ama kisiki,ilinichukua nusu saa kuuacha mtaa wetu nikaingia mtaa wa pili,huu ulikuwa na watu wachache zaidi na nyumba zilikuwa mbalimbali kiasi.
Nikakatiza pembeni ya makaburi,nikasimama,nikayatazama na kujiuliza " kwanini nisingekuwa nimelala pale? Nipumzike!"...loooh lakini sauti nyingine ikaniambia "una uhakika ukilala pale utapumzika? Nikagutuka nikatazama huku na huko hakuna kiumbe nikaongoza njia kuliacha eneo la makaburi na kuzidi kupotelea mbali zaidi na nyumbani.
Hatimaye nikawasili sehemu pweke,barabara kubwa ya kokoto,kulia na kushoto kukiwa na msitu na vichaka vingi,kiza ni kingi kutupia macho simu yangu ni saa sita na robo usiku!
Ikafika mahali kuna njia panda na upande wa kulia kuna mti mkubwa sana aina ya mbuyu mahali pana pana joto sana bwana,pana joto kali,mapigo ya moyo yakanienda mbio " duuucha dunduncha ducha dunduncha" sasa mapigo niliyasikia hadi masikioni..
Nywele zikanisimama na vipele vya uoga vikanitoka hewa ikawa nzito na uvumilivu ukaniisha na sasa nikatimua mbio hata nilipoliacha eneo lile kwa umbali wa mita mia mbili hivi,na sasa nikaanza kutoka katika makazi ya watu.
Kufika hapa ikanipasa kujiuliza ni wapi naelekea,sikuwa napajua napoelekea kumbukumbu ya misukosuko ya kimaisha na masimango yasiyoisha zikanijia,woga wote ukabiisha donge zito la uchungu,hasira na kukata tamaa likanivaa,machozi yakanitoka,nikashika njia na kuendelea na safari,safari isiyojulikana!
Baada ya mwendo wa dakika ishirini hivi nikaingia katika barabara kubwa ya lami,nikashika uelekeo wa kushoto,ilielekea ufukweni,baada ya masaa mawili hatimaye nikawasili ufukweni,nikazitupia macho hoteli kadhaa zilizotamalaki eneo lile,nikaachana nazo na kushuka mchangani mbali kidogi na mahoteli yale,nikajikalisha kitako na kutafakari nilipotoka,nilupo na ninapoelekea,lakini mbona mbele kyna kiza kizito!
KIZAAZAA!
Hatimaye saa tisa ikawadia,nilichoka,na sasa ilikuwa ni safari ya kurudi,nikajizoa zoa na kushika njia kurudi nyumbani,bahati nzuri barabara hii ilikuwa na taa hivyo ikawa ahueni kwangu.
Baada ya mwendo wa dakika arobaini hivi nikahisi kama kwamba kulikuwa na mtu nyuma yangu,nikageuka kwa kasi, ebo! Nikaona nguo ya rangi ya khaki,aidha gauni au kanzu ikiishia na kufutika machoni kwangu....
Mshtuko uluonipata ukanifanya hata nguvu za miguu ziniishie nikajikuta nikiketi katika mfereji mfupi uliojengwa pembeni ya barabara.
"Ni nini hiki? Ni kweli au ni mawazo yangu tu?" Nikajiuliza,nukatazama huku na huko hali ni shwari,labda niliangalia vibaya bwana nikajizoazoa na kuendelea na safari..
Kiroja kingine tena! Ati nina vivuli viwili,kimoja ni changu na kimoja kimevaa kanzu kama si gauni!(mataa ya barabarani yanawaka hivyo mtu akipita kivuli chake kinaonekana kwa ufasaha kabisa) nikatetemeka kwa woga,nikageuka nyuma ati nacho kikageuka! Nikawa natembea kwa kurudi kinyume nyume,ati nacho kinarudi kinyume nyume!.
Lakini mbona kivuli changu kupo mbele yangu hiki cha nyuma ni cha nani? Na tumeachana umbali wa hatua kama tatu hivi toka kilipo hadi nilipo,nikaona huu sasa utani,nikifa si nife tu ebo! Nikakata shauri kukifuata he! Ati nacho kinageuza kila nikikifuata nacho kinaenda nyuma zaidi,ikabidi nikikimbize sasa..kikapotea.
Nikageuka na kuanza kukimbia kwa taratibu mithiri ya mbio za riadha,nikachoka nikaanza kutembea baada ya mwemdo mrefu kivuli kile kikarudi! Sikusimama nikaendelea kutembea tu.
Hata hivyo nikaanza kuhisi mwili kuchoka sana,miguu inauma na usingizi ni mwingi sana,nikajikalisha juu ya ukingo wa karavati kutafuta pumzi maana ilikuwa ni safari ya masaa mawili zaidi hadi nifike nyumbani...nikaanza kusinzia na hatinaye fahamu zikakomea hapo.
Kelele za watoto wakicheza ndizo zilizonigutusha,nikafumbua macho..afanalek! Nilikuwa nimelala chumbani kwangu..miguu ilikuwa imevimba kiasi na mwili mzima ulikuwa unaniuma...
"Lakini mimi mbona nilikuwa kule barabarani?" Nikajiuliza nisijue kilichotokea,nikaamka na kulibinua bati ninalotumia kama mlango,nikapenyeza kiubavuubavu hadi nje.
Nikawatazama nyusoni niliowakuta nje,wapo kawaida,hawana hata habari,pengine niliokotwa na wasamaria wema! Lakini mbona watu wapo kawaida kama hakuna kitu?...nikashindwa kuvumilia nikaamua kumuuliza mama ni muda gani niliingia kulala!
Akanijibu "we si uliingia kulala saa nne weww? Maswali gani hayo usinisumbue" ni nani aloyenirudisha nyumbani,na kile kivuli ni kiumbe gani? Je ndicho kilichonirudisha nyumbani? Lakini hakijanidhuru, hili ni fumbo niishilo nalo hata sasa kuna wakati natamani kukiona tena kivuli kile kilichovalia kanzu au gauni lililopauka lakini hakitokei tena.
Sent using
Jamii Forums mobile app