mjanja wa kijiji
JF-Expert Member
- Oct 2, 2018
- 1,582
- 4,378
Duh,mwambie aangalie hata muandiko uko tofauti
ngoja nikuchongee kwa MOD mimi kwa ukuda ndio mwenyewe.
haa haaa haaaaa mkuu achaa achaaa haa haaa acha asee ukuda so poa(natania tuu)... But its true hapo ni pipo tofauti kabisangoja nikuchongee kwa MOD mimi kwa ukuda ndio mwenyewe.
Biashala ina mambo mengi ndug u uchawi ktk biashala upo nakupa kisa kimoja hivi miaka ya nyuma nilifanya biashala ya duka maeneo ya kwa mkandawile huko nikawa nikiweka mtaji biashala nauza vizuri ila hela jioni siioni nikajiongeza mana pale kulikuwa na waha wanauza hao mpk basi basi nikaenda sehemu kwa mzee mmoja kule Kunduchi yy ni marehemu kwa sasa akaniangalia nyota akasema inabidi kazi yako tuifanye siku ya j5 kulingana na ulivyo ila apatikane kuku mweupe ambaye tutatoa damu yake kweli nikaacha hela ya kuku pale nikaondoka siku nimefika akafanya mambo yake na akanichanja chale kadhaa mwilini yule mzee ni mha akaniambia nakupa hii azima kaiweke dukani kwako huyo ni jini atakuwa anakujazia bidhaa pale dukani na ndio wafanyabiashala wakubwa wanamtumia akanipa na masharti kadhaa basi nakumbuka nilikimbiza pale ila nilikuja kukosea sharti moja kila kitu kikafa ila tangu hapo hakuna ninachofanya kikaenda sawa tena mpk sasa
Mkuu kiimani ni watu wachache sanaa katika huu ulimwengu wenye uwezo wa kuzaliwa kama wako, hii ni karama adimu sana ambayo M/Mungu huwajaalia waja wake ili kujidhihirisha na wasioamini waamini ya kamba yupo na anatenda.Ndoto za ajabu naota mara chache sana kwa mwaka.
Wiki iliyopita niliota ndoto ya ajabu sana! Niliota nipo kwenye hekalu la kuabudu, ndani ya hilo hekalu walikuwemo watu wawili tu mimi ni watatu wao. Mmoja amesimama kwa mbali na mwili wake una mawimbi mawimbi. Mwengine alikuwepo karibu yangu.
Aliye karibu yangu alikuwa ananikaribia pembeni yake kulikuwa na kivuli kizito na chenye umbile tofauti na la kwake. Akakivua kile kivuli kwenye mwili wake kama mtu anavyovua nguo halafu akielekezea kije kwangu.
Kile kivuli kilinivaa mwili mzima! Mwili wangu niliusikia tofauti ya mwili wote ambao sikuwahi kuusikia. Halafu kikawa kinanivaa kuniingia mwilini huku nahisi maumivu, na kikanivaa mwili mzima!
Licha ya mapungufu yangu mengi ila najifahamu na Mungu ndiye anayejua zaidi. Mtume anasema Uislam una twariqah 360, yeyote atakayepita moja ya hizo twariqah yupo salama. Mi ni sunni, ni mtu wa twariqah! Nafuata twariqah ya Sheikh Abdul Qadir Al Jeilan. Ambayo hiyo twariqah ni moja ya 360. Huyu Abdul Qadir Al Jeilan ni kiongozi wa Mawalii(sage) wote. Atakayeifuata twariqah yake aliyeipitia yeye (twariqah ni njia) anasema ukiwa na shida uwe magharibi au mashriki ya Dunia au Kas au Kus ukimuita kwa kutaja jina lake tu atakusaidia.
Kwenye hiyo ndoto nikalikumbuka jina lake. Nikalitaja jina lake kama alivyosema atakusaidia, kilichotokea nikashindwa kutamka jina nikawa kama mwenye kigugumizi. Huku kivuli kikawa kimenivaa, mwili unaniuma nikawa nachoka nakihisi kabisa kinaingia mwilini. Nikataja jina lake kwa kumaanisha, sauti mdomoni hainitoki nikamtaja kwa moyo. Kile kivuli kikaanza kunitoka.
Maumivu ambayo niliyasikia yaliniumiza. Navuliwa kitu ambacho kinaniumiza ni kizito lakini ni kile kivuli kilichonivaa! Kilinitoka chote mwilini nikawa nahisi maumivu na nikawa nahema sana ila bado nipo kwenye ndoto. Aliyenitupia hicho kivuli kumuangalia yupo nje ya hekalu amesimama huku ananingalia. Lakini kile kivuli kilichonitoka kikawa kipo mbele yangu kimesimama kikamfuata aliyenitupia. Yule mwengine ambaye mwili wake una mawimbi mawimbi mda wote alikuwa amesimama tu! Kisha akawa ni mwenye kuondoka. Lakini bado mimi nilikuwa nahema sana huku nimeinama chini. Kwa ghafla akasimama na akanifuata huku akiniangalia.
Nikashtuka kutoka usingizini mwili ukawa unauma. Nikawa na wasiwasi nililala vibaya kuhusu haya maumivu ya mwili ama laa!
Duh pole sanaa mkuu, ulimwengu wako wa kipato ushatawalia hapo.Kumpata si rahisi kihivyo kazana sana maombi kwa kufunga katika mjumuisho wa siku 7 au 21 kama unaimani haswa na Mungu amekupa karama utajibiwa ila ni lazima uachane na yoote amabayo ni chukizo kwa Mungu.Nimeajiriwa lakin mambo yangu hayaendi mpaka Leo, unakopa mkopo wanakukata alafu inafikia kipindi unaambiwa makato hayaendi benk husika, unarudi nyumbani migogoro isiyoisha yaan n tabu tu, nishasema nikija kumfaham mbaya wangu ntamfanyia mbaya sana
Sent using Jamii Forums mobile app
Sanaa sanaa mkuu me huwa nawaangalia wazee wa leo mtu ana mvi lakini unakuta ni masikini wa kutupwa mpaka huwa najiuliza hivi huyu miaka yoote alikuwa anafanya nini hapa dunianii!!! Kiukweli wengi wanawafanyia wengine kazi hapa duniani.Watu wana vifungo vya nguvu za giza , watu wengi wanateseka na kuaribiwa maisha na nguvu za giza it’s not a small matter .
Twende mbele turudi nyuma , Tanzania kuna wachawi wa kutisha, Mabilionea wengi ndan na nje ya nchi wanakimbilia Kwa waganga kuchukua nguvu za kiroho /giza . Na mtu akishaingia kwneye nguvu za giza ni ngumu sana kupambana nae , ngumu sana Sijui uwe na nguvu za Mungu kias gani Ndo Uweze kujinasua
Sent from my iPhone using JamiiForums
Mwalimu Christopher Mwakasege liked your post.Mkuu kiimani ni watu wachache sanaa katika huu ulimwengu wenye uwezo wa kuzaliwa kama wako, hii ni karama adimu sana ambayo M/Mungu huwajaalia waja wake ili kujidhihirisha na wasioamini waamini ya kamba yupo na anatenda.
Si watu woote hupata bahati ya kupata ujumbe kupitia malaika kama ilivyo ww na ndo wengi wanateswa sanaa na wale waovu.
Aliyekuwa akipambana ni malaika wako kukuokoa maana ulikuwa kwenye mchakato wa kuingizwa kwenye kazi maalumu. Mshukuru Mungu mkuu kwa kipawa alichokujaalia watu aina yako hata wakifanya sala kwa ajili ya wengine hufanikiwa kwa haraka kupata majibu
Kwa imani mkuu naamini hivyo. amani iwe nawe pia.Mwalimu Christopher Mwakasege liked your post.
Dah unajua kuna vitu ndugu yangu si rahisi kuvikwepa kwa mfano sharti nililokosea mie kama ingekuwa sasa hivi ingekuwa rahisi kulidhibit mana angalau nimekua sasa sharti kubwa nilijisahau kuwa ukifanya mapenzi na mwanamke uhakikishe usiiguse ile azima mpk siku saba sasa dah ikawa bahati mbaya
Hii ya kuitwa imenitokea juzi pia..Week iliyopita nimejilalia zangu..Kuna muda nikastuka nikaingia jf usiku wa manane nikachat weeh..muda wangu wa kusali ukawa umefika nikajisemesha sisali leo ngoja nilale..nikazima tochi ya simu nikaweka simu pembeni nikasikia sauti dirishani imeita jina langu Mara 3..weweee..nilipatwa na joto la ghafla nikatoa sonyo huyo nikalala zangu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee mpaka wauza Karanga wanatengeneza mambo yao..Kuna mahali niliwahi sikia, biashara bila kuitengeneza kidogo ni nadra sana kutoboa
Sent using Jamii Forums mobile app
Zinaonekana na kuuzika zinauzika sana ni ishu ngumu kuielezea hapajini atakuwa anakujazia bidhaa pale dukani
Jini anajaza duka kiukwel kwel kabsa na au n visually tu kwamba zinaonekana ila haziwez kuuzika, hii imekaaje mkuu?
Thanks huu ndo ukweli wenyewe.Shetani na mawakala zake wana operate kwenye ulimwengu wa giza / Roho ambao sisi binadam wa kawaida hatuna uwezo huo . Na shetani ni mjanja na ana akili sana .
Kama umeamua kupambana na shetani , hakikisha una imani dhabiti iliyonyooka, don’t understimate the devil [emoji49]. Usifikiri unaweza kumchallenge shetani kipumbavu, remember shetani Ana uwezo wa kiungu, Ana Uwezo kama Mungu .
Inshort Shetani pia ni mungu, ingawa kazi zake nyingi ni uharibifu, lakin Shetani pia kuna mambo mengi tu mazuri anayafanya kama Mungu , kuponya watu , kuwapa watu utajiri na Mali , shetani Ana uwezo wa kufanya yale Mungu anayoyafanya so wewe binadamu wa kawaida usifikiri unaweza kupambana nae au kum oppose kirahis kama wengi wanavyofikiria.
If you can’t fight them , join them .
Mimi sio mpinga kristo , na wala sina nia ya kuingiza watu kuzimu,
the truth is , the best coffee is always DARK and BITTER .
Hata hao wachungaji mnaokimbilia kuombewa na kuponywa na kuchukua miujiza, wanaenda kuchukua nguvu kwa Mkuu wa ulimwengu huu ( lucifer)
Tena wanaenda kujinadi kabisa kanisan na kulitaja jina la Yesu bila aibu yeyote , na kupitia hilo hilo jina, watu wanaponywa. That’s how the devil operates .
Warumi
Sent from my iPhone using JamiiForums
Ina nitokea sanaMkuu kiimani ni watu wachache sanaa katika huu ulimwengu wenye uwezo wa kuzaliwa kama wako, hii ni karama adimu sana ambayo M/Mungu huwajaalia waja wake ili kujidhihirisha na wasioamini waamini ya kamba yupo na anatenda.
Si watu woote hupata bahati ya kupata ujumbe kupitia malaika kama ilivyo ww na ndo wengi wanateswa sanaa na wale waovu.
Aliyekuwa akipambana ni malaika wako kukuokoa maana ulikuwa kwenye mchakato wa kuingizwa kwenye kazi maalumu. Mshukuru Mungu mkuu kwa kipawa alichokujaalia watu aina yako hata wakifanya sala kwa ajili ya wengine hufanikiwa kwa haraka kupata majibu
kama ni hivyo bas naona hamna haja ya viwanda. Serikali inatakiwa iinvest kwenye utaalam huu kama mbadalaZinaonekana na kuuzika zinauzika sana ni ishu ngumu kuielezea hapa
Una matatizo yako wewe, hakuna uchawi hapo. Hizo ni stress, tafuta pesa.Usemacho ckupingi Mimi mwenyewe hapa kuna uchawi nimefanyiwa sijui nimetupiwa jini sielewi
Nakumbuka kuna Banda niliwahi kupanga uswahilini, basi katka Ile nyumba nilikua naishi na mama wa kiha ambaye alikua na watoto watatu
Asa cjui kitu gani nilichomkosea Yule mama nakuanza kunitesa nakumbuka kuna siku mjuu wake aliingia ndani kwangu na sikua na mazoa na Yule mtoto basi alipokua mle ndani akaanza kuchezea vitu mara anachukua sabuni anamwaga, bodysray anairusha juu , mafuta anayamwaga nukimkataza anakua mkali kweli mwishiwe nikamuita mama yake akaja kumchukua
Cku nyingine aliingia ndani na kupanda kitandani kwangu then akawa anatambaa kama nyoka pale kitandani kwangu na akawa amekakamaa sana
Basi siku zilivyenda nikawa nikilala pale kitandani naota mambo ya ajabu sana haitoshi kuna kitu nakihisi kinatambaa nikikiangalia sikioni
Ikafika kipindi nikilala pale kitandani mchana naongea peke yangu yaani yanajirudia matukio kibao ambayo niliyasahau na nakua na hasira sana yakutaka kwenda kulipiza kisasi
Inshort mpaka muda huu hilo tatizo linanisumbua mkuu nashindwa nilitatue VP cjui.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mbaya wako yuko kichwani kwako.Nimeajiriwa lakin mambo yangu hayaendi mpaka Leo, unakopa mkopo wanakukata alafu inafikia kipindi unaambiwa makato hayaendi benk husika, unarudi nyumbani migogoro isiyoisha yaan n tabu tu, nishasema nikija kumfaham mbaya wangu ntamfanyia mbaya sana
Sent using Jamii Forums mobile app
Una matatizo yako wewe, hakuna uchawi hapo. Hizo ni stress, tafuta pesa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Soo kip wanakihiitajiUkiona tajiri au msanii anagawa pesa hovyo ogopa sanaa ogopa mnoo yaani kimbia haswaa. Hakuna bure hii dunia ya tatu aisee ogopa sanaa wagawa pesa iwe kwa kurusha ama kwa kugawa taratibu.
Kama wanania ya kusaidia watu si wakajenge vituo vya afya huko watu wapate huduma ya kudumu.