Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Ukiuliza NDICHELIWE GUEST aliyekuwa RCO Iringa baadaye RPC Dodoma Omary Mganga aliwahi kukimbia nje na boxer kutokana na mauzauza aliyoyaona hapo Guest lakini ni hapo hapo guest ukitaka story za hilo tukio utazipata.
 
Ukiuliza NDICHELIWE GUEST aliyekuwa RCO Iringa baadaye RPC Dodoma Omary Mganga aliwahi kukimbia nje na boxer kutokana na mauzauza aliyoyaona hapo Guest lakini ni hapo hapo guest ukitaka story za hilo tukio utazipata.
Huyu Omary Mganga alikuwa RCO Masasi, then uRPC alianzia Iringa na mwishowe akastaafia Dodoma mkuu. Baada ya kustaafu alifanya kwa mkataba TAMISEMI miaka kama miwili ndio akastaafu mazima.
 
Wachungaji tuwape heshima zao ,na hizo sadaka wanahaki kuzipata tu.
 
Mimi natumika kanisa fulani kama mjoli wa Bwana Yesu. Uchawi upo lakini hauna nguvu kama hujajiunganisha nao. Mama yako mkubwa kuombewa na kushindikana sio kwamba Mungu hana nguvu au hatendi, ila alijiunganisha na nguvu za giza hususan alipoenda kwa waganga ndio maana ulimpa uhalali Ibilisi kumuonea na hatimaye mauti. Hii ndio changamoto kubwa inayotesa wengi.
Upitapo kwenye Jaribu la kulogwa, ukienda kwa waganga ndio kwisha habari yako kwani Shetani hawezi mtoa shetani mwenzako. Unatakiwa usimame na Mungu tu tena kwa kumaanisha japo pia hii ni neema na ufunuo wa kimungu.
Pole sana ndugu yangu.
 
Uchawi upo sema tu kuamini kunakuja kama mtu ameshawahi kupitia mauzauza au laaa.

Kipindi nasoma shule ya msingi miaka hiyo nakumbuka nilikuwa nachuana na binti mmoja. Akishika namba moja mm namba mbili. Nikishika namba moja basi namba mbili.

Baada ya muda ikawa kila ukifika wakati wa mtihani naumwa napelekwa hospitali. Hali hiyo ikatokea kama mara 6 mfululizo.
Siku moja Dr wa hiyo hospitali alikuwa anafahamiana na bi mkubwa akamwambia mwanao hataki shule kila siku anaumwa yeye tu. Ndipo bi mkubwa akashtuka.

Hali ile ikaja kujirudia siku ya mitihani umefika mi naumwa bahati nzuri yule binti niliyekuwa nachuana naye akaja kuniona basi bi mkubwa akatoa la moyoni mbele yake akasema " kila mitihani unapokaribia mwanangu anaumwa sasa mwaka huu nataka nijue kinachofanya huo ugonjwa uwe unasubiri mitihani tu." Wote tukabaki kimya yule binti wala hakujibu chochote.

Toka siku hiyo miaka ikaenda sikuwahi kuumwa tena hadi Leo hii sijawahi kuumwa hata malaria namshukuru Mungu.

Lakini baada ya kumaliza Elimu ya msingi tulipangiwa shule tofauti nilikuja kusikia kumbe yule binti alikuwa na tabia ya kuchuka akili za watu. Alivyoenda sekondari alikutana na wajanja wenzie ndo ikajulikana.

Kwa sasa hivi hata sijui yuko wapi.
 
Uchawi upo sana me mwenyewe kuna Mganga aliniambia ili ufaulu mtihani nitajie jina la mwanafunzi anaefanya vizuri hapo shuleni kwenu pia unipe na namba yake ya mtihani

Aisee niliogopa pia nikaona bora nifeli tuu kuliko kupata one halafu kumbe ni akili za mwingine
 
Kisa kingine nakumbuka Maza alikuja kijijini kutokea Dar na kiukweli mama alikuwa hana maelewano mazuri na mama mkwe wake ambaye sisi tunamwita bibi

Ile nimetoka kwa bibi ili niende nikamsalimie na nipate vizawadi aisee ile nataka kumuhagi mama nilijikuta naishiwa nguvu na kujikuta napepesuka na kuanguka chini huku nikiwa nimefumba mdomo

Kumbe Bibi aliniingia mwilini mwangu na endapo ningemuhagi mama basi angekumbwa na matatizo eidha kuumwa na kufa kabisa ila inaonesha mama alikuwa na kinga kali sana.

"2006" ilikuwa
 
Nyie kwenu ni walozi

Sent from my Infinix X624B using JamiiForums mobile app
 
Nimecheka sana. Amekutana na wenyeji, hotatenaneee, kwaakua mbui.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…