Hapo Mwanza shule ya Pamba Sekondari anasimulia dereva wa pick up zilizokuwa zikipaki hapo miaka ya 2000 mwanzoni, sijui sasa hiv kama bado zipo.
Alikuja jamaa kutokea Magu, ndani huko kijiji nimesahau, alikuja Mwanza mjini kununua vifaa vya ujenzi, kanunua alivyotaka akamaliza akawa anatafuta usafiri wa kumpelekea vitu vyake nyumbani kwake.
Kafika kwa wale jamaa, akamfata wa kwanza akamuuliza vinakokwenda akaambiwa, dereva akakataa, dereva wa pili akakubali akajua kalamba dili, akamtajia bei, yule mteja akamwambia hakuna tabu. Wakaenda dukani wakapakia safari ikaanza.
Wamefika Magu mjini wakapaacha, wakaingia ndani huko ki pick up kinachanja mbuga tu safari imewiva, kwenda mbele mwendo ukawa unapungua gari inaelemea upande mmoja, dereva akastuka akasimamisha gari, kufika kwenye tairi kitu upepo umepungua mnoo, jamaa ikabid apige jeki abadili tairi. Akamaliza safari ianze, tairi nyingine ikapata pancha tena, dere hajakaa sawa akasikia tumbo limemvuruga akamwambia jamaa asikilizie kimtindo atafute chaka ajisitiri, akapata.
Ile jomba dere ameshusha suruali achutame, ile anashuka ashushe mzigo akasikia anajiburuza kwenye ukuta wenye upele, acha jamaa atoke mbio urud kwenye gari! Yule mteja wake akamuuliza, kulikoni tena, jamaa akamsimulia alichokutana nacho, yule mteja akacheka kweli kweli akamwambia sasa wewe ulitaka kujisaidia ukutani kwa watu!? Dereva anashangaa tu, ukuta uko wapi pale!? Yeye anaona vichaka tu na miti ya mbali mbali.
Yule mteja wake akajitambulisha kwa dereva akambia yeye ni mganga wa kienyeji na pale walipo ni Gamboshi, kama alikuwaga anapasikia basi ndio eneo walilopo. Yule mganga akampaka dawa machoni yule dereva akamuonesha ule mji ulivyo. Dereva anasimulia anasema hajawahi ona mji mzuri kama ule, si kwenye sinema wala picha. Ni mzuri hatari, na watu wana shughuli zao kama kawaida ila wako uchi na hakuna anaemshangaa mwenzie. Akamuonesha na ukuta aliotaka kuunyea akajiparua kalio. Yule mganga akazipaka tairi dawa zote zikakaa sawa, na ile ilofunguliwa akaiangalia ni nzima! Safari ikaendelea, alipofika kwa mganga akaoneshwa njia nyingine akarudi.