Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kumbe uchawi mpaka wajue detail zako, na uchawi hauwezi kufanyika bila kua na hizo detail

Kama haiwezekani kupata detail kwa kutumia uchawi, sasa mbona vijiweni kuna stori mingi kua waganga wanaagua bila wewe kusema chochote wewe hii unaizungumziaje? Kwako mwalim kashasha

It's Scars
Uchawi hauitaji details, uchawi unataka sababu tu mtu akipata sababu hata ya kukusababishia unakwenda na maji. Anaweza akaja kukuomba chumvi kile kitendo cha kumnyima tu ni sababu tosha, '' ''tunayaweza yote katika yeye atutiaye nguvu''.
 
Nikiwa na miaka Tisa ya ndoa yangu sikuwahi dhani wala kujua wife ni mchawi maana alikuwa msomi wa juu sana na mtu wa kanisa sana.siku moja nikiwa nimelala ulivuma upepo mkali mno gafla nikiwa macho nikajikuta nanyanyuliwa juu aisee nilisali sala zote gafla nikarudishwa chini.Kuangalia pembeni yangu alipolala mwenzangu naona mbwa aisee ulikuja kama usingizi hivi sekunde wife akarudi ktk hali yake ya ubinaadamu.Kesho yake nikahama home na ndoa ikafa.


Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kama sio chai aisee ni balaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka ya nyuma tunatoka mererani usiku wa manane tuko na pikipiki almaarufu baja tullikutakana na moto mkubwa ukiwa umetanda barabarani kama vile unavuka ,tulikuwa sita tukajishauri sana lakini kwasababu tulikuwa wengi tulipata ujasiri wa kupita ila cha kushangaza tulivuka na hatukuungua wala kuhisi chochote kuangalia nyuma baada ya kuvuka moto uko vile vile
HahahahaHahahah
 
Miaka kadhaa iliyopita enzi ya mpira wa sodo a. k. a chandimu kulikua na mechi ya fainali kugombea mbuzi kati ya timu X na timu Y. Sasa siku chache kabla ya mechi timu X ilienda kwa mganga kuroga ili wapate ushindi, kufika kwa mganga kama kawaida mganga akaanza na ramli. Baada ya kupiga ramli kwa muda kidogo mganga anasema matokeo yanaonesha mtapigwa bao 1-0 (kumbe wapinzani nao walishaenda kuroga kwa mtaalam wao), duh jamaa wakapagwa mganga tusaidie kupindua matokeo. Mganga akasema itawezekana kupindua matokeo kama mtaniletea papai liliozaliwa peke yake kwenye mpapai. Basi jamaa wakaanza kuhangaika kutafuta mpapai uliozaa papai moja tu ili wampelekee mganga apindue matokeo. Cha kusikitisha mpaka siku ya mechi jamaa walikosa kabisa mpapai uliozaa papai moja, hakuna jinsi wakaingia uwanjani hivyo hivyo.
Full time : X 0-1 Y Jamaa wakalala kama alivyosema mganga [emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina kisa kimoja kilitokea Huko MWANZA nyegezi ndani ya Saut Kuna makabuli pale wakiristo wanazikana basi siku yenyewe ilikua jioni sasa akaibuka kiumbe mmoja binti anamanywere mengi basi Tuliokua pale chuoni kusikia hivyo wote mbio kumuona aliefufuka radio ya chuo ikawa inatangaza mtu kafufuka kilikua kimbembe cha hatari police walikuja wakauchukua wakampeleka Bugando wenyeji Kumbe walikua wanajua hadi kwao alikufa miaka kazaa badaa ya kumaliza shule hapo shule ya msingi nyamalango akaugua maralia kwa mjibu wa mama mzazi jina kama namkumbuka walikua wanamwita Maria gembe hakukaa Sana pale Bugando C1 akafa tena. Ngoja niishie Hapa
 
Nadhani alikuwa msumbufu huko gamboshi ndo maana wakamrudisha
Nina kisa kimoja kilitokea Huko MWANZA nyegezi ndani ya Saut Kuna makabuli pale wakiristo wanazikana basi siku yenyewe ilikua jioni sasa akaibuka kiumbe mmoja binti anamanywere mengi basi Tuliokua pale chuoni kusikia hivyo wote mbio kumuona aliefufuka radio ya chuo ikawa inatangaza mtu kafufuka kilikua kimbembe cha hatari police walikuja wakauchukua wakampeleka Bugando wenyeji Kumbe walikua wanajua hadi kwao alikufa miaka kazaa badaa ya kumaliza shule hapo shule ya msingi nyamalango akaugua maralia kwa mjibu wa mama mzazi jina kama namkumbuka walikua wanamwita Maria gembe hakukaa Sana pale Bugando C1 akafa tena. Ngoja niishie Hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2005 hapo Tarime Secondary kuna jomba mmoja alikuwa ni classmate Msukuma huyo kutoka Magu ndani huko aliitwa Kija Charles.

Hiyo siku tupo prep, kuna mdada mmoja alikuwa na majini, akapandisha bana siku hiyo, watu taharuki, sasa yalivyokuwa yanazungumza yakamtaja huyo mlozi na alichotaka kumfanyia akashindwa. Kumbe yule jomba alishatomber dorm moja zima, la pili alikuwa kafika nusu, wadada wakaandamana kumtafuta huku kelele zikiwa zimetamalaki madarasani. Hakuonekana shule karibia wiki nzima.

Kumbe jamaa alikuwa anawatomber kichawi
 
Hapo Mwanza shule ya Pamba Sekondari anasimulia dereva wa pick up zilizokuwa zikipaki hapo miaka ya 2000 mwanzoni, sijui sasa hiv kama bado zipo.

Alikuja jamaa kutokea Magu, ndani huko kijiji nimesahau, alikuja Mwanza mjini kununua vifaa vya ujenzi, kanunua alivyotaka akamaliza akawa anatafuta usafiri wa kumpelekea vitu vyake nyumbani kwake.

Kafika kwa wale jamaa, akamfata wa kwanza akamuuliza vinakokwenda akaambiwa, dereva akakataa, dereva wa pili akakubali akajua kalamba dili, akamtajia bei, yule mteja akamwambia hakuna tabu. Wakaenda dukani wakapakia safari ikaanza.

Wamefika Magu mjini wakapaacha, wakaingia ndani huko ki pick up kinachanja mbuga tu safari imewiva, kwenda mbele mwendo ukawa unapungua gari inaelemea upande mmoja, dereva akastuka akasimamisha gari, kufika kwenye tairi kitu upepo umepungua mnoo, jamaa ikabid apige jeki abadili tairi. Akamaliza safari ianze, tairi nyingine ikapata pancha tena, dere hajakaa sawa akasikia tumbo limemvuruga akamwambia jamaa asikilizie kimtindo atafute chaka ajisitiri, akapata.

Ile jomba dere ameshusha suruali achutame, ile anashuka ashushe mzigo akasikia anajiburuza kwenye ukuta wenye upele, acha jamaa atoke mbio urud kwenye gari! Yule mteja wake akamuuliza, kulikoni tena, jamaa akamsimulia alichokutana nacho, yule mteja akacheka kweli kweli akamwambia sasa wewe ulitaka kujisaidia ukutani kwa watu!? Dereva anashangaa tu, ukuta uko wapi pale!? Yeye anaona vichaka tu na miti ya mbali mbali.

Yule mteja wake akajitambulisha kwa dereva akambia yeye ni mganga wa kienyeji na pale walipo ni Gamboshi, kama alikuwaga anapasikia basi ndio eneo walilopo. Yule mganga akampaka dawa machoni yule dereva akamuonesha ule mji ulivyo. Dereva anasimulia anasema hajawahi ona mji mzuri kama ule, si kwenye sinema wala picha. Ni mzuri hatari, na watu wana shughuli zao kama kawaida ila wako uchi na hakuna anaemshangaa mwenzie. Akamuonesha na ukuta aliotaka kuunyea akajiparua kalio. Yule mganga akazipaka tairi dawa zote zikakaa sawa, na ile ilofunguliwa akaiangalia ni nzima! Safari ikaendelea, alipofika kwa mganga akaoneshwa njia nyingine akarudi.
 
si movie hivi vitu vipo mie nina jirani ambaye wamezaliwa mapacha yaani pacha wake macho yake ni mabaya akiangalia kitu basi hakitoenda sawa mfano unapika utachochea wee lakini hakiivi hadi umwambie kishika tu basi mambo yana kuwa sawa


Sent from my iPhone using JamiiForums
Sasa huu ni uchawi au?

Maana Nimewah kuadithiwa kuhusu uncle yangu mmoja aliyefariki akiwa teenager.. Inasemekana kuwa alikuwa na uwezo wa kuokota chochote atakayoombwa na mtu asiyeweza kupata hicho kitu ila ile ni shida kweli sio kumchoresha. Watu walikuwa wanamtafuta wakipata shida wanamsimulia then ye anawapa pole wala hapangi chochote ila baada ya muda anapata ufumbuzi.

Binafsi nilichukulia kama story tu ila sasa hii ya kwako nikiunganisha na hii ndo nakosa majibu kuwa ni uchawi au laana/baraka anayozaliwa nayo?
 
Back
Top Bottom