Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Sio ya jogoo io kweli,anyway znaweza kua different ila same story.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuh lete Visa kadhaa vya kuverify hili
Kuna kipindi hapo hapo nilipopanga na yule mama wa kigoma, alikua ananitoa nje kimazingara na alikua ananitesa kweli

Basi siku moja nilala chakushangaza nikawa najiona nimetoka sijui wapi kule tena nilikua nimechoka sana nikawa naelekea kwenye chumba changu

Cha ajabu ile nakata kona nikamuona yule mama wa kiha kasima mlangoni tuanpoingilia akiwa amevaa nguo za kaniki(nyeusi) na kiremba cheusi theni akaninyooshea mkono huku anaongea maneno ya kichawi ghafla nikashitka

Ingawa badae nilipo lala nikajiona nipo ndani tena hata kuona vzuri siwezi nikiwa napapasa kitanda kilipo

Hiii inamaana gani
Yaani manaake yule mama alinichukua kimazingara usiku nakwenda kunibebesha magunia ya njegere alizokua anauza pale ilala.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 

🤣🤣🤣
 
nilipanga nyumba,chumba cha uani...sasa ikawa daily night Kali lazima mapaka yajae na kupiga kelele za kutosha juu ya bati...na mengine yanagonga dirishani..

kelele zikaendelea lakini nikishaamka na kuwasha UDI na kushtua Bob Marley, hayo makelele yanakata..na mbaya zaidi ni juu ya bati langu tu..

jirani yangu ticha nikimuuliza kuhusu hizo kelele anakataa hajawahi kuzisikia...na hata nilipomuuliza aliyeniachia chumba juu yaa mapaka,naye alikataa

ajabu nilipomuuliza baba mwenye nyumba juu ya makelele ya kutosha ya hao paka,naye alikataa kuwasikia.!

na kuanzia siku namuuliza hizo kelele zilikoma kabisaa..sijui alikuwa na uhusiano gani na hayo makelele ya mapaka.!!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uliposema na umri wako mdogo uliruhusiwa kuingia kwenye nyumba mganga nikajua kwamba hii ni chaiiiiii
 
Umenikumbusha uchawi wa unyakyusa miaka ya 2004 pale Tukuyu kwenye kiwanja cha mpira karibu na Stendi, kulikuwa na mkesha wa mwenge sisi tumeroka
Mfijinja dah!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Tukuyu kulikuwa na watalaamu kipindi cha nyuma pale uwanja wa mpira Tukuyu Mjini kulikuwa na mbio za mwenge.
Kabla ngoma za asili au ling'oma halijapigwa mvua ilianza kunyesha dakika chache wazee wa mila wakaitana na wakazuia mvua.

Siku ya ling'oma kulikuwa na uchawi haswa maana kulikuwa kama na ligi ya ngoma kutoka sehemu mbalimbali, nakumbuka kuna ling'oma kutoka Bujesi hawa walikuwa wakipiga ngoma Tukuyu inasimama.

Siku nyingine nilikutana na kisa cha kukutana na vibwengo mimi na jamaa yangu kwenye mashamba ya chai Kyimbila. Alinishawishi tufate ling'oma Ushirika kulikuwa na Mashindano ya ngoma. Wakati wa kwenda tukapanda Hiace "Big Poppa". Usiku ikawa kasheshe saa 3 hakuna gari tukaamua tutembee kufika mashamba ya chai tunaona kibwengo kinatembea upande wetu kila tukisogelea kinaongeza spidi. Gafla kikapotea tunafika maeneo ya Kamangila Bar kuna mzee tukamwambia akacheka na kusema nyie ni wageni.

Visa ni vingi huko Sakura Pangani usiku mkali tupo na pikipiki mara raia yupo njia panda ile kusogeza pikipiki hakuna kitu.

Njia ya Mpanda-Sumbawanga tupo na Isuzu Kb pick up kuna raia anagonga body kama ana amrisha gari isimame na gari iko mwendo kipindi hicho njia mbovu.
 
Pangani kulikuwa na mzee anaitwa Halichwi huyo alikuwa anaogopeka balaa, ilikuwa hakitaka jambo jua halikuchi hilo jambo linatokea.

Huyu alikuwa akiwa kwake jioni anatembea na majini yake kwenda kufata mahitaji.

Hapo Usagara Tanga mjini kuna mzee alikuwa mganga wa kitabu miaka ya nyuma kidogo kuna Kipindi alikuwa anayafungulia majini yanakuwa nje hapo karibu na kwake na njia hiyo ya Kwenda Coast Lodge.
 
Hii hata Kule Amboni Estate imewahi kutokea kulikuwa na mzungu kazoea Tanzania akawa ananyanyasa sana wabongo kwenye kampuni.

Wakampiga juju kila akienda Pangani anaumwa sana, akiwa Ulaya anakuwa vizuri.
Mzungu akaona isiwe tabu akaondoka mazima Tanzania.
 
Tanga miaka ya 82. Kuna jama alifanya mapenzi na mke wa mtu. Ghafla alipomaliza kitu kikakatikia ndani lkn damu haimwagiki. Alikuja kwa mganga pale Gatundu. Mtu mwingine ukimuangalia mashine unaiona imetulia. Yeye binafsi haioni na hata akipeleka mkono anakuta hamna kitu.
...........,..................

Jamaa mwingine tena alitembea na mke wa mtu. Wakamaliza fresh kila mtu akachukua hamsini zake. Jamaa alikua anakakaa nyumba isiyo na ceiling board. Ghafla wakati amepumzika chumbani kwake ametulia kitandani baada ya kumshuhhulikia mke wa bwege akaona panya amebeba dhakari na pum*** anakatiza nayo kwenye mbao juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…