Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Duh pole Sana Aiseee, sahiv lakini una watoto wengine?
 
Duh poleni sana jamani! Pengine angemuuliza huyo mzee vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha tu Mkuu najiuliza mpaka Leo sipati jibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah watu wabaya sana pole sana.

tatizo lugha
 
..Arusha..
Mimi nilikuwa nikiumwa nikienda shule tu na ilikuwa shule ya msingi..nikiruhusiwa kwenda nyumbani nakuwa mzima wa afya.Ikawa hivyohivyo..

Kuna kipindi ghafla uwezo wa kuona ukawa unapungua yaani nlikuwa nikiangalia mbele naona kama ukungu tu...ilikuwa balaaa.ila kuna mtu alinipa dawa ya majani .nikapona

Kuna siku niliumwa ..mpaka watu walijua nimekufa wakaanza kulia plus maandalizi ya kunizimisha macho nk.na hapo anae nizimisha macho ni bibi mmoja ambae alikuwa mchawi balaa.lakini MUNGU alikuwa mwema kwangu.nilizinduka ila jicho moja likawa limepata kengeza ..
Na mwanzo nilikuwa mzima kabisa nilikuwa na macho ya kawaida kabisa

Lakini tokea siku hiyo sijawahi kumwa tena na sasa ni mtu mzima na maisha yangu..
Na sijui sababu ya mm kuumwa ilikuwa nn
..uchawi upo tusali sana na kuomba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona zipo kila mahali? Kwa mfano nenda jukwa la wakubwa kule utaona live watu walivyotiwa giza kwa wanayojadili na kuyashabikia. Nguvu hixo xinatenda kazi hata sasa, ila wengi mnadhani ni tunguli tu.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Duuh hatari sana....
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Tanga hawafaiii mzeee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi sijawahi kutana na hayo mauzauza, na ninaomba MUNGU nisikutane nayo maana nitakufa hapo hapo. Ila kuna visa viwili nilihadithiwa na wazee wangu.
Cha kwanza ni baba yangu mzazi, wakati akiwa kijana barobaro alikuwa anapenda sana kutembea usiku. Alikuwa anaishi maeneo ya Tegeta. Siku moja wakati anarudi usiku akiwa anatembea akawa anasikia kama kuna mtu nyuma yake anamfuata ila akigeuka hamuoni, akakaza mpaka akafika magetoni. Akajiandaa kulala akafunga mlango na kuzima taa akapanda kitandani.
Wakati bado usingizi haujampitia vizuri akawa anahisi kama mtu anafungua mlango kwa nje anamchungulia, akapotezea akalala. Katikati ya usingizi akahisi kukabwa na mtu akiwa amelala, akajitahidi kujitetea lakini bado, akajaribu kupapasa akahisi ameshika jitu lenye manyoya mengi sana mikononi kama manyani yale. Hapo ndo akajua shit just got real. Akaamka akawasha taa hakulala mpaka asubuhi. Alikuja kusaidiwa na mzee mmoja hv alikuwa anakaa mwenge almaarufu kama Babu wa Mwenge marehemu. Akamwambia lilikuwa jini alikumbana nalo njiani. Lakini bado since then hakukoma kutembea usiku.


Cha pili ni mama yangu. Ni mchaga wa rombo, anakwambia zamani walipokuwa mabinti wadogo kulikuwa na majitu yanaitwa "Mangauneri" wajuzi mtanisaidia. Walikuwa kama binadamu tu wanakuja hadi nyumbani mnakula nao chakula cha usiku ila wanakijiji walikuwa wanayajua kwa hiyo wanamkaribisha tu akimaliza chakula anaaga anaondoka. Sasa baada ya hapo ni kuwasha moto mkubwa maana akiondoka anasikilizia mkishalala anakuja anachukua vijinga anawachoma navyo especially matakoni. Waliokuwa wanapasua mbao porini walikuwa wanakutana nao sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mara nyingi ukifuatilia mtu aliyekuchezea ni mtu wa karibu na familia yenu ambaye anajua uwezo wako wa akili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka ulikosea sana kumpa ushindi shetani na wachawi? Ulishajua ushindi upo kwenye maombi kwanini ulienda tena kwa waganga nyumbani? Damu ya mwanao itakulilia daima.maana hajafa amekiwa msukule labda.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana Mkuu,pole sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Itakuwa alienda kwenye jua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]daah usithubutu kukutwa
vijinga vya matakoni[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] em wachaga waje watupe muongozo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…