Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Tanga miaka ya 82. Kuna jama alifanya mapenzi na mke wa mtu. Ghafla alipomaliza kitu kikakatikia ndani lkn damu haimwagiki. Alikuja kwa mganga pale Gatundu. Mtu mwingine ukimuangalia mashine unaiona imetulia. Yeye binafsi haioni na hata akipeleka mkono anakuta hamna kitu.
...........,..................

Jamaa mwingine tena alitembea na mke wa mtu. Wakamaliza fresh kila mtu akachukua hamsini zake. Jamaa alikua anakakaa nyumba isiyo na ceiling board. Ghafla wakati amepumzika chumbani kwake ametulia kitandani baada ya kumshuhhulikia mke wa bwege akaona panya amebeba dhakari na pum*** anakatiza nayo kwenye mbao juu
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]unaweza kuzimia hv hv kudadeeki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikuwahi shuhudia live uchawi ila niliwahi shuhudia matukio mengi ya kichawi...

Miaka 2007 hadi 9 niliinshi nyumba moja magomeni mikumi karibu na bondeni kule kwa mzee mmoja wanamuita Fungo,

Nikiamka usiku wa manane naenda kukojoa naskia ngoma inachezwa sebuleni kwao waliishi nyumba kubwa mimi chumba cha nje na hiyo ilikua mara nyingi sana kuskia hata ikitokea nikishtuka usingizini naskia wakiimba, kupiga ngoma na kucheza.

Siku nkapanga safari kwenda kusalimia kijijini ikabidi nikubaliane na mzee alale chumbani kwangu maana kulikua na wezi sana miaka hiyo,

Baada ya wiki kurudi nkakuta kapeti limechanwa chanwa sanaaaaa na ni maeneo yale yanayokanyagwa tu, na vipande vimejazana huko chini kibao,
Hata sikuuliza kwa mazingira niliyoyaona nkajua tu ngoma ilihamia gheto kwangu na watakua wanavaa viatu vyenye ncha kali ndio maana wakalichana vile..

Lakini cha ajabu matukio yote hayo sikuwahi kua na hofu hata chembe hata sijui kwanini...

Kuna nyumba tulipanga maeneo ya sinza mapambano, mara nyingi tu mke wangu huona watu wako uchi aidha nje wakichungilia dirishani na wengine wapo chumbani kwetu, na hapo yule macho live, lakini hata anaponiadidhia wala sipati hofu yoyote, hua naona kawaida tu, sijui ni kwanini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kijiji kimoja mkoa X, mzee mmoja alipowaona kuku wa jirani wanashambulia mahindi shambani mwake akaamua kuwatimua kwa kuwapiga na mawe.
Alipoamka asubuhi akajikuta mguu mmoja umetoka uko pembeni hakuna damu wala nini, akiwa katika taharuki nini afanye akalala tena kuamka kesho yake mguu wa pili pia umetoka uko pembeni.
Mpaka leo huyo jamaa yuko na ameshakuwa mzee haelewi nini kilimkuta anatumia wheel chair, uchawi upo.

Kweli duniani watu wana roho mbaya sana! Unamnyang’anya mtu miguu yake yote ati kwa vile amefukuza kuku wako shambani kwake? Huyo jamaa mwenye kuku ni “mshamba” sana
 
Wacha na Mimi niwape mkasa niliyoshuhudia katika mahakama moja miongoni mwa wilaya za Tanga.
Nikiwa katika harakati za kutekeleza majukumu ya kikazi nilipanga nyumba moja hivi iko vizuri tu.wapangaji tulikuwa watatu tu, baba mwenye nyumba Ni kijana mwenzetu ana mishe zake. Sasa bhana huyu baba mwenye nyumba kwenye biashara zake akafanya magumashi yaliyompelekea kushatakiwa na kufunguliwa kesi mahakamani. Kesi ilikuwa kubwa ya kumfunga kifungo kirefu tu. Kwa kuwa huyu baba mwenye nyumba tulikuwa tukielewana stori kwa Sana akanambia nimsindikize mahali kwa mganga. Tukaenda aisee tulipofika mganga akatueleza shida tuliyoendea kesi jinsi ilivyo na imebaki shahidi tu kuja kutoa ushahidi siku ya kesi jamaa ahukumiwe kwa namna yoyote jamaa hachomoki. Mganga akasema kanileteeni Nazi moja tu na si kitu kingine duh tukasema hapa hamna mganga. Tukaenda nunua Nazi tukampelekea, mganga akaandika maneno ya kiarabu kwenye ile Nazi kwa juu ikiwa haijapasuliwa ( maandishi yalikuwa ya rangi nyekundu). Kisha akasema saa 8 usiku ile Nazi ikapasuliwe njia panda ya kuelekea mahakamani.
Tuliporudi home tukawa tunasema mganga mzinguwaji kesi kubwa yy anatufanyia mzaha, basi saa nane usiku tukaenda njia panda ya kuelekea mahakamani jamaa jamaa akajifunga kaniki nyeusi Kisha akaipasua kama alivyoelekeza mganga.
Siku ya kesi ikafika ndipo nilipojuwa kuwa dunia no Zaidi ya tunavyoiona. Jamaa kafikishwa kizimbani kasomewa mashtaka kakataa akaitwa shahidi wa Kwanza, hakimu Kila swali akimuuliza shahidi anasema kasahau hakumbuki kitu, shahidi wa pili ndiye was muhimu Sana aisee jamaa alivyopanda kutoa ushahidi alikuwa bubu seriousky kudadeki acheni tu Kila akiulizwa anashindwa kuongea anabaki baaaa...baaaa...mmmm. Hakimu alidata akaahurisha kesi.
Siku tajwa ya kesi kufika hakuna shihidi alokuja Tena na Tena. Hakimu akafuta kesi na jamaa akawa huru.
Hivi vitu vipo aisee Ni mpaka ushuhudie ndiyo utaamini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Muda si mrefu nitakuwa na afro kama avatar yako.
 
Gamboshi ipo kweli usukuman huko ila hizo story zake za kichawi zimetiwa chumvi. Nimesoma na jamaa mmoja mpwapw secondary form four 2004, Emmanuel Holehole alikua katokea Gamboshi. Alinambia Gamboshi kwa kawaida tu hakuna lolote Kama wanavyosema.
Gamboshi Ni ukweli au simulizi za kusadkika mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh, mimi nimeshuhudia uchawi wa kutisha kwenye nchi moja inaitwa Tanzania.
Kuna li Chama inaitwa CCM, tangu mwaka 1961 hadi leo 2029 watu wanalala kwenye nyumba Kama mabanda ya nguruwe na kula yao ni taabu lakini wanavumilia tu badala ya kutumia nguvu kuyatoa ma CCM, ama kweli uchawi upo

Sent using Jamii Forums mobile app

Watu wanaendelea kuweweseka na kushika watu uchawi badala ya kutunga sera mbadala...
 
Jirani yangu kuna siku alikuwa ananisimulia alikuwa anasafiri na broo wake usiku walikuwa kwenye gari yao. Safari ilivyokuwa inachanganya mbele wakamuona mtu kwa mbali kama anasimamisha gari. Kumuangalia vizuri kumbe ni mwanamke, halafu ni mrembo tu! Dogo akamwambia bro huyu mwanamke atakuwa jini tu haiwezekani usiku huu wote asimame njiani peke yake, tumpite tu.

Brother yake akamwambia usihofu. Akasimamisha gari. Akamwambie ndio mrembo! Yule mwanamke akamwambia naombeni lift nimekwama huu usiku naelekea eneo fulani. Brother yake akamwambia yule mwanamke ingia. Safari inachanja mbuga brother yake akaanza kumwambia yule mwanamke. Inakuaje unatusumbua unasimamisha gari wakati eneo unalotaka kwenda unaouwezo wa kufika?

Yule mwanamke akajibu sielewi unachozungumza. Brother yake akamwambia yule mwanamke, usi' panic! Sisi tuliokupa lift tunajua kwamba wewe ni jini! Ndiyo tunakuuliza kwa nini umetusumbua kusimamisha gari wakati kufika eneo unalotaka uwezo huo unao wewe kama wewe?

Yule mwanamke akawaambia simamisheni gari! Majamaa wakasimamisha. Wakasikia mlango wa siti ya nyuma unafunguliwa. Kugeuka yule mwanamke hawamuoni tena! Brother yake akasema, unatusumbua wakati uwezo wa kufika unao. Wakaendelea na safari.

Nikamuuliza sa mbona huyo jini katumia style ya zamani sana? Jamaa akanijibu, majini ni wapumbavu wapumbavu tu.
 
Jirani yangu kuna siku alikuwa ananisimulia alikuwa anasafiri na broo wake usiku walikuwa kwenye gari yao. Safari ilivyokuwa inachanganya mbele wakamuona mtu kwa mbali kama anasimamisha gari. Kumuangalia vizuri kumbe ni mwanamke, halafu ni mrembo tu! Dogo akamwambia bro huyu mwanamke atakuwa jini tu haiwezekani usiku huu wote asimame njiani peke yake, tumpite tu.

Brother yake akamwambia usihofu. Akasimamisha gari. Akamwambie ndio mrembo! Yule mwanamke akamwambia naombeni lift nimekwama huu usiku naelekea eneo fulani. Brother yake akamwambia yule mwanamke ingia. Safari inachanja mbuga brother yake akaanza kumwambia yule mwanamke. Inakuaje unatusumbua unasimamisha gari wakati eneo unalotaka kwenda unaouwezo wa kufika?

Yule mwanamke akajibu sielewi unachozungumza. Brother yake akamwambia yule mwanamke, usi' panic! Sisi tuliokupa lift tunajua kwamba wewe ni jini! Ndiyo tunakuuliza kwa nini umetusumbua kusimamisha gari wakati kufika eneo unalotaka uwezo huo unao wewe kama wewe?

Yule mwanamke akawaambia simamisheni gari! Majamaa wakasimamisha. Wakasikia mlango wa siti ya nyuma unafunguliwa. Kugeuka yule mwanamke hawamuoni tena! Brother yake akasema, unatusumbua wakati uwezo wa kufika unao. Wakaendelea na safari.

Nikamuuliza sa mbona huyo jini katumia style ya zamani sana? Jamaa akanijibu, majini ni wapumbavu wapumbavu tu.
[emoji2]jini kaleta uduwanzi akakutana na binadamu mduwanzi vilevile!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiboko ya wote nendeni GAMBOSH simiyu.ni kakijiji kadogo lakini ikifika usiku taa za umeme magari utafikiri upo dubai panawaka panachangamka ikifika asubuhi utashangaa nyumba moja moja za majani

Sent using Jamii Forums mobile app
Huko ndio kuliko wapatia idea Marvel wakatengeneza black panther.
Gambosh=Wakanda. [just saying]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu Uzi unatembea fasta utazidi ule wa Wala epo kimasihara

Binadamu wanakuwa ‘fascinated’ na ‘mystery’ au miujiza. Suala ambalo akili ya kawaida ya binadamu inashindwa kupata jibu lake humfanya apate dukuduku la kupata ufumbuzi wake. Kwa sababu hiyo mjadala huu utakuwa mrefu sana. Tunaomba wadau waendelee kutuletea vimbwanga zaidi vya ukweli. Ingawa inawezekana wengine wataleta ‘fix’ tu za kusimuliwa ambazo hazijathibitishwa.
 
Nishawahi sikia kisa kinschohusishwa na uchawi

Kuna masela wawili walienda kwa mganga ili wapate utajiri

Mganga akawapa dawa akawaambia wakaoge usiku makaburini na wakitoka mlangoni kwa mganga hawatakiwi kugeuka nyuma

Basi unaambiwa safari yao iliandamwa na misukosuko yakutisha, mara wasikie muungurumo wa simba akiwa nyuma yao na vimbwenga vingi lakini walijitahidi kukaza ili kutovunja sharti la kugeuka nyuma

Sasa ulipofika usiku majira ya saa 8 ikabidi waende makaburini kuoga ili kumalizia zoezi lao la mwisho ili wawe mamilionea

Walipofika makaburini wakavua nguo wote nakubakia uchi kisha wakapanda juu ya kaburi ili waoge

si unajua ukiwa katika ile mood flani hivi unaoga halafu umefumba na macho ili maji yasiingie machoni.

wakastukia tu paap! wameshikwa makalio kwa nyuma.

Aaah unaambiwa wote ilibidi wageuke nyuma kwa haraka huku wanakimbia na kupiga makelele

Kesho yake kijiweni wakaanza kulaumiana "aaah wewe ndiye ulizingua, we ungekausha bila kupiga mikelele mi nisingechochora kwani kushikwa tako kitu gani bwana" yani leo nisingekua nakunywa kahawa hapa ningekua nimejikoki huko kwenye hotel zinazotambulika na dunia"
 
Kweli duniani watu wana roho mbaya sana! Unamnyang’anya mtu miguu yake yote ati kwa vile amefukuza kuku wako shambani kwake? Huyo jamaa mwenye kuku ni “mshamba” sana
Ndo tabia za wachawi, wachawi hawapati faida yoyote wao wanataka kuona mtu anateseka tu ndo furaha yao. Hicho kisa ni cha kweli na kimetokea Ludewa mkoa wa Njombe ukiweza ulizia wenyeji wa huko watakuambia na jamaa amekuwa tegemezi wa kupewa misaada tu, miaka ya nyuma 2000's hiki kisa kiliandikwa kwenye gazeti fulani, it's a true story.
 
Back
Top Bottom