Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kubababake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimecheka mpk Bia imenipalia!
Huyo jini alikuwa bado mwanafunzi
 
kwa kweli story hii, inanihitaji kumtafta mwalimu wangu wa fasihi aliyenifafanulia liwaya ya "joka la mdimu" mpaka nikaelewa, aje anifafanulie na tungo za liwaya hii..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daaa nimecheka broo kauzu huyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimecheka mpk Bia imenipalia!
Huyo jini alikuwa bado mwanafunzi
Haha! Huyo jamaa huwa ananiacha hoi sana! Kuna siku kuna mwanamke alipandisha majini bhana! Wakaja viongozi wa dini kufanya kisomo. Si tulikuwa pembeni tunaangalia picha jinsi linavyokwenda. Yule jini akaanza huyu mwanamke nampenda siwezi kumuacha!

Huyo mshikaji si akanyanyuka bhana akamsogelea huyo mwanamke aliyepandisha majini. Jamaa akaanza; Nyie majini washenzi sana! Kwenu hamna mademu! Unampenda unampenda nani rudi kwenu huko!
 
Msalimie mkeo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiki kisa kilinitokea mimi mwenyewe miaka ya 80, kati ya 86/87. Sikumbuki mwaka sahihi sababu ya umri mdogo niliokuwa nao, ila nilikua najitambua. Tukio hilo lilitokea sehemu ambayo baadaye nilikuja kujua kuwa inaitwa makuburi jijini Dar, baada ya kuwauliza wazee nikiwa na umri wa kutosha kwenye miaka ya 90. Maana ni tukio ambalo hadi leo huwa tunataniana sana tukikutana familia nzima. Nakumbuka ilikuwa kipindi hicho Mzee alikuja Dar kwa ajili ya kusoma UDSM baada ya kuamua kujiendeleza. Sasa akaona ili asome vizuri, ni vema awe pamoja na familia yake. Kwahiyo baada ya kumaliza taratibu za kujisajili chuoni, akaamua kutafuta nyumba. Ndio akapata nyumba nzima huko makuburi. Basi akafuata familia yake, mama, mimi na dada yangu. Basi tukafika jijini Dar, na kuanza maisha mapya. Lakini hatukuchukua raundi, ndani ya mwezi mmoja tu. Ndio likatokea tukio hilo. Siku hiyo ilikuwa ni usiku mnene, sikumbuki ilikuwa ni wa saa ngapi. Ila nilikuwa sijapata usingizi bado. Hata dada angu alikuwa hajalala. Maana tulikuwa tunalala kitanda kimoja(mzungu wa nne). Pia tulikuwa tunalala na binti wa nyumba ya jirani, alimuomba bimkubwa ili atupe kampani maana tulikiwa wadogo kuliko yeye. Pia ni mwenyeji. Mimi kidume niko upande wangu kimya, nasubiria usingizi wakati wao wanapiga tu stori. Hapo tumeshazima taa yetu ya chemli. Nimekaaaa....mara ghafla nikashtuka naona mtu mweupe amesimama pembeni ya kitanda tena usawa wangu!! Nikashtuka, ila sikufanya chochote. Nikawa namtazama tu. Baadae nikamuona anaanza kutembea kukizunguka kitanda. Kapiga raundi moja kisha akakaa juu ya kingo za kitanda upande walikoweka vichwa dada na mwenzie. Mi namuangalia tu! Akapiga raundi ya pili, akakaa tena palepale! Ikabidi nimshtue sista,(nikamwita jina lake) mtu huyo!! Wakashtuka...wakaangaliaa...hawajaona kitu. Akanimaindi"hebu lala huko...usitusumbue!" Mmmh...nikaona hili balaa! Yaan mtu huyu hapa halafu wanasema hawamuoni! Itakuwaje?! Ikabidi nitulie tu...akapiga raundi ya tatu halafu akaja usawa wangu akiwa ukutani akasimama! Nikabaki nashangaa, kitanda kimegota hadi ukutani, huyu anawezaje kutembea bila shida?! Wakati najiuliza nikashangaa kuona ananisogezea mkono wake!! Akisogeza, na mimi nasogea kimyakimya... hadi nikafikia kwenye ukingo wa kitanda, yaani kinachofuata ni kudondoka!! Ujasiri ukanishinda, ikabidi nipige yowee...""baba mtuuuuu!!!" Hapo niko chini tayari!! Sista na mwenzie walivyoskia hivyo ikawa vurugu mechi, na lile giza. Ilikuwa ni mwendo wa kuparamiana tu!!!Dingilai alikurupuka geto kwake na taulo huku kashika panga huku bimkubwa akiwa nyuma yake! Kufika pale kuwasha chemli, akapekuwa hadi uvunguni. Wakaambulia chenga tu, nikawasimulia ilivyokuwa. Ingawa sista nae alidai walivyokurupuka walimuona kabla hajatoeka ingawa simuamini sana. Tangu siku hiyo wote tukawa tunalala chumba kimoja. Na yule binti akakataa kuja kulala. Wiki hiyo hiyo tukarudishwa kwa bibi, dingi akarudi hostel za chuo.
Na kisa kingine nilikutana nacho mwaka ya 2008, ingawa hakikunilenga mimi ila kiliashiria ulozi moja kwa moja. Mimi huwa nilikuwa na tabia ya kupenda kurudi usiku sana nyumbani. Utakuta nakaa home kuanzia asubuh, nafanya shughuli zote. Ila ikifika saa 10 jioni, ndio natoka. Na kurudi ni kuanzia saa 3 hadi 6. Sasa siku hiyo narudi zangu, mida ya saa 4 usiku. Njia ya mkato ina makaburi, naogopa. Njia ndefu kuna kakichaka karefu, kanatisha! Ila huwa napita bila shida. Ila siku hiyo nikajikuta tu naingiwa hofu! Ikabidi nipige moyo konde, maana lazima nirudi home. Basi nikatembea kwa kasi balaa, nikapanga nikikaribia karibu na hicho kichaka nipite kwa kasi ya upepo!! Basi nakaendaaa, nilipokaribia kichaka nywele na mwili vyote vikasisimka. Nikasema leo kazi ipo, nikajikoki...nikatoka nduki la hatari na nakimbia(huwa napenda). Kufika katika ya hicho kichaka nikakuta bonge la kinu limefunikwa!! Hiyo breki na kona niliyokata, Mungu tu ndiyo anajua. Na kipindi hicho nilikuwa niko vizuri kwa mazoezi. Sikugeuka nyuma hadi nyumbani. Niliwaza sana, karibu wiki nzima. Hizi ningekigonga na kubinuka ingekuwaje?! Baada ya mwezi nilimsimulia bimkubwa, alinisema sana! Nikapunguza kutembea usiku. Saa mbili niko home.
 
Pole sana mkuu
 
Nimecheka Kwa nguvu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…