Kisa cha kwanza ambacho kinanivutia hadi leo ilikua mwaka 1998, Niko na jamaa yangu, Tunatokea Shule ya Wasichana Kifungilo tunarudi shuleni kwetu Magamba Secondary (now Sebastian Kolowa University)! Usafiri miaka ile usafiri ulikua wa shida sana, tukawa tunasubiri usafiri pale Lukozi, SAA Tisa au kumi hivi jioni. Mvua ikaanza kunyesha, wenyeji wakasema kuwa Mvua haitanyesha kwa kuwa Mzee Fulani yuko shambani kwake anauza mapeasi yake.
Ghafla yule Mzee akawa anapita, aiseee seriously kwa Mara ya kwanza tangu nizaliwe sijawahi kuona MTU hanyeshewi na mvua! Yaani mvua inanyesha lakini yeye hanyeshewi kabisa
Sent using
Jamii Forums mobile app
Mkuu utakua umechanganya majina ya kituo kdg sbb majina km yanaendana..
Kituo kitakua ni mkuzi.
Nimeishi kule kiasi maana mzee alikua meneja misitu pale magamba forest(hope unapajua ni katikati ya msitu, kambi ipo isolated na wanakijiji, japo huduma zote zipo) kabla hajahamishwa..
Lukozi ni Juu ya Magamba km unaenda Mtae huko na kifungiro n km unaenda mlola..
kwahio, unatoka kifungiro unaingia mkuzi, unakuja magamba coast, unaingia trade unakuja magamba sec(secomu) ndio unaelekea huko lukozi...
Na huko kuelekea Lukozi ndio kuna msitu unaitwa 'kandele ka paa' huko ndio kuna mapicha sio ya nchi hii, waulize waendesha magarii...
Na ukitokea huko mkuzi...
kimbembe kipo pale kati ya msitu kwenye daraja flan kubwa, maji yanayopita ni mengi ila yanashuka taratbu, kila upande ni giza kubwa si barabarani sio msituni maana maeneo hayo ndio msitu umefura kisawa sawa na miti ni mikubwa mirefuuu kwaio hata mwanga wa jua haupenyi...
Kwaio pana sifa ya Ukimya, giza kubwa, msitu mnene, Daraja kubwa lenye maji mengi,
You can imagine....
pale Hata walevi wakipita wanaacha kelele kwanza.. ndio utajua Pombe inaogopa nayo..
Maji yenyewe hayapigi kelele wala ndege wa polini wewe upge kelele ni nani?....
Pametokea matukio mengi sanaaa.....
Yote kwa yotee yale maeneo yana mapicha picha sanaaaa...
Huko huko mkuzi kuna mzungu mmoja maarufu sana naamini hata wewe unamfahamu, alikua anaitwa mzuka,
Kisa cha kupewa hili jina ni kwamba alikua na shamba akaambiwa popote utakapoona huu mti usiukate ni makazi ya majini/shetani..
Akapuuza siku akaukata...
Alikula bonge ya banzi, kuanzia pale akawa amepinda shingo, kichwa kimelalia upande mmoja...
Maisha yake yote yaliobaki alikua akitembea na kikapu kilichojaa mawe upande mmoja ili ku balance mwili maana ulikua umelala upande mmoja...
Pia tushawahi pita sehemu usiku miti ikalala yoteee.....
Pia mzee alishawahi salimiwa na vibwengo usiku akitoka magamba coast akipita ule uchocholo wa magamba sec...
Akavitukana sana huku anachomoka kasi ya ajabuu..
alifika nyumbn hana kiatu kimoja.....
Kuna mapicha mengi sanaa kulee....
Yale maeneo yote yalikua makazi ya wajerumanii,
nyumba nyingi km ya mkapa, ngwirizi na majumba mengi sana yamejaa...
Hata sisi kambi yetu ilijengwa na mjerumanii,
Majumba yao yamedizainiwa kiajabu sanaa....
Tumeish kwenye nyumba miaka na miakaaa,
eti tunakaribia kuhama ndio tunajua tunaishi juu..
kumbe chini kuna nyumb nyingne yenye mavyumba na hapo barazani chini kumbe ni bonge ya kisima..
Ilikua ukizunguka msituni kukuta sehemu imesakafiwa au makorokocho korokocho mengi ni kitu cha kawaidaaa..
Nimepamisss long time sanaaaa..