bablon6
JF-Expert Member
- Jan 26, 2018
- 630
- 566
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]mbwa ni snitch alienda kupeleleza
Sent using Jamii Forums mobile app
kuna tukio lilitokea mkoa wa Rukwa wilaya na kijiji X.
watu wa kijiji hicho huwa jumapili wanapumzika kazi za shamba wanaenda kanisani kwani kijiji na mashamba yalipo kuna umbali na watu wengine wanalala huko huko kuna nyumba za muda ila jumapili wote wanakuwa kijijini.
basi kuna mama mmoja siku ya jumapili alikuwa anaenda shamba kuchuma mboga za majani, ili ufike shambani kuna msitu unapita. Wakati anakaribia kufika ule msitu akapishana na mbwa akiwa kasi anaelekea njia ya kijijini lakini yeye hakumjali kwani mbwa si kitu cha ajabu kwa kijijini.
akiwa anaendelea na safari yake katikati ya msitu akamuona mtu amekaa kwenye gogo akamsalimia na kuendelea na safari yake, kapiga hatua tatu akasikia yule mtu anamuita jina lake akageuka ili amuaangilie vizuri lakini kila akimuangalia yule mtu sura yake ikawa haileweki kama vile mtu anayejitazama kwenye kioo chenye ukungu.
yule mtu akaanza kumuuliza maswali yule mama:
mtu: huku akimtaja jina, unaenda wap?
mama:shambani.
mtu: kufanya nini?
mama: kutafuta mboga za majani.
mtu: wale samaki aliokuletea D kwa nini hujapika wale.
yule mama alishangaa jinsi alivyomuelezea mambo ya nyumbani kwake lakini akataka kumpuuza ili na safari lakini yule mtu alimwita tena safari hii kwa ukali, yule mama alipogeuka akashangaa baada ya kumuona yule mtu kawa wa ajabu zaidi kuliko mwanzo kwani sasa hata miguu yake utafikiri ni mtu anayeelea angani na sura isiyoeleweka kama ni mwanamke au mwanaume.
yule mtu akamuamuru yule mama kurudi alikotoka haraka huku akimwambia kwamba una bahati sana Leo. yule mama kwa hofu huku akitetemeka akaanza kukimbia kurudi kijijini kufika mwanzo wa msitu akapishana tena na yule mbwa akiwa kasi anarudi msituni.
Sent using Jamii Forums mobile app