Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kwanza nianze kwa kuwaomba radhi kwa maelezo marefu ya huu mkasa

Niliandika mara yakwanza sijui nni kikatokea simu ikawa imehome njee kabisa ya aplication cjui nini kilisababisha

Basi bandugu acha namimi niendelee kutoa mikasa ambayo nimekumbana nayo hiii ni post ya 3 nadhani

Nakumbuka kuna nyumaba niliwahi kupanga maeneo ya kigogo jijini Dar, asa wakati naishi pale nikawa nakumbwa na mambo mengi sana ikiwemo mikosi ya hapa na pale homa zisizo na kichwa wala miguu yaani kwakifupi mpaka afya yangu ukazota.

Siku moja alikuja rafiki yangu mmoja hivi kisha nikamueleza matatizo yanayonikumba jamaa akaishia kunipa pole tuu

Basi yule jamaa akaniambia leo nataka kulala hapa gheto kwako kwani cna nauli nikasema poa hatimae giza liliingia ilipofika mida ya saa2 yule yule jamaa alitangulia kulala basi mi nikawa naangalia Tv kwa bimkubwa

Hatimae nilirudi majira ya saa 5 usiku nikamkuta yule jamaa yupo macho ile cjakaa sawa yule jamaa akaniambia kaa chini nikueleze kilichotokea, akaniambia ebhana huyu baba ambae ni ostazi nimemuona anaingia humu ndani yeye na mwanae wa kiume tena waliingilia hapo kwenye kona ila kwakua nimewaona kwenye usingizi niliwatukana kisha wakapotea

Jamaa akaniambia hata hayo matatizo uliyonieleza nahisi nihuyu anaku7bishia aisee ckuamini
Ostazi ambaye kila ikifika jion anaswalisha watoto wake, yaani me nasema hakuna atakae iona pepo mwisho wa Dunia
Basi tulilala me najamaa ingawa yule ostaz hakua na maelewano mazuri na jamaa yangu kwani hata salam akawa anaipokea kinyonge sana kitendo kilichopelekea yule jamaa kukata kabisa kuja pale
Siku zilienda huku nikindelea kuteswa ikifika usiku, na mimi uwezo wa kuhama nikAwa sina kwani mlipa kodi alikua nibimkubwa basi nikaendelea kukomaa palepale

Cku moja nakumbuaka nilikua naangalia Tv ndipo nikamuona jamaa mmoja anaelezea dawa ya mkunazi jinsi ilivyo na uwezo na ktk maelezo yake alisema inauwezo wa kuzuia nguvu za giza na kuondoa mikosi ya hapa na pale

Ikabidi nimvutie waya nijue anauzaje na anapatikana wapi akanipa maelekezo theni nikamuibukia alikua anakaa maeneo ya mbagara kwa Azizi Alli

Hatimae nilifanikiwa kununua ile Dawa nilipo rudi nyumbani nilifuata maelekezo kama alivyoniambia,

Basi nilichanganya kwenye maji ile dawa nyingine nikawa nakunywa nyingine naogea kuondoa mikosi nikachukua nyingine nikamwaga kwenye kona kona mle chumbani kwangu

Hatimae giza liliingia nakumbuka siku hiyo nilala mapema tuu kwani nilikuwa najickia vbaya , asa ilipofika mishale ya saa 7 nikashtuka nikaona mlangoni kunamwanga mkali uliombatana na kishindo nilivyozidi kuamka nikawa naona mtu anakimbia kuelekea Chooni huku kakishikilia kile kifaa kilichokua kinang'aa
Basi baada ya muda fulani nikasikia anarudi kutoka kule chooni na round hii hakua na kile kitu, akafka mpaka pale mlangoni akasimama asa me nikasonya manaake nasikia mchawi na sonyo ni vitu viwili tofauti, aisee alikimbia mpaka ndani kwake

Kumbuka hiyo inaelekea saa8, basi nikatoka nje moja kwa moja nikaelekea chumba cha ndg wa yule ostaz mchawi nkabisha hodi theni jamaa akafungua

Nikamuhadisia, akasema hivyo vitu vpo na sikwamba havipo vipo sana na namjua anae fanya hivi, pia jamaa akaniambia yeye mwenyewe kuna kipindi ilikuwa ikifika jioni kuna kiumbe kinakuja juu ya paa lake na kinaanza kufagia mara michanga inamwagwa juu ya paa lake

Jamaa mwishowe akanishuri niende kwa mama yao ambae anishi kinondoni nikamsemee kwa vtendo anavyonifanyia ila mimi nimamwambia acha tuu kwani nimapito Ya Dunia

Basi yule jamaa akaniamabia nenda kalale kwani usiku ulikua mwingi mnoo nakumbuka ilikua saa9 nikafanya hivyo

Kumbe yale mazungumzo mimi na mdogo wake yule ostazi mchawi aliyasikia hivyo akafanya kila njia akatufarakanisha, siyo siri hali ikawa tofauti kwa jamaa kwa jinsi nilivyo mzoea, mara nikawa nikimueleza kitu yule jamaa anashout tena unakuta ananiambia chukulia kawaida hayo mambo ikaenda yule jamaa kanigeuzia mimi kibao nikawa naonekana mimi ndiyo mchawi pale mtaani

Hali ilienda hivyo hatimaye hata yale madawa niliyoweka kama zindiko akaharibu yakawa hayana nguvu tena hivyo akawa ananitesa balaaa

Akawa anafanya juu chini ili aniue kwani nilishajua siri zake hiyo hali iliendelea mara nikawa naota mindoto ya ajabu ajabu

Bimkubwa naye nikawa namwambia lakini akawa ananiambia yeye hana hela ya kunipa ili nihame kwani biashara zake zilikua haziendi vzuri
Siyo siri wachawi wanaroho za kikatili sana hawana huruma na ukiwa hauna kinga wanakuonea sana..........


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka mingi nyuma wakati nipo kanda ya ziwa. Timu yetu ya mtaa ilifanikiwa kuingia nusu fainali ya kombe la wilaya. Kutokana na kuwahofia wapinzani wetu, tukashauriana twende kwa mganga. Tulipofika nakumuelezea shida zetu, akatwambia kamateni yule kuku pale (kulikuwa na kuku wanakula kula pale nje kwa mganga).

Tulikamata kuku jike, mwenye madoa doa kama kanga. Mganga akaongea maneno yake pale, alaf akamchinja. Yule kuku hakutoa damu hata kidogo, mganga akashtuka. Alivyompasua ndani akakuta vitu vyote kuanzia figo, maini, moyo, utumbo n.k vimeoza. Palepale mganga akatwambia nendeni tu mkakamilishe ratiba vijana wangu wenzenu wameshawawahi.

Ile mechi tulipigwa 5-1.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh
 
Mkuu kwn bi mkubwa kuna jambo lolote ulimkosea mpk akwambie kuwa amekusamehe??

Then kile kisa cha lile dubwana lililotengenezwa na mganga kiliishaje, au mlilishinda vp lile jini?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Njoo Buza nikupe chumba cha uhani utakaa miezi 6 bure

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]dah
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiranga, Nakuuliza,Ulishawahi kufanya tafiti yoyote kuhusiana na existing ya uchawi?

Sent using Jamii Forums mobile app


Hii ya kua macho halafu naona nanyuliliwa juu kwa kuvutwa na kitu kisichoonekana imeshanitokea mara mbili sitakaa nisahau, uwa ninasali sala zote mkuu
 
Hii ya kua macho halafu naona nanyuliliwa juu kwa kuvutwa na kitu kisichoonekana imeshanitokea mara mbili sitakaa nisahau, uwa ninasali sala zote mkuu
Mara nyingi Ni michezo ya wanga kukusumbua kusumbua tu.
Ila Kama una roho ngumu ikiwa wanakusumbua sumbua unaweka tego wakinasa wewe huiti majirani unawaingiza ndani,unachukua KY unafukua tope kwisha kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…