Saint anne Ushawahi kuona moto unawaka kitandani na hakuna alieuwasha? ? Na kitanda hakijaungua? ? Kitanda kinatikisika hakuna alietikisa earthquake ikasome Ushawahi ona? ? Ile umekaa na Kachanga kitandani mara vuup unaona kama shoti imepiga kitandani mara tatu. Paaaa moto unawaka unazima unawaka unazima na kitanda chumba chote kama tsunami inapiga Umewahi ona????!!
It happened nyumbani kwangu ...
Ilikua hivi. .
Kachanga kalipozaliwa tu ndipo kasheshe likipoanzia. Baada ya kujifungua tu dogo usiku alikua anaota kama ndoto ambazo kumbe hazikuwa ndoto bali ni uhalisia alikua anaota kama kuna mtu anakuja usiku anakua anamziba pua hivi na kumfanyia vitu ambayo wakati huo yeye anaona kabisa kama anafanyiwa ila akitaka kupiga kelele kuomba msaada hakuna anayemsikia yani sauti haitoki. .taka kupiga kelele za msaada wapi. .hata akitaka kumwita anaelala nae chumba kimoja hawezi.
Akiamka asubuhi ananihadithia kuwa dada tangu nilipojifungua usiku usiku natokewa nahivi na vile. .Mi nikawa namwambia kuna nguvu za giza zinakufatilia. .inaonekana zilikutafuta sana tangu ukiwa mjamzito lakini hazikufanikiwa stil zinakufatilia. Sali sana dogo dunia ina mambo mengi. (Nina imani kali sana mimi yani moyo wangu ukikataa kitu lazima kinakua hovyo au cha majanga yani ninachodoubt mara nyingi huwa hivo hivo kama nilivohisi )
Ikaendaa Ikaendaaa muvi yenyewe ilikua siku mtoto ametimiza mwezi mmoja kamili yani the same tarehe amezaliwa mwezi uliopita wakuuuuu. .omba yasikukute kumbe Tarehe 15 kuamkia 16 ndipo wifi mtu( mkuu wa wachawi na team yake walikuja kumchukua mtoto na hapo nyuma housegal alikua ameshampa dawa mtoto nyingine alishamnywesha na kuwafanyia vitu kadhaa kwa kulazimishwa nahuyo wifimtu . Walijuanaje mimi mwenyewe nilishangaa sana.)Kwani baada ya wiki kadhaa ndiye aliyekua anawahudumia mama na mtoto
Mtoto alizaliwa tarehe 16 sasa Ile tarehe 15 usiku wakati tumelala dogo aliona kama kuna mtu ambae alikua ni mdada alikuja na kuwa kama anachukua mkono wa dogo ( mamamtu) na kuupeleka shingoni kwa Kachanga dizain kama anamlazimisha mamamtu amkabe mtoto..dogo akawa anatoa mkono ile ya kukataa huyo dada anamlazimisha kumkaba mtoto dogo anagoma vutana vutana dogo anaishiwa nguvu badae akashtuka na kumuangalia mwanae mtoto alikua analia sanaaaaaaaa. . Akasali na kulala asubuhi akaja kuniambia tena dada usiku nimetokewa na hivi. .
Ile kunisimulia nami nikakumbuka usiku huo huo wa tarehe 15 kuamkia 16 niliota ndoto kuwa mtoto( Kachanga ) gafla amepotea kwenye mazingira ya kutatanisha na mama yake yupo ukweni ila amekondaaaaa ngozi imekua kama mzee. .Hapo ukweni ndugu zake tumeenda kumuona ndugu yetu ila tunaona wanapitisha sahani zenye mapaja ya nyama za watu yaliyochomwa paja jekunduuuuu mara mikono ya watu lakini kama nyama ambazo watu wanakula. The same night kuna dada yetu mwingine yeye aliota mtoto wa dogo amefariki ila anaonekana yupo dirishani kwenye chumba fulani.
Niliposikia hayo ya dogo nikaunganisha ile ndoto yangu nilishtuka sana nikamwambia dogo jiandae leo mchana tunaenda kwa mchungaji hii hali si ya kawaida.
Ukapita mchana wote jioni imefika usiku saa 2 kasoro ndio nikashtuka OMG mbona hatukwenda kanisani kwa mchungaji? ? Nikamwambia dogo sasahivi vaa muache mtoto twende kanisani mara moja Kwani alijifungua kwa oparesheni. .na ndokwanza alikua anatimiza mwezi mmoja. Dogo akawa anasema aaahhh dada bwana usiku umeingia tutaenda kesho. .mimi roho ilikataa kabisa nikamlazimisha vaa twende anasema tutaenda kesho asubuhi dada roho iligoma kabisa nilisema hapana moyo wangu umegoma kulala leo bila kwenda kwa mchungaji huwezi jua .usiku mkubwa na roho haikubali kabisa kuacha kwenda
Akavaa tukaenda hapo saa mbili usiku..tukaenda hatukumkuta mchungaji tukamsubiri
Dada akamuhadithia kwa ufupi tu mchungaji akasema kwakua ni usiku wacha nimuombee kidogo ili awahi mtoto si akaanza kuomba troooobaaaa....
Dogo alikua kama wale wenye mapepo
NITAENDELEA KESHO NIKIPATA MUDA
Cc
Smart911
Sent using
Jamii Forums mobile app