Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

imani ya binti yako ni kubwa mkuu mtumie vizuri na kama akikua hivyo atawasaidia sana maana atakuwa kama mhimili wa familia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole Sana.
Mnahitaji maombi Sana..
Napendekeza muanze wenyewe kuomba..maana hakuna mtu atakuombea vizuri kuzidi unavyojiombea mwenyewe.

Maombi Ni silaha.
Mimi sijawahi shuhudia hayo aisee na sitamani kushuhudia,huwa najitahidi Sana kusali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh ninomaaa sanaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Madam mahondaw pole sana mkuu kwa mapito ya mdogo wako binadamu tunapitia mengi sana.....naomba umwambie mdogo wako kwanza afunge hata siku 1 huku akitamka mda wote Yesu naomba niguse, pia awe na nyimbo za kuabudu karibu nae mfano nyimbo 2 nilizoshuhudia ukuu wa Mungu ni HAUFANANISHWI wa Boaz danken NA NIGUSE (UKINIGUSA WEWE NITAKUWA SALAMA) YA glorious celebration......

Siku za kusali asubiri muda kutakako kuwa na utulivu kama sio muoga basi iwe usiku.....aandike mahitaji yake kwenye karatasi tu then awe anapiga magoti anavyosali karatasi aiweke chini mbele yake au akisimama awe ameisimamia karatasi yenye mahitaji yake...

basi atafute Luka 1:37, Yeremia 33:3 na mathayo 7:7-8..... asome hii mistari 3 na moyoni ajisemee Mungu naomba uniguse nahitaji kuona ukuu wako.... asali kwa mfano huu huku nyimbo ya kuabudu unaomba taratibu aanze kwa kuabudu kwanza

Asante Mungu wa rehema kwa upendo wako kwangu, najua mimi mkosefu na sistahili mbele zako Yesu wangu, naomba unisamehe dhambi zangu....nanyunyizia damu ya Yesu ya agano jipya ikanitakase dhambi zangu, mwili wangu, nafsi na roho yangu......

Neno lako katika luka 1:37 linasema hakuna linaloshindikana kwako nanyunyizia damu ya Yesu ya agano jipya juu ya maisha yangu na juu ya vifungo vyote vya kishetani nilivyofungwa damu ya Yesu ikanifungue na kuniweka huru.... Nanyunyizia pia damu ya Yesu kristo ya agano jipya juu ya familia yangu nikiomba ulinzi e Yesu wangu roho zote chafu juu ya familia yangu na mtoto wangu hazifananikiwa neno lako katika mathayo 7 linasema tuombe nasi tutapewa naomba ulinzi juu ya familia yangu Yesu...

Nanyunyizia damu ya Yesu kristo ya agano jipya iliyoamriwa na Mungu inene kwa ajili yangu juu ya nyumba nzima damu ya Yesu ikatupe ulinzi na kinga dhidi ya roho chafu na kama ilivyoandikwa katika ufunuo 12:11 kuwa nao wakamshinda kwa damu ya mwanakondoo basi natumia damu ya Yesu kristo kushinda hila zote za shetani na nguvu za giza...Amen

Ila kama anataka KUNENA kwa lugha hata kama hajaokoka ila anadhamiri ya kutaka kusema na Yesu(Mimi nilinena kwa lugha nikiwa sijaokoa)

basi atafute nyimbo ya kuabudu nashauri iwe Haufananishwi aiweke afatishe nyimbo yote aimbe akijisemea moyoni nahitaji uniguse Yesu....

then aianzishe alafu nyimbo inavyoendelea kuimba aseme tu Asante Yesu mara nyingi asiache akiona unaanza kuishiwa kama pumzi vuta pumzi na endelea kusema asante Yesu mara nyingi awezavyo ndani ya dakika 5 ataanza kunena kwa lugha( kwenye kunena kwa lugha japo atakuwa anaongea lugha ya kipekee moyoni mwake aendelee kusema mahitaji yake)

mfano mimi siku niliyonena kwa lugha sikuacha kusema Mungu nahitaji uponyaji wako na hapo sikuwa nimeenda kanisani kama miezi 5,

nilisali hivyo kwa hiyo njia ya kunena kwa lugha it happened nilinena kwa lugha muda mrefu sana na miujiza nikapata... kwa mtu mmoja mmoja namshauri asali kwa kunena kwa lugha ataona kazi ya Mungu inavyotendeka na hata kama muoga, akianza kunena tu Mungu atakupa ujasiri wa ajabu (Ninauhakika na hii fanya leo usijaribu Mungu atakuonesha ukiulizwa wake)

naimani itawafaa katika kusali Stopper3 Antonio de Guzman



Sent using Jamii Forums mobile app
 
alafu wachawi wengi huwa wanajificha kwenye dini ili waonekane watu wema....

Mara ya kwanza niliposali kwa kunena kwa lugha sikuamini Boss wangu ambaye ni Mama wa makamo na anayeonekanaga kashika sana dini kumbe behind anajua waliingia viapo na shetani (narudia waliingia viapo na shetani) ili watoto wawe hawafanikiwi katika eneo hilo eneo la kazi....na siku ya kwanza kuhudhuria ibada hiyo ijumaa(boss hakuwepo) tuluabudu na kusali tu na watoto... nikajikuta naanza kunena kwa lugha maana wakati watoto wanaabudu mimi nilijikita kusema asante Yesu mpaka leo naamini Mungu alinichagua mimi nibebe lile eneo kwa maombi,

Hilo eneo lilikuwa limejitenga kidogo na eneo la kazi, Nilivyorudi oficin nliendelea kunena kwa lugha zaidi ya saa zima, ilikuwa experience ngumu sana maishani mwangu nilioneshwa rohoni jinsi Boss na washirika walivyotoa kafara Vichanga kama miezi 7 au 8..... Happy ninavyonena kwa lugha roho inaniambia boss ndio mbaya

Boss alipigiwa simu na mtoto ikiwa saa 1 akacheka kwa dharau akasema mimi muongo..... but all in all Mungu yupo na anafanya kazi maana baada ya yale maombi viapo na shetani walivyoingia vilikuwa vinawalinda na kuwapa nguvu kiasi kilchofnya boss acheke kuwa mm mdogo kwake na nilipata kesi kubwa sana it was me going to jail for about 40 to 50 years ulimwengu wa shetani mbaya sana ila thanks God nilipona na sikufungwa japo kazi ilipepea maana dhumuni la shetani lilikuwa ni kuniondoa tu pale kazini waendelee kufanya hayo makafara......

Ila Mungu alivyo wa ajabu baada ya miezi michache tu nilipata connection ambayo niliomba Mungu apatikane mtu atakaenishika mkono kama alivyowapa wana wa Israel Musa... It happened nilikutana na black America mmoja around ninakokaa akanifanya mpango nikapata job yenye 100% salary rise....

Sio hivyo tu niliomba Mungu anifunge kwa mda nisijihusishe na Sex aiseh, kuna siku nimetoka kununua kinga kabisa nikawa nasema Mungu kama unanipenda naomba Nioneshe kitu chochote nisifanikiwe kwenye hili tukio..... akati narudi kutoka kununua kinga nilichokutana nacho kikanifanya niamini Mungu yupo....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
umenena vema sana kujiombea ni Muhimu na kuna nguvu zaidi mimi ninajiombeaga na huwa ninapata upako wa ajabu... Jaribu pia kusali kwa kuweka wimbo wa kuabudu kunakuwaga na nguvu zaidi....

But uoga wa nini mkuu? Jifunze kusali kwa kunena kwa lugha hautaogopa japo utaona mambo ya ajabu sana.....

Binafsi siku niliyosali kwa kuandika mahitaji kwenye karatasi na kuanza kusema tu asante Yesu huku wimbo wa haufananishwi ukiimba, nilikumbana na nguvu hatari zaidi za giza ila niliendelea kunena nikawa naoneshwa na roho nimuandikie mtu ambaye Yupo mlangoni amenasa kuwa Yesu hapendi hapo nikachukua peni na karatasi nikaandika nikamuandikia ghafla rohoni naona kuna mtu anasema niache it was tough na niliogopa kiasi kidogo ila kwakuwa nanena kwa lugha sikutishika.....

Nilimuangalia my mom ananituliza hapo kinywa kinashindwa sema nikawa naona naenda kufa basi namuangalia tu mama namshangaa natamani nimwambie kuwa Yesu tu ndo anaweza nipitisha usiku huu salama ila nikawa siwezi, nikaoneshwa mchawi wangu atajaribu kurudi na wenzie kwamba nimewakera hapo roho mtakafifu ndo ananipa taarifa ghafla tu nikaanza kulia sana nikamuandikia mama angu kwenye karatasi kuwa wale wabaya wangu wakirudia watakufa maana nilioneshwa watarudi huo usiku...

hapo saa 6 Yesu akanifunulia kuhusu hao watu kufa nilipata uchungu wa nafsi nikalia sana na hapo nikaomba Yesu asiwaadhibu kwa kuwaua wakishindana na nguvu zake, maana nitajihisi ninahatia ila niliona kabisa wakirudi basi asubuhi hawataamka hata mmoja.....

Muda nalala nikiwa naendelea kunena kwa lugha niliendelea kusali kwa moyo kuwa Yesu anakusudio gani namimi maana nilifunuliwa kuwa siwezi kufa maana ninaagano na Yesu na bado agano hilo halijatimia mpaka leo najiulizaga sana ninaagano gani na Yesu kiasi kwamba aliniokoa nisife usiku ule wakati mimi ni mtenda dhambi.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi pia huwa nasali kwa lugha na hakuna siku nilikuwa na nguvu Kama siku ya kwanza kunena.

Mkuu Sio kwamba naogopa... huwa sioni vitu na sijawahi kuona vitu live yaani moja kwa moja.
Huwa napewa kupitia mawazo au ndoto..unakuta Roho mtakatifu ananiambia ndani fanya Hiki,fanya kile, mwambie huyu hivi lakini sio muonaji wa vitu moja kwa moja.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama upo kwenye imani hizi za mitume na manabii wa kisasa za mafuta sitashangaa haya uliyonena

Ila Mungu hawezi kukufanyia ujinga huo iwe matangazo anao utaratibu wake maalum

Pengine una pepo la utambuzi ndani yako unalolifananisha na Roho Mtakatifu
 
daah haya mambo magumu sana..ila all ina ll Mungu yupo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kiwango hicho kinatosha maana ndicho Mungu alichoweka kwako mkuu na endapo kutatokea kitu ambacho Mungu atataka uone utaona tu.... Mungu aendelee kukupigania mimi nikinena kwa lugha ndiyo napata amani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu imani za mitume?? With all due respect ninamjua Mungu wa kweli na umewahi kunena kwa lugha?? Hiyo hali yangu ni hali ya kawaida sana tena ni kiwango cha chini kabisa kwa mtu anaenena kwa lugha.... na mchungaji ambaye anamshika mtu na kumwambia kama amefungwa kizazi labda na kweli ikawa hivo kumbe ni pepo wa utambuzi e??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh
 
hiyo hela ulitoa wapi ili urogwe? nenda bagamoyo katoe hilo dau halafu ulete majibu.
Kinachonishngaza juu ya hawa wanaodai hakuna uchawi/nguvu za giza hadi kufikia hatua ya kusema wanatoa dau ili warogwe,, hakuna kati yao ambaye amethubutu kwenda sehemu elekezwa (wanakopatikana wachawi) na kutangaza kwamba kama kuna mchawi amroge. Wengi wao wanaishia kusema mara watatekwa ama watadhuriwa physically kitu kinachoonesha kuwa wanajua hizi mambo zipo ila kwakuwa wako nyuma ya visimu na browser wahajifanya kupinga. Ikiwa hawaamini hili, wajaribu kwenda walikoelekezwa kisha walete mrejesho.
 
Amen Mungu ni mwaminifu sana, hiyo ilikuwa njia yako ya kumpokea Yesu vitu vya kuota ni vya kuombea sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unasemea kwao Smart911
 
Duh mambo nimoto, naomba unitafutie mchumba aliyeiva kiimani kama wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…