ndukulusudicho
JF-Expert Member
- Aug 14, 2017
- 501
- 768
Kwani hata waganga si huwa wanatabiri? Mtu kutabiri na mambo yakawa hivyo sio uthibitisho kuwa ana MunguMkuu imani za mitume?? With all due respect ninamjua Mungu wa kweli na umewahi kunena kwa lugha?? Hiyo hali yangu ni hali ya kawaida sana tena ni kiwango cha chini kabisa kwa mtu anaenena kwa lugha.... na mchungaji ambaye anamshika mtu na kumwambia kama amefungwa kizazi labda na kweli ikawa hivo kumbe ni pepo wa utambuzi e??
Sent using Jamii Forums mobile app
ila inategemea unatabiri kwa jina la nani na unatumia nini?? Kama mtu anatabiri kwa jina la Yesu hakuna shida kabisa.....maana hakuna uhusiano direct WA nguvu za nuru na gizaKwani hata waganga si huwa wanatabiri? Mtu kutabiri na mambo yakawa hivyo sio uthibitisho kuwa ana Mungu
Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo sidhani km atakua hai mpaka leo pengine ngoma ilishamchukuaMwaka 2005 hapo Tarime Secondary kuna jomba mmoja alikuwa ni classmate Msukuma huyo kutoka Magu ndani huko aliitwa Kija Charles.
Hiyo siku tupo prep, kuna mdada mmoja alikuwa na majini, akapandisha bana siku hiyo, watu taharuki, sasa yalivyokuwa yanazungumza yakamtaja huyo mlozi na alichotaka kumfanyia akashindwa. Kumbe yule jomba alishatomber dorm moja zima, la pili alikuwa kafika nusu, wadada wakaandamana kumtafuta huku kelele zikiwa zimetamalaki madarasani. Hakuonekana shule karibia wiki nzima.
Kumbe jamaa alikuwa anawatomber kichawi
Yupo anadunda freshHuyo sidhani km atakua hai mpaka leo pengine ngoma ilishamchukua
Duh, pole sana maandiko huwa unasoma kweli? Kwamba mtu akishataja jina la Yesu basiila inategemea unatabiri kwa jina la nani na unatumia nini?? Kama mtu anatabiri kwa jina la Yesu hakuna shida kabisa.....maana hakuna uhusiano direct WA nguvu za nuru na giza
Sent using Jamii Forums mobile app
Madam mahondaw pole sana mkuu kwa mapito ya mdogo wako binadamu tunapitia mengi sana.....naomba umwambie mdogo wako kwanza afunge hata siku 1 huku akitamka mda wote Yesu naomba niguse, pia awe na nyimbo za kuabudu karibu nae mfano nyimbo 2 nilizoshuhudia ukuu wa Mungu ni HAUFANANISHWI wa Boaz danken NA NIGUSE (UKINIGUSA WEWE NITAKUWA SALAMA) YA glorious celebration......
Siku za kusali asubiri muda kutakako kuwa na utulivu kama sio muoga basi iwe usiku.....aandike mahitaji yake kwenye karatasi tu then awe anapiga magoti anavyosali karatasi aiweke chini mbele yake au akisimama awe ameisimamia karatasi yenye mahitaji yake...
basi atafute Luka 1:37, Yeremia 33:3 na mathayo 7:7-8..... asome hii mistari 3 na moyoni ajisemee Mungu naomba uniguse nahitaji kuona ukuu wako.... asali kwa mfano huu huku nyimbo ya kuabudu unaomba taratibu aanze kwa kuabudu kwanza
Asante Mungu wa rehema kwa upendo wako kwangu, najua mimi mkosefu na sistahili mbele zako Yesu wangu, naomba unisamehe dhambi zangu....nanyunyizia damu ya Yesu ya agano jipya ikanitakase dhambi zangu, mwili wangu, nafsi na roho yangu......
Neno lako katika luka 1:37 linasema hakuna linaloshindikana kwako nanyunyizia damu ya Yesu ya agano jipya juu ya maisha yangu na juu ya vifungo vyote vya kishetani nilivyofungwa damu ya Yesu ikanifungue na kuniweka huru.... Nanyunyizia pia damu ya Yesu kristo ya agano jipya juu ya familia yangu nikiomba ulinzi e Yesu wangu roho zote chafu juu ya familia yangu na mtoto wangu hazifananikiwa neno lako katika mathayo 7 linasema tuombe nasi tutapewa naomba ulinzi juu ya familia yangu Yesu...
Nanyunyizia damu ya Yesu kristo ya agano jipya iliyoamriwa na Mungu inene kwa ajili yangu juu ya nyumba nzima damu ya Yesu ikatupe ulinzi na kinga dhidi ya roho chafu na kama ilivyoandikwa katika ufunuo 12:11 kuwa nao wakamshinda kwa damu ya mwanakondoo basi natumia damu ya Yesu kristo kushinda hila zote za shetani na nguvu za giza...Amen
Ila kama anataka KUNENA kwa lugha hata kama hajaokoka ila anadhamiri ya kutaka kusema na Yesu(Mimi nilinena kwa lugha nikiwa sijaokoa)
basi atafute nyimbo ya kuabudu nashauri iwe Haufananishwi aiweke afatishe nyimbo yote aimbe akijisemea moyoni nahitaji uniguse Yesu....
then aianzishe alafu nyimbo inavyoendelea kuimba aseme tu Asante Yesu mara nyingi asiache akiona unaanza kuishiwa kama pumzi vuta pumzi na endelea kusema asante Yesu mara nyingi awezavyo ndani ya dakika 5 ataanza kunena kwa lugha( kwenye kunena kwa lugha japo atakuwa anaongea lugha ya kipekee moyoni mwake aendelee kusema mahitaji yake)
mfano mimi siku niliyonena kwa lugha sikuacha kusema Mungu nahitaji uponyaji wako na hapo sikuwa nimeenda kanisani kama miezi 5,
nilisali hivyo kwa hiyo njia ya kunena kwa lugha it happened nilinena kwa lugha muda mrefu sana na miujiza nikapata... kwa mtu mmoja mmoja namshauri asali kwa kunena kwa lugha ataona kazi ya Mungu inavyotendeka na hata kama muoga, akianza kunena tu Mungu atakupa ujasiri wa ajabu (Ninauhakika na hii fanya leo usijaribu Mungu atakuonesha ukiulizwa wake)
naimani itawafaa katika kusali Stopper3 Antonio de Guzman
Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa bwana ulimwacha mke kwa kuwa kawa mbwa usiku mmoja tu km na yy alitumika na wachaw huoni km ulimuonea? au kuna tukio lingine lilijitokeza.Nikiwa na miaka Tisa ya ndoa yangu sikuwahi dhani wala kujua wife ni mchawi maana alikuwa msomi wa juu sana na mtu wa kanisa sana.siku moja nikiwa nimelala ulivuma upepo mkali mno gafla nikiwa macho nikajikuta nanyanyuliwa juu aisee nilisali sala zote gafla nikarudishwa chini.Kuangalia pembeni yangu alipolala mwenzangu naona mbwa aisee ulikuja kama usingizi hivi sekunde wife akarudi ktk hali yake ya ubinaadamu.Kesho yake nikahama home na ndoa ikafa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Leo nmepata muda ngoja nishuhudie na mimi jinsi nliumwa vitu vya ajabu...ilikua mwaka 2017 kuna sehem tulihamia mimi na mme wangu basi baada ya kuhamia eneo hili ambalo tulinunua kuepuka mambo ya kupanga sasa wakati tunafanya process za kununua tulitaka kufata sheria yaan kuuziana kupitia mwana sheria sasa mjumbe akawa amepigia mahesabu apate fungu hapa( hatukumpa hata senti) sasa tukawa tunafanya ukarabati kidogo maana lilikua gofu akawa anajifanya kuja kuzoa udongo mm nikawa nastuka uyu udongo wa nini lakin sikutaka kumwambia kitu wakati huo ashalalamika sana mtaani na kutangaza mbovu juu yetu nakuanza kutungombanisha na watu sisi tuliamua kukaa kimya...kashasha ikaanza usiku ukiingia nikawa naumwa magonjwa ya ajabu sana mara moyo kama unataka kuchomoka yaan nikawa nashindwa kupumua usiku tukawa tunakesha bila kulala hadi asubuhi nikiaenda hospital hakuna ugonjwa wowote nlizunguka hospital baadhi hakuna ugonjwa basi nikaanza kusali kidogo mwenyewe hali bado basi tukaamua kuhama na mme wangu tukahamia kibaha kulikua na nyumba ya bure cha ajabu kule nikawa nalala vizuri sana na siumwi kitu lakin tukawa tukirudi hapa tunapokaa ikawa naendelea kuumwa basi nakumbuka ilikua mwez wa 10 2017 nikaanza kuumwa tumbo yaan tumbo linavimba linakua kubwa afu gumu sana afu kila chakula nachokula naenda chooni kinatoka kama kilivyo yaan nikila wali hapohapo nikitoka kula naenda chooni wali unatoka kama ulivyo nikawa nikila chochote kinatoka ivyoivyo nikaenda hospital kupima sina ugonjwa wowote nikawa nampigia dadaangu ameokoka akawa ananimbea kwenye simu napata kaunafuu kidogo badae hali inaendelea palepale yaan nliteseka nlikonda sana ikafikia hatua nikaanza kutapika yaan nikila hata kama ni chungwa natapika huku nmevimba tumbo hasa mda mwingine naenda chooni huku haja kubwa huku natapika usiku silali nakesha nikienda hospital hakuna kitu sasa kuna sehem moja hivi nikaelekezwa kwenda kwenye maombi nikapewa namba za mtumishi hapo siwez kukaa siwezi kulala tumbo limevimba nahisi kufa yaan nlikua naenda kukata roho kabisa network zilikua zinakata kabisa nikawa nasali MUNGU anisadie yaan nikajikuta nmepata ka nguvu kidogo nikashika simu nikapiga namba ya mtumishi ikawa haipokelewi nikajua ndio nakufa hapo badae mme wangu akanibeba anipeleke hospital na hapo mm sitaki kwenda hospital roho ilikua inanituma nikienda hospital nakufa na nikamwambia kabisa mm naenda hospital ila siwez kupona nataka kwenda kwenye maombi ndio roho inanituma bade yule mtumishi nikamtumia msg kua na hali mbaya sijiwez naumwa nikiwa njian naelekea hospital ndio akanijib akaniambia tuko kanisan njoo tu ikabidi nikodi bajaji hadi walipo nlivofika nikaanza kuombewa nikadondoka nakumbuka nlivostuka niko chini yule mtumishi akaniambia usiku uliota nini nikamjibu nliota niko sehem afu nalishwa vitu vinanuka sana basi akachukua maji mapya kabisa akayaombea akaniambia kunywa hayo maji moyoni nimekata tamaa yakupona nikasema uyu ananipa haya maji ntapona kweli ila nikasema ngoja ninywe nlivokunywa yale maji nikasikia kutapika nikaenda chooni yaan nlitapika mavitu meusi kama mkaa mazito mno nikabaki nashangaa tu nikarud ukumbini nikayamalizia yale maji nikabanwa choo kwenda chooni nikajisaidia vitu vya ajabu sana nilivotoka chooni nikapona kabisa sikuamin macho yangu nikamshukuru sana Mungu kwakuniponya na yule mtumishi akaniambia nyumba ya pili upande fulani kuna mzee alikufanyia haya kwasababu fulani nikabaki namshangaa Mungu kua ni kweli huo upande kuna mtu wa hivyo na ni kweli tulikua na mgogoro yaan nlivorudi hme nikalala asubuh kuamka wakwanza kukutana nae afu akanikimbia yaan alinikimbia nikabaknamshangaa na tangu sikuile yule baba anaogopa hata kupita njia hii ya hapa kwangu na akiniona njian yeye anapita sehem nyingine ...najitahidi sana kusimama na Mungu tangu kipindo hicho sijawahi umwa hata maleria na hata kitu kibaya kikitaka kutokea najua na nasimama kukizuia na kinapita mtu mchawi akija kwangu namuona na wengi wananiogopa na nakili hakuna mchawi anaeniweza kwa sasa
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ubarikiwe pia na kama umesali hivyo nadhani umeona nguvu ya maombi ya kunena kwa lugha.... Be blessed
kila siku nasoma biblia jina la Yesu linanguvu sana na umefuatilia sala yangu hapo juu kwamba sijatoa usaliji wa maandiko.... but all in all Mungu ndo anajua na nina mengi sana ya kushuhudia ukuu wake sikuanza tu kumtafuta Mungu kwa kusoma biblia mkuu nimepitia vipindi vigumu sana maishani mwangu.......Duh, pole sana maandiko huwa unasoma kweli? Kwamba mtu akishataja jina la Yesu basi
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ubarikiwe pia na kama umesali hivyo nadhani umeona nguvu ya maombi ya kunena kwa lugha.... Be blessed
Sent using Jamii Forums mobile app
Ubarikiwe mkuu maisha yana vitu vingi sana.... Mimi kuna siku weekend kwenye saa 4 asubuhi bi mkubwa alianza kuumwa tu ghafla mwili mzima ulimuuma alizidiwa sana, alilia kama mtoto hapo yupo na dogo angu wa kike, alilalamika maumivu karibu saa zima alishinda anagaragara sakafuni.... na kuna kitu ni kama kilikuwa kinamkaba shingoni kuongea anaongea kwa tabu sana sauti ya kukoroma na kupumua kwa shida......
Naanza leo kuyafanyia kazi maelekezo yako kuna kitu kinanikwamisha sijui ni nn sijawah kua hivi zaman najiona naelekea kubaya
Sent using Jamii Forums mobile app
Amenkiwango hicho kinatosha maana ndicho Mungu alichoweka kwako mkuu na endapo kutatokea kitu ambacho Mungu atataka uone utaona tu.... Mungu aendelee kukupigania mimi nikinena kwa lugha ndiyo napata amani
Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi mwenyewe mpaka nilipopokea baraka nikiwa nasali kwa njia ya kuandika maombi ndio nikajua kuna nguvu sana....ubarikiweAmen
Nimejifunza kitu kutoka kwako..
"Kuandika mahitaji wakati wa kuomba"
Nilikuwa nachukulia kawaida tu ila kumbe ni njia nzuri.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hii njia yakuandika inakuwaje mpendwa? Au unaandika kile unachopenda Mungu akutendee? Samahan msaada hapoMimi mwenyewe mpaka nilipopokea baraka nikiwa nasali kwa njia ya kuandika maombi ndio nikajua kuna nguvu sana....ubarikiwe
Sent using Jamii Forums mobile app